The African Hope Community Organization {TAHCO}
Ni taasisi iliyoanzishwa tarehe 14th Feb 2014 na mwanzilishi akiwa ni ndugu Staphord Burren kwa kushilikiana na ndugu Elikana William Bugemwe kwa lengo la kuifikia jamii ya kitanzania na Africa kwa ujumla.
Lengo la TAHCO ni kutoa elimu kwa vijana,kupambana na ungezeko kubwa la watoto wa mitaani,kutoa elimu kwa waathirika wa ugonjwa wa ukimwi.
Hivyo basi tukiwa kama shirika tumeweza kufanya mambo baadhi na kufanikisha kwa mafanikio mazuri,tumeweza kutembelea baadhi ya vituo vya kulelea watoto yatima na kutoa elimu kwa vijana ambapo tulishirikiana vyema na UMATI tukafanya tamasha katika maeneo ya Mtongani kwa Aziz Ally Bank club ambapo tulifanikisha kwa kufanya vizuri na vijana wa pale wakaonesha moyo wa kushirikiana nasi.
TAHCO bado inaendelea kufanya mambo mengine mengi ambayo yanakwenda kufanikisha malengo yetu.