Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Tanzania women of Action Tawa inawatakia heri ya mwaka mpya  2013

On suturday 24th Tawa and other stake holders joined the 50 plus campaign which was organized by Tanzania 50 plus Campaign This campaign is coordinated by Dr E mannuel kandusi a prostate cancer survival ,and also a Managing director for Center For human Rights Promotion where 50 plus campaign is  one  of  its deprtment.During this event Tawa also contributed some items to support this campaign during its visit to cancer patient at Ocean Road hospital

             KWA NINI TUNAHITAJI USHIRIKI WA MWNAMKE KATIKA KATIBA MPYA?

Kwa kuwa tunahitaji katiba itakayokidhi matakwa ya mwanamke na mwanaume ,hivyo ushiriki wa makundi yote haya kwa uwiano sawa ni muhimu ili kuleta mabadiliko ya kweli na kupata katiba itakayosimamia  usawa, haki ,utu na heshima  ya wananchi wake bila kujali jinsia.

   Kutokana na changamoto hii na kwakuzingatia  idadi ya watanzania inayoonyesha kuwa wanawake wana idadi kubwa ikilinganishwa na idadi ya wanaume katika sensa iliyopita inayoonyesha wanawake ni asilimia hamsini na moja ( 51%  )ya watanzania wote ,Hivyo wanawake tunalojukumu la kuwahamasisha wanawake wenzetu walioko pembezoni  ili wajue umuhimu wa katiba ya nchi na waweze kujitokeza kushiriki katika mchakato wa kuandaa katiba mpya kwa kuchangia / kutoa maoni yao.

Tanzania Women of action (Tawa) tumefanikiwa kupata uwakilishi katika kongamano la wanawake na katiba liloandaliwa na Women Fund Tanzania(WFT) .Kongamano hili limefanyika kuanzia tarehe 22 mpaka 24  october mwaka huu na kuhudhuriawa na washiriki wanawake kutoka mikoa 19 ya Tanzania.Kwa ushiriki huo tumeweza kuweka mikakati ya pamoja ya masuala muhimu yanayo mgusa mwanamke ili yaingizwe  katika katiba mpya.

Katika utafiti Tunaoendelea kuufanya ,tumegundua masuala mbali mbali katika kundi la wanawake walioko pembezoni na kugundua kuwa ,ili wanawake tuweze kushika hatamu na kuleta mabadiliko ya kweli ni lazima tuyajumuishe makundi ya wanawake yaliyoko pembezoni.