Fungua
Tanzania Women of Action(Tawa)

Tanzania Women of Action(Tawa)

Dar es salaam, Tanzania

Katika majumuisho ya wiki hii,tumugundua sababu kubwa zinazosababisha migogoro isiyoisha inayoikumba serikali yetu ya  Tanzania.Hii ni kutokana na tabia za watanzania ambao wamezoea kulalamika bila kuchukua hatua,vile vile watanzania tuna kasumba ya kusahau.Kutokana na sababu hizi watanzania tuamke ,tuwajibike ,kwa kuchukua hatua kwa kufika mahali husika ,tupeleke ujumbe na hoja zetu  kwa  maandishi ili malalamiko yetu yawe na kumbukumbu ,kwani haki haipatikani bila kuipigania na hatima ya maisha yetu yapo mikononi mwetu wenyewe .

Wito wetu kwa asasi za kijamii ni kuwaomba tuwajibike kwa pamoja ili kuelimisha jamii {kuijengea uwezo jamii} kuanzia ngazi ya famili , mtaa n.k ili tuunde nguvu ya pamoja itakayoondoa    mifumo mibovu ya uongoziwa wa nchi yetu  ambayo insababisha matatizo yasiyo kwisha kwa kila sekta ,mfano  elimu ,afya. na nyingine nyingi.Kwa kuwajengea uwezo wananchi watadhibiti siasa katika sehemu za utendakazi.

4 Februari, 2012
« Iliyotangulia Ifuatayo »

Maoni (1)

Tanzania Women of Action(Tawa) (Hananasifu Kinondoni) alisema:
Kiashilia kikubwa cha maelezo hapo juu ni suala la mafuriko ,wananchi wameathirika na janga hilo lakini waliopata msaada ni asilimia ndogo sana na wahanga ambaaohawakufikiwa ,Keko, Mbagala ,Tabata , Tandale na maeneo mengineyo yamelalamika lakini hawakuchukua hatua yoyote hivyo kilio chao kubaki nacho wenyewe
4 Februari, 2012

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.