Fungua
Tanzania Albino Society

Tanzania Albino Society

Lindi Manispaa, Tanzania

Taasisi ya Watu wenye Ulemavu wa Ngozi - Tawi la Lindi au kwa lugha ya Kiingezreza Tanzania Albino Society (TAS) - Tawi la Lindi imetekeleza mradi wa Kujenga Uwezo na Uelewa kwa Watu wenye Ulemavu kuhusu Sera ya Taifa ya Walemavu kwa watu wenye ulemavu na wadau wengine kutoka katika Kata 5 za Manispaa ya Lindi. Kata hizo ni; Mingoyo, Ng'apa, Makonde, Ndoro na Msinjahili. Mradi umetekelezwa kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Januari hadi Machi, 2011. Mradi umeweza kuwafikia watu wenye ulemavu na jamii kiujumla wapatao 45 kutoka katika kata za utekelezaji wa mradi na hivyo kuongeza uelewa wa watu wenye ulemavu na jamii kuhusu Sera husika. Pia kuongezeka kwa ushiriki wa watu wenye ulemavu katika michakato ya Sera na Maendeleo. Mafanikio mengine ni kuboreka kwa mawasiliano na ushirikiano kati ya Viongozi na watendaji wa Serikali za Mitaa na Waandishi wa habari dhidi ya Watu wenye ulemavu.

Mradi huu umefadhiliwa na taasisi ya The Foundation for Civil Society ya Dar Es Salaam kwa jumla ya Fedha za Kitanzania zipatazo Milioni Nne Laki Tisa Sitini na Tatu (TZS. 4,963,000/=) tu. Mradi umefanikiwa pia kuongeza ari na hamasa ya watu wenye ulemavu kufahamu Sera na Sheria mbalimbali zinazolenga kulinda na kutetea haki na wajibu wao katika michakato ya Maendeleo. Aidha, TAS Lindi inatarajia kuendeleza jitihada za kuwajengea na kuwawezesha watu wenye ulemavu kiuwezo katika nyanja tofauti za; Kiuchumi, Kijamii, Kisiasa na Kiutamaduni kwa kutumia vyanzo tofauti vya raslimali ili kuhakikisha na kupelekea watu wenye ulemavu kuwa na ustawi na maendeleo endelevu.