SCHOLARS FOCUS AGAINST SOCIAL MISERIES (SFASM).
RIPOTI MAALUM KUHUSU KIKAO CHA MRENGO (MTWARA REGION NGOs` NETWORK.)
MADA; TATHMINI YA KIWANGO CHA UFAULU WA WANAFUNZI WA DARASA LA SABA NA KIDATO CHA NNE MKOANI MTWARA.
Hivi karibuni MRENGO waliandaa mdahalo maalum uliohusisha wadau mbalimbali wa Elimu mkoani Mtwara mnamo tarehe 08/10/2011,kuanzia saa mbili asubuhi katika ukumbi wa chuo cha ufundi maarufu kama `Masandube` ambao ulichukua takribani masaa saba, ,pia viongozi mbalimbali walialikwa ikiwemo Wabumge,Madiwani,Walimu,Wazazi na taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali.
Mjadala;
Hapo awali Mwenyekti wa MRENGO alimkaribisha mgeni rasmi ambaye alikuwa Mkurugenzi wa manispaa mkoa,kisha afisa Elimu Mkoa aliwasilisha mada,hali ya maendeleo ya elimu Mkoani Mtwara,kisha azaki mbalimbali zilipewa fursa ya kuwasilisha mkakati mbadala wa kuimarisha ubora wa elimu mkoani Mtwara ikafuatiwa na majadiliano ya wadau wote juu ya nini tatizo na nini kifanyike ili kuiokoa hali ya elimu Mtwara.
Hata hivyo imeelezwa kuwa kiwango cha ufaulu hususan katika shule za msingi Mtwara kinazidi kushuka mwaka hadi mwaka kama kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa na Afsa Elimu Mkoa
Pichani (kushoto)ni mgeni rasmi Mkurugenzi wa Manispaa Mkoa akitoa hotuba juu ya maendeleo ya Elimu mkoani Mtwara, (kulia) Afsa Elimu wa mkoa wa Mtwara akitoa takwimu juu ya Elimu.
Matatizo yaliojitokeza;
Miongoni mwa matatizo yaliojitokeza ni;
-
· Utoro uliokithiri
- · Mimba (kwa wasichana)
- · Upungufu wa Walimu
- · Upungufu wa vifaa vya ufundishaji mfano Madarasa
- · Mtihani wa kidato cha pili kutokuwa na athari kwa wanafunzi
Changamoto zingine zikiwemo,Umaskini,Mfumo mbovu wa sheria,Upungufu wa miundombinu,Uhusiana mbovu kati ya walimu na wanafunzi,Ukimwi,Mshahara(kipato) mdogo kwa waalimu na Ajira kwa watoto.
Pichani ni Wanaharakati kutoka SFASM Bi Mdee Mwanaiza (kushoto) Bw.Living Anthony (Katikati).Bw Mahenge Godian (Kulia) wakichangia mada juu ya Elimu.
Majumuisho ya mwisho ya watoa mada;
Wajumbe waliombwa kutengeneza vikundi maalumu kwa ajili ya kufanya hitimisho la nini kifanyike,kisha viongozi wa vikundi hivyo walipewa fursa maalumu ya kuwasilisha kwa maelezo.
· Kuangaliwa tena kwa Sera na Sheria ya elimu nchini kwa ushirikishaji wa wadau mbalimbali wakiwemo wataalam
- · Kuimarisha ulinzi na Usalama hususani katika shule za bweni
- · Kuongeza kipato cha Waalimu
- · Kuboresha vifaa/dhana za ufundishaji
- · Kuboresha elimu juu ya mahusiano ya kimapenzi
- · Kuboresha mtaala wa elimu
Kuachana na Tamaduni na Mira potofu hususani zinazomkanadamiza mototo wa kike .
Pichani(kushoto) Wadau alipewa nafasi kuunda vikundi ili kujadili nini kifanyike kukabiliana na changamoto katika Elimu (Kulia) Wadau wa Elimu kutoka Asasi mbalimbali.
Hitimisho;
Mdahalo ulionesha kufanikiwa kwa kiasi fulani japo viongozi mbalimbali wa kiserikali walionekana kutoitikia mualiko huo mfano Wabunge na kwa mujibu wa mwenyekiti wa MRENGO kuwa hiyo ni hali inayojirudia mara kwa mara kwa viongozi wetu.Mijadala imekuwa ikitumika kufikisha ujumbe kwa jamii au wadau mbalimbali kama walivyofanya MRENGO,lakini bado kuna changamoto ya kutotimiza mikakati hiyo kwa vitendo.