TAARIFA YA KIKAO NA MAAZIMIO YALIYOFIKIWA KATI YA POVERTY FIGHTING TANZANIA NA TEYODEN
TAREHE: 02/10/2012.
LENGO LA KIKAO:KUJADILI NAMNA YA KUSHIRIKIANA KATIKA KUPUNGUZA UMASIKINI WA KIPATO KWA VIJANA KUPITIA MPANGO WA VICOBA KATIKA MANISPAA YA TEMEKE.
MAHALI KIKAO KILIPOFANYIKA:OFISI ZA PFT-TANDIKA MTAA WA KITUNDA PLOT NO:38,TEMEKE.
WALIOHUDHURIO:
- Issa Mohamed Tunduguru -PFT
- Hassan Mohamed Pwemu –TEYODEN
- Abela Kamulali -TEYODEN
- Yusuph Kutegwa -TETODEN
- Kasali Mgawe -TEYODEN
- Emmanuel Kwilasa - PFT
- Robert Duma - PFT
AGENDA ZILIZOJADILIWA/MADA ZILIZOJADILIWA
- KUANZISHA USHIRIKIANO KATI YA PFT NA TEYODEN KATIKA KUPUNGUZA UMASIKINI WA KIPATO KWA VIJANA
- TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA
- USHIRIKI WA VIJANA KATIKA VIKUNDI VYA UZALISHAJI MALI/VIKUNDI VYA KUWEKA NA KUKOPA/VIKUNDI VYA SHUGHULI ZA KIUCHUMI.
- MENGINEYO
Kikao kilifunguliwa na Mkurugenzi mtendaji wa shirika la POVERTY FIGHTING TANZANIA kwa kuwakaribisha wageni na kisha kutoa nafasi ya kujitambulisha kwa kila mjumbe aliehudhuria kikao.
Wajumbe wote walipata nafasi ya kujitambulisha na baada ya hilo,Mkurugenzi wa PFT alitoa nafasi ya kuendelea na agenda zilizokuwa mezani.
- KUANZAISHA USHIRIKIANO KATI YA PFT NA TEYODEN KATIKA KUPUNGUZA UMASIKINI WA KIPATO KWA VIJANA.
Agenda ya kwanza ilianza kwa Mkurugenzi kutoa maelezo kwa ufupi juu ya wito uliotolewa kwa TEYODEN kufika ofisi za PFT ili kujadili juu ya mambo muhimu kwa mstakabali wa vijana wa Tanzania hususan ni Manispaa ya Temeke.
Mkurugenzi alieleza namna PFT inavyoendesha programu ya VICOBA kama njia ya kukabiliana na umasikini wa kipato miongoni mwa jamii.Alieleza jinsi ambavyo programu hii imekuwa chombo cha kuwaunganisha wanajamii kupitia vikundi vyao vya vicoba ambapo hukutana kila wiki kwa ajili ya kununua hisa pamoja na mambo mengine kujadili masuala mtambuka kama vvu/ukimwi.
Lakini pia jinsi ambavyo familia zenye kipato cha chini kinavyoweza kumudu kujikimu katika maisha ya kila siku.Ilielezwa kuwa mfumo huu wa vicoba unawanufaisha wanakikundi pia katika kujifunza mambo yanayo husu maana ya vicoba na umuhimu wake kwa watu wenye kipato cha chini na hasa kwa wale wasio weza kumudu kupata mikopo kutoka katika taasisi za kifedha ambazo mara nyingi huhitaji kuwa na dhamana pamoja na mashariti mengine ambayo humfanya mtu wa kipato cha chini kushindwa kupata mikopo,ilielezwa namna mwana kikundi jinsi anavyonufaika na elimu ya utawala bora katika vikundi vyao vya uzalishaji mali,mambo ya kibenki na kujengewa uwezo katika mambo mbali mbali ikiwemo elimu ya ujasiriamali na namna ya kuendesha biashara ndogo ndogo na za kati.
Hata hivyo kabla ya kumaliza kutoa maelezo kwa kifupi juu ya programu zinazoendeshwa na PFT,mshauri mwelekezi wa PFT alipewa fursa ya kusoma takwimmu zinazoonyesha asilimia ya vijana waliojiunga katika mpango huu wa VICOBA unaoratibiwa na PFT.
Mshauri mwelekezi alitoa takwimu zikionyesha kwamba kati ya vikundi 115 vya VICOBA ambavyo tayari vimeshaanzishwa ni asilimia 32% ya wanachama vijana wenye umri wa kuanzia miaka 18-35 walio katika programu ya vicoba.Aidha ni asilimia 17 tu ya wanachama wa vicoba ambao ni wanaume.
Nafasi iliyotolewa kwa wajumbe kutoka TEYODEN ili waeleze shughuli za mtandao wa vijana.Katibu wa TEYODEN alieleza shughuli zinazofanywa ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya stadi za maisha kwa vijana,programu ya VVU na ukimwi,afya ya uzazi(Reproductive health),ujasiriamali kwa wasichana waliopata mimba za utotoni(Young mothers in financial involvement),kuwawezesha vijana kukabiliana na mazingira hatarishi na sanaa kwa maendeleo(SMK).Katibu wa mtandao aliendelea kueleza kuwa TEYODEN ina vituo vya vijana katika kila kata nk.
Hata hivyo TEYODEN walieleza jinsi ambavyo wamefanikia kuanzisha SACCOS ya vijana ambayo tayari imeanza kazi.
Mwenyekiti wa TEYODEN aliushukuru uongozi wa PFT kuwakaribisha na kupongeza kwa kufikiria na kuona inafaa kufanya kazi kwa pamoja na hasa kwa kuliangalia tatizo la vijana na umasikini.Alisema hili ni wazo zuri ambalo kwayo likitiliwa mkazo litakuwa ni moja ya njia ya kuwasaidia vijana wanaoelemewa na lindi la umasikini na ukosefu wa ajira.
Baada ya maelezo hayo kwa ufupi kuhusu kazi zinazofanywa na PFT na TEYODEN,wajumbe walikaribishwa kuendelea na mjadala ili kuona ni namna gani tunaweza kushirikiana kwa pamoja ili kuweza kuwashirikisha vijana kwa wingi katika kuunda vikundi vya kiuchumi na kuweza kuzitumia fursa zilizopo kupitia mbinu binafsi(Self initiatives).
Baadhi ya changamoto zilizotolewa na mjumbe kutoka TEYODEN alisema,Kuna haja ya kuangalia namna ya kubadilisha mtizamo wa vijana (Mind-set) ili ushiriki wa vijana katika mambo ya maendeleo uwe na tija,mfano alisema leo hii vijana wakiitwa kwenye semina ya kuwanufaisha wao bado kwa sehemu kubwa watataka walipwe,pasipo malipo huenda wasihudhurie kabisa au wasiendelee na semina,nyingine ni kwamba vijana wana fani zao lakini hawazifanyii kazi.
Mjumbe mwingine kutoka mtandao wa vijana alisema vijana hawana mitaji,vijana wanahitaji mafanikio ya haraka haraka,lakini pia kufuatia takwimu zilizopatikana kutoka PFT wakati wa zoezi la kutambua uwiano wa wanachama wa VICOBA kwa umri wao na jinsia zao (Sex and Age distribution),ilifahamika kuwa ni asilimia ndogo sana ya vijana walioko katika vikundi vya vicoba,je wengine wako wapi?je ni kwanini vijana wengi hawajiungi na makundi ya kichumi/uzalishaji mali?
Baada ya majadiliano marefu pande mbili kati ya PFT na TEYODEN wajumbe walikubaliana kuwa kuna haja ya kuanzisha ushirikiano wa pamoja kuitumia programu ya vicoba kama chombo cha kuwakwamua vijana kutoka katika lindi la umasikini wa kipato.
- TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA
Kufuatia wimbi la vijana wengi wanaoingia katika soko la ajira kuwa kubwa (angalia jedwali)
Residence |
Age Group |
||||
15-24 |
25-34 |
35-64 |
65+years |
Total |
|
Urban areas (Including Dar es salaam) |
9.3 |
3.0 |
1.0 |
1.1 |
3.7 |
Rural |
1.2 |
0.9 |
0.3 |
0.3 |
0.7 |
Total |
3.1 |
1.5 |
0.5 |
0.4 |
1.5 |
Source:Intergrated Labour Force Survey(ILFS) 2006 (NBS,2007 b)
Agenda hii ilizungumzwa kwa upana wake na wajumbe huku wakiangalia uwiano wa ajira katika sekta iliyo rasmi na sekta isiyo rasmi.Takwimu zinaonyesha sekta isiyo rasmi ndio inayotoa ajira kwa vijana wengi na kwa ujumla wake takwimu zinataja kuwa sekta isiyo rasmi inaajiri 63% zaidi ya ajira zilizo katika sekta rasmi,hivyo wajumbe walijadili namna gani vijana wanaweza kujiajiri au kuajiriwa katika sekta isiyo rasmi.
Changamoto zilizobainishwa na wajumbe ni pamoja na ukosefu wa mitaji,ukosefu wa elimu ya ujasiliamali,kutokuwa na sehemu rasmi za kufanyia shughuli zao,ushiriki mdogo wa kuunda vikundi vya kiuchumi/uzalishaji mali,Je ni kwa kiwango gani vijana wanashiriki katika kuandaa sera mbalimbali zinazohusu maisha yao kwa ujumla?na je ,ushiriki wa vijana wa kawaida katika masuala ya sera una umuhimu gani?vijana kuwa na mawazo ya kuajiriwa nk.
Wajumbe walijadili kwa kuzingatia uhalisia wa vijana ambao wengi wapo kwenye mtandao wa vijana kutokuwa na fursa za kushiriki katika shughuli za uchumi.
Maazimio
1) PFT na TEYODEN washirikiane katika kukuza ajira kwa vijana kupitia sekta isiyo rasmi,kwa kuunda vikundi vya kiuchumi/uzalishaji mali ili vijana wengi zaidi waweze kujiajiri,vikundi hivi vitajengewa uwezo kiuchumi kwa kuwashirikisha vijana katika vikundi vyao vya kiuchumi ili waweze kupata mitaji kupitia mikopo itakayotolewa kwenye vikundi vya vicoba.
2) PFT na TEYODEN iiombe idara ya vijana manispaa Temeke na ngazi ya wizara kushirikiana na wizara ya viwanda na biashara kuhamasisha vijana kuijua na kuitumia,sera ya maendeleo ya vijana na sera ya wajasiliamali wadogo na wa kati ili vijana iwawezeshe kuwapatia mwongozo na dira katika kutekeleza shughuli zao kwa ufasaha na pia kuifanya itumike ipasavyo.
3) Kuiomba wizara ya kazi na ajira iandae sera ya ajira na sheria za kazi kwa sekta isiyo rasmi ambapo vijana wengi wanaajiriwa huko.
4) Kuhamasisha matumizi ya mfuko wa vijana unaotolewa na serikali ili utumike kama chachu na nyongeza ya mitaji kwenye vikundi vya vicoba vya vijana vitakavyoratibiwa kwa ushitika kati ya PFT na TEYODEN.
5) Kuhamasisha urasimishaji wa shughuli/biashara za vijana/wanyonge ili ziweze kutumika kama dhamana ya mikopo kutoka vyanzo vingine vya mapato (Mkazo utawekwa kwenye kuhamasisha MKURABITA.
6) Kuimarisha mfumo wa mafunzo ya kuwajengea uwezo vijana katika stadi mbali mbali ikiwemo stadi za ujasiriamali,usimamizi wa fedha na biashara nk
7)
- Ushiriki wa vijana katika vikundi vya kiuchumi/uzalishaji mali
Kufuatia ushiriki mdogo wa vijana katika vikundi vya kukopa na kuweka,vikundi vya VICOBA wajumbe walijadili kwa kina ni kwa nini vijana wengi hawashiriki katika vikundi vya vicoba,vikundi vya kuweka na kukopa.
Baadhi ya sababu zilizobainika kutokana na majadilianao ya wajumbe ni kwamba vijana wengi wana haraka ya maendeleo ya ghafla,na hivyo kushindwa kwenda sambamba na mifumo mbali mbali ya kuweka na kukopa ikiwemo vicoba ambapo utaratibu huchukua muda kidogo hadi kufikia kuanza kukopeshana,hii hupelekea vijana kutokuwa na shauku ya kujiunga,kutokuwa na uvumilivu wa kuanza shughuli za uzalishaji mali/biashara kwa kianzio/mtaji mdogo,kukosa elimu ya ujasiriamali nk
Pia vijana wengi imebainika kutokuwa na habari hata juu ya mfuko rasmi wa vijana ambao ungeweza kusaidia kuwa chanzo cha fedha kutunisha mitaji yao ama kukopeshana kupitia vikundi vyao.
Kutokuwa na elimu ya kuunda vikundi na kuvisimamia,kujiendesha,kujua utawala na namna ya uchaguzi wa shughuli za kufanya za uzalishaji mali.
Maazimio
1) Kupanga mkakati madhubuti wa kuwahamasisha vijana washiriki katika vikundi vya kiuchumi
2) Kuandaa mpango maalumu wa mafunzo wa kuwajengea uwezo vijana ili wapende na waweze kushiriki katika vikundi vya uzalishaji mali.
3) Kuwaelimisha vijana juu ya kupanga mipango yao ya maendeleo kwa kuweka mipango ya muda mfupi,mipango ya muda wa kati na mipango ya muda mrefu.
4) Kuwafuata vijana huko waliko kwenye mitaa yao ili kuwapelekea mpango huu wa VICOBA itakayokuwa ni chombo cha kuwafanya wakutane kila wiki na kubadilishana uzoefu na mbinu na kuwa chachu ya wengine kuunda vikundi.
4.Mengineyo.
Agenda hii iliweka muafaka wa kukutana tena katika siku itakayo pangwa ili kuona hatua itakayofuata katika kupanga namna ya kuanza kutekeleza programu hii itakayo kuwa imejielekeza kwa vijana.
Ilikubalika kwamba kabla ya kuanza kazi italazimika kuandaa mkataba wa makubaliano(Memorandum of agreement) utakao eleza makubaliano hayo kati ya PFT na TEYODEN,Nini cha kufanya,mgawanyo wa majukumu na mambo mengine muhimu yatakayo saidia kutekeleza programu hii kwa ufanisi.
Mwenyeketi wa TEYODEN alifunga kikao kwa kuwashukuru wote waliohudhuria,namna michango ya mwazo na mijadala ilivyokuwa na tija na pia alishukuru PFT kwa kuleta wazo hili na hasa kuwashikisha TEYODEN.
Kikao kiliahirishwa mnamo saa 7:38 mchana mpaka hapo kitakapo itishwa tena.
VIJANA WATOA MAONI JUU YA UBORESHAJI WA SHUGHULI ZA VIJANA HASA UJASIRIAMALI.
Masuala ya msingi yaliyozungumziwa.
-Nini vikwazo vya wajasiriamali vijana wa Temeke?
-Tutawafundishaje vijana jinsi ya kuweka mafunzo wanayopata kwenye vitendo?
Maoni kutoka kwa vijana.
Vaijana walisema kuwa,Semina zinazotoleewa ni za kubabaisha na huwa zinatolewa bila kufuata mfumo maalum ambao utawawezesha vijana kupata elimu inayokusudiwa. Kwa mfano kama semina ni ya siku mbili huwa inatolewa kwa siku moja ili kubana matumizi.Kwa mfumo huu vijana hawezi kuelewa na kuona semina kama sehemu ya mafunzo mabadala yake ni sehemu ya kujipatia fedha.
Vijana walipendekeza kuanza na vitu vidogo kwa uwezo uliopo na kwa wakati huu ili shughuli za ujasirimali zikue taratibu na kwa uhakika.
Ili kukuza shughuli za mtandao na kuufanya uwe na vijana wengi,ungeafanyika ufuatiliaji wa shughuli za vijana ikiwemo Asasi ngapi za Temeke zinafanya kazi za vijana tuzialike kuleta vijana katika vikao vya mtandao.
Hata hivyo kuna haja ya kubadilisha mtazamo wa mafunzo badala ya kufanya mafunzo ili vijana wapate pesa ni vyema kufanya mafunzo ili kuwafanya vijana wenye mahitaji waelimike na wajitegemee.
Mmoja wa wachangiaji alitoa angalizo kuwa hakuna maendeleo yanayoanzwa na watu 100, watu/vijana wachache wenye moyo na waliotayari ndio watakaoweza kuwaonyesha vijana wengine kama maendeleo yanawezekana.
Ni vyema sasa kubadilisha mfumo uliopo na Kukubali mifano iliyopo na kuitumia ili kupenyeza ujumbe kwa vijana katika vitu wanavyovipenda: Mfano sanaa, michezo,jogging,picnic mashindano ya mpira na masuala mengine.
VIJANA (MDAHALO WA VIJANA)WATOA MAPENDEKEZO YA KUBORESHA SHUGHULI ZA MTANDAO WA VIJANA MANISPAA YA TEMEKE.
Vijana kutoka wastani wa kata 10 walikutana katika kikao cha vijana katika ofisi ya Mtandao wa vijana manispaa ya Temeke kujadili namna ya kuendeleza shughuli ya mijadala ya vijana ambayo hufanywa 2 kila mwezi ili vijana kubadilishana uzoefu na ujuzi juu ya masuala yanayohusu vijana.
Katika kikao tarehe hicho cha tarehe 21/7/2012 vijana walitoa mapendekezo juu ya namna ambavyo changamoto na zinazokabili vituo zinavyodhoofisha utendaji wa kila siku wa vituo vya vijana.
1. Ukosefu wa uelewa kwa viongozi waliochaguliwa ngazi ya kata juu ya stadi za uongozi na kuhusu mwelekeo wa utendaji kazi wa mtandao wenyewe.Jambo hili limeonekana kudhoofisha kata zote.
2.Ukosefu wa ofisi kwa vijana ngazi ya kata hali inayowafanya kukaa kwenye baa na ofisi za CCM jambo linalowanyima fulsa ya ushiriki vijana wa vyama vingine.Mfano kat ya Buza
3.Viongozi wa juu wa mtandao kuto tembelea vituo imeonekana pia kuwa moja ya changamoto hizo.
4.Vituo vya kata kutokuwa na tija kwa vijana kwa kuwa kila wanapokuja hakuna kitu kinachoshikika.
Mapendekezo juu ya nini kifanyike.
- Kutolewa kwa mafunzo kwa viongozi na wanachama wa vituo vya kata.mfano mafunzo ya ujasiriamali na stadi za maisha ambapo mkazo zaidi uwepo kwa vijana kujifunza kazi za mikono,ubunifu na ujuzi wa kazi za kuingiza kopato kwa vijana.
- Stadi za uongozi na wajibu wa viongozi katika kusimamia vituo.
- Mafunzo juu ya dira.madhumuni na na shughuli za TEYODEN ili kuwezesha viongozi na wanachama wa vituo kujua shughuli za mtandao kwa undani
- Kuboresha mfumo wa mawasiliano kwa kutuma msg na kupiga simu kwa viongozi na wanachama wa vituo ili kuwapa taarifa kwa kila shughuli inayoendelea katika Mtandao.
- Kuanzisha group ya mtandao kwenye face book ili kuwezesha upatikanaji wa taarifa kwa vijan a wanaoweza kupata taarifa hizi kwa haraka kupitia mtandao.
Programu ambazo zinatarajiwa kufanyiwa kazi kwa kipindi kijacho.
Uendeshaji wa mafunzo kwa vijana hasa katika maeneo ambayo wameyapendekeza lakini pia kwe ye eneo zima la utendaji na uboreshaji wa kituo cha vijana ngazi ya kata.
Utoaji wa taarifa za kazi kwa kila mwezi ili kusaidia kubuni mipango na miradi ya TEYODEN kwa kipindi kijacho.
Vijana wawakilishi wa vijana kutoka kata za Manispaa ya Temeke wakiwa katika mjadala wa pamoja katika ofisi za TEYODEN.
Vijana wakifuatilia kwa makini maelezo ya mratibu wa mdahalo wakati wa kikao cha vijana cha kituo cha vijana ofisi ya makao makuu ya TEYODEN.
PROGRAMU YA YOUTH INFORMATION CENTRE YAJA TANZANIA,DAR-ES-SALAAM IKIWA SEHEMU YA MAJARIBIO.
Wizara ya habari,utamaduni,vijana na michezo imepokea na kukubali mpango wa taarifa na habari kwa vijana utakaojulikana kama Youth information Centre.Mpango huu uliasisiwa ama kupendekezwa na bi Joyce Shahidi mkurugenzi msaafu wa Idara ya vijana ya wizara hiyo kwa alipokuwa kwenye kikao cha wadau nchini kenya miaka kama miwili iliyopita.
Programu hii inalengo la kurahisisha upatikanaji wa habari zitakazohusu nyanja mbalimbali za ustawi wa vijana hasa ukizingatiwa kuwa vijana ndio wahanga wakubwa wa changamoto nyingi za maisha.Hivyo kituo cha habari cha vijana kitakuwa kinajibu maswali ya vijana katika changamoto mbalimbali watakazo kuwa wanakabiliana nazo.
Kituo katika hatua za awali kitakuwa ni cha mfano kwa kuanzia katika wilaya za Temeke,Ilala na Kinondoni na kutakuwa na kituo cha taifa cha habari kwa vijana vyote vitakuwa chini ya wizara na Manispaa husika.
Wizara imeunda timu ya watu 7 kushughulikia mchakato wa uundwaji wa kituo hicho na kwa pamoja na wadau walihojiwa imeundwa timu ya watu 14 itakayotoa maoni juu ya namna gani kituo hicho kitakavyochukua sura ya vijana wa kitanzania.
TEYODEN imetoa uwakilishi wa vijana wawili katika timu hiyo ya mchakato wa maoni na kuchagiza uundwaji wa kituo hicho.
Vijana tuamke na kufuatilia juu ya fulsa hii muhimu kwetu.
Wadau 12 wa timu ya Uundwaji wa kituo cha Habari cha vijana wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa katika Hotel ya Peacock tarehe 12/7/2012.
Wadau wa timu ya Uundwaji wa kituo cha Habari cha vijana wakiwa katika mjadala wa pamoja wa namna ya kuanzisha kituo cha habari cha vijana katika Hotel ya Peacock tarehe 13/7/2012.
WAWAKILISHI 6 WA TEYODEN WAFANYA TATHMINI JIJINI ARUSHA NA WENZAO KUTOKA NEWALA,MAGU,HAI ARUSHA MJINI NA MWANZA MJINI KUMALIZA HATUA YA KWANZA MRADI WA WASICHANA WALIO PEMBEZONI.
Katibu mtendaji wa TEYODEN akiwa na wawakilishi wengine 5 wakifanya mjadala wa pamoja juu ya shughuli zilizofanyika,mafanikio,changamoto na mapendekezo katika mradi wa mabinti walio pembezoni.Kikao hiki kimefanyika katika ukumbi wa Kumbukumbu ya Azimio la Arusha.
Vijana wawakikishi wa mitandao 5 ya vijana wakiwa katika mitaa ya Arusha kujionea wenyewe uzuri wa jiji hilo la kitalii.
Vijana wawakikishi wa mitandao 5 katika picha ya pamoja chini ya mnara wa Azimio la Arusha.
TEYODEN YATOA MILINI SITA(6) KUSAIDIA VIKUNDI VYA WASICHANA WALIOJIFUNGUA KATIKA UMRI MDOGO.
Wasichana waliojifungua katika umri mdogo sasa wamepata fursa ya aina yake baada ya kukabidhiwa cheki zenye thamani ya milioni 2 kwa kila kikundi.
Akikabidhi cheki hizo mkuu wa wilaya ya Temeke katika ukumbi wa Amka youth aliwataka wasichana hao kuwa makini na pesa hizo na kwamba zitumike kwa miradi iliyokusudiwa ili kuwaletea tija katika maisha yao.katika risala yake mkuu wa wilaya ya Temeke aligusia pia suala la vijana kuwa na miradi ya kudumu ya kiuchumi na hasa masuala ya kilimo.Aliwataka vijana kutozarau kilimo na sio tu kilimo cha shambani kwa jembe la mkono lakini kilimo cha kisasa ambacho kinatumia mbinu za kitaalam.Alisisitiza kilimo mfano cha nyanya ni sehemu ndogo tu ya ardhi inaweza kutumika na ikazalisha nyanya nyingi.Hivyo vijana hao wa kike wakaweza kujiajiri wenyewe.
Katika risala yao kupitia mwakilishi wao Zakia wasichana hao waliojifungua kabla ya umri walimuomba mgeni rasmi kuwa mlezi wa vikundi hivyo.Pia waliiitaka jamii kuwaangalia wasichana wenye umri wao kwa umakini wasije kutumbukia katika matatizo kama yao na kuwaweka katika changamoto za kimaisha kama wanazozipata wao.
Mradi huu umefadhiliwa na Population Council, unasimamiwa naTAMASHA na unatekelezwa na TEYODEN.
MRADI WA MABINTI WALIOPEMBEZONI WATEMBELEWA NA MGENI KUTOKA MADAGASKA.
Mgeni wa kutoka Nchini Madagaska, Bi. Marium Toure ambaye ni Ofisa kutoka UNICEF Madagaska ametembelea mabinti ambao ni walengwa wa mradi wa kujenga uwezo wa mabinti waliozaa katika umri mdogo na kutulekezwa na wenzi/familia zao.
Mradi huu unatekelezwa katika kata 4 za Manispaa ye Temeke, kwa ushirikiano kati ya TEYODEN watekelezaji,TAMASHA wasimamizi na POPULATION COUNCIL wafadhili.Lengo hasa ni kuwezesha wasichana hawa kupunguza changamoto za maisha walizonazo na kuwaepusha na maambukizi ya V.V.U imeelezwa sana katika taharifa,magazeti na tafiti kwamba wasichana hawa wapo katika hatari ya kupata mimba nyingine na hata maambuziki ya ukimwi kwa kuwa katika mazingira hatarishi.
Katika mazungumzo ya kubadilishana mawazo na wasichana mgeni huyu ambae aliambatana na Richard Mabala ambae ni mkurugenzi wa TAMASHA aliwataka wasichana kutohuzunika kwa kuwa wapo katika maisha yenye changamoto nyingi.
"kuzaa sio kosa,ila tatizo ni umri wenu kuwa mdogo pamoja na hayo mlipaswa kuwa katika uangalizi wa familia na waliowapa mimba"alisema Bi. Marium.
Kwa mujibu wa Bi. Marium alieleza kuwa wasichana wa nchini ,Madagaska hawana programu kama hii zaidi ya progammu za kusaidia vijana hasa eneo la stadi za maisha na stadi za ujasiriamali.
Tatizo la wanajamii hasa vijana wa Madagaska ni kudai pesa kwa kila shughuli inayofanyika hata kama ina lengo la kuwasaidia wao wenyewe dhana ambayo anaishangaa sana kutoikuta kwa vijana wa Tanzania.
Marium alipongeza sana juhudi za TEYODEN na kusema kuwa wasichana wanatakiwa kutokata tamaa na kujichanganya kufanya hata kazi za kiume kama kuendesha bodaboda,kuosha magari na kazi nyingine ambazo zitawafanya kujipatia kipato na kupunguza umasikini.
Mwisho alimpongeza Bw. Mabara kwa kazi zake nzuri ambazo pia zimewasaidia vijana wa Madagaska.
TEYODEN YAFANYA MAFUNZO REJEA KWA MENTORS MRADI WA KUJENGA UWEZO WA KINAMAMA WADOGO WALIOSAHAULIKA.
TEYODEN imefanya mafunzo rejea ya siku 3 kwa mentors(walimu wa wasichana) 16 kutoka kata za Azimio,Kibada,Vijibweni na Mtoni.Mentors hawa hapo awali walipatiwa mafunzo ya satdi za maisha,elimu ya ujasiriamali na mafunzo ya uwezeshaji ili waweze kuwa walimu,waangalizi lakini kama walezi kwa wasichana 80 katika kata 4 za mradi kama zilizokwisha taja hapo juu.
katika tathimini ya TAMASHA iliyofanywa na mwakilishi wa TAMASHA katika Mradi huu bi Aziza ulikuta mapungufu kidogo kwa walimu hawa ikiwemo uwezo usiridhisha katika utoaji wa masomo kwa wasichana ngazi ya kata za mradi.Hivyo ufumbuzi wa haraka ulionekana ni kuwarusha katika mafunzo ya hatua ya pili ili kukazia hasa katika eneo la mbinu za uwezeshaji.
Mwisho wa mafunzo haya ya siku 3 wawezeshaji rika(mentors) walijiwekea mipango kazi yao ili kuwezesha kufanya kazi kwa urahisi na kwa mwelekeo wa pamoja.
Mategemeo ya TEYODEN ni kwamba wasichana wataboresha shughuli zao ili tuwawezeshe kupata mitaji ya kuanzisha na kuboresha shughuli zao za kiuchumi.
TEYODEN inategemea kuwapa kiasi cha sh 8,000,000/= sawa na sh 1,000,000 kwa kila kikundi.Kila kata inavikundi 2 vya wasichana 10 kila kimoja.
Apply to the YouthActionNet Global Fellowship Program!
Launched in 2001 by the International Youth Foundation, YouthActionNet strengthens, supports, and celebrates the role of young people in leading positive change in their communities. Each year, 20 exceptional young social entrepreneurs are selected as YouthActionNet Global Fellows following a competitive application process. The year-long Fellowship program includes:
Skill-building:
- A seven-day leadership retreat for twenty selected Fellows which offers dynamic peer-to-peer learning, collaboration, and sharing among young visionaries
- Focus on the personal growth and leadership abilities of Fellows, in addition to providing instruction in specific skills required to manage innovative, world-changing organizations
- Year-round learning opportunities based on Fellows' individual needs and the six dimensions of leadership highlighted in the YouthActionNet® Global Curriculum: Personal, Visionary, Political, Collaborative, Organizational, and Societal.
Networking and Resources:
- Membership in the YouthActionNet® global network of fellows and alumni
- Grant opportunities
- Opportunities to network and collaborate with IYF projects and partners
Advocacy:
- Training in areas such as communications planning, media outreach, message development, presentation skills, and innovative uses of new media technologies
- Access to global advocacy platforms and media coverage
Eligibility
- Open to all young people aged 18-29 (as of October 7, 2012)
- Applicants should be founders of existing projects/organizations, or leading a project within an organization.
- Proficiency in English is required; applications must be submitted in English
- Must be available to attend full retreat (all expenses paid) in the second week of October 2012.
Key Dates
- March 12: Applications must be submitted by 11:59pm on this day.
- March 28: All applicants will be contacted regarding the status of their application.
- May 22: Finalists will be notified
The 2012 retreat will take place during the second week of October 2012 inTurkey.
For more information visit:
http://www.youthactionnet.org/index.php?fuse=aboutfellowship
Kwa habari na taarifa kuhusu wilaya ya Temeke kama vile idadi ya watu kata na mgawanyo wa rasilimali na mengine mengi unaweza kutembelea website hapo chini ili kupata habari za kina na majibu ya maswali unayotaka kuyapatia majibu.