Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations
Saidia Jamii kuishi (SAJAKU) ni Shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa rasmi mnamo tarehe 05/08/2007 na kusajiliwa tarehe 24 July 2008,Lilianzishwa katika kijiji cha Msangamkuu katika Halmashauri ya wilaya Mtwara,Lengo la kuanzisha shirika hili Kupambana na kupunguza umaskini wa KIPATO,UJINGA na MARADHI katika Mkoa MTAWARA,SAJAKU kwa sasa ina ofisi mbili moja ikiwa kule katika kijiji cha MSANGAMKUU na ofisi nyingine iko Mtwara mjini katika mtaa wa madukani na inatizamana na NSSF.