Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations
Mtoto Hassan Adam mwenye umri wa miaka 12 mkazi wa mtaa wa Itenzi. Nyumba namba IT/MW/669 kata ya Gombe jijini Mbeya amekuwa akinyanyaswa na kuchapwa mara kwamara na mama yake Bi Ashura Hassan na Baba yake  Bwana Adam Jemedari na kumpelekea kupata majeraha kutokana na kushindwa kwenda Madrasa na kunyimwa chakula zaidi ya siku mbili na akiwa analala chini bila godoro na shuka chakavu

Na hivyo kusababisha mtoto huyo kutoenda shule kwa zaidi ya siku za 7 kutokana na majeraha makali yaliyompelekea kushindwa kukaa. Ukatili huu dhidi ya watoto na haki za binadaamu.Kutokana na tukio hili mama yake mzazi ameamua kukimbilia mkoani Morogoro, eneo la Mang'ula

Mwenyekiti wa mtaa huo Januari Robert ameahidi kushughulikia suala hilo.
Samahani kwa usumbufu utakaojitokeza katika kuona picha mtandao umetatiza picha imeshindwa kuonekana kwenye ukurasa.
September 17, 2011
« Previous

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.