Envaya

large.jpg

Ni ndg. Hassan Luheko Mnaute, kiongozi wa OLAI, akisisitiza jambo la mwezeshaji katika mkutano wa hadhara wa uhamasizaji Ndg. Feruz kutoka idara ya ardhi ya wilaya Tandahimba, kuhusu kuizingatia sheria 5 ya ardhi ya vijiji ya mwaka 1999 katika kijiji cha Nachunyu kilichopo wilayani Tandahimba, mkoani Mtwara - Tanzania.

16 Januari, 2018
« Iliyotangulia Ifuatayo »

Maoni (3)

Hassan Luheko Mnaute (Kijiji cha Chaume, kata ya Chaume, wilaya ya Tandahimba, mkoa wa Mtwara - Tanzania.) alisema:
Organization for Land and Agriculture Improvement (OLAI) pamoja na malengo yake, inajishughulisha pia kuihamasisha jamii juu ya uzingatiaji wa sheria Na. 5 ya ardhi ya vijiji ya mwaka 1999, na kanuni za ardhi za mwaka 2002. Pasipo na ardhi hapana kilimo, hivyo ni jukumu letu wanajamii kushiriki kikamilifu katika kuzingatia sheria ya ardhi na kuwajibika katika utunzaji wa mazingira ili mazingira yatutunze na ardhi itupe maendeleo kwa manufaa yetu sisi na vizazi vijavyo. Tushirikiane pamoja.
17 Januari, 2018
Hassan Luheko Mnaute (Chaume wilayani Tandahimba - Mtwara, Tanzania.) alisema:
Ni wazi kuwa, hakutakuwapo mwanajamii ambe hatahitaji mabadiliko ili kuendana na mwamko wa wakati. Mazingira ni dira (Vission) ya kuiongoza jamii katika kupanga, kushiriki kwa kuizingatia mifumo ya matumizi bora ya ardhi ili kwa pamoja, kuuinua uchumi kwa ajili ya maendeleo yetu. Organization for Land and Agriculture Improvement (OLAI), inatoa msaada wa ushauri na uhamasishaji wa sheria Na. 5 ya ardhi ya vijiji ya mwaka 1999. Karibuni OLAI ili kubadilishana uzoevu.
23 Januari, 2018
Hassan Luheko Mnaute (Kijiji cha Chaume, Tandahimba - Tanzania. ) alisema:
Migogoro (Mashauri) ya ardhi katika jamii hii na mahala pengi nchini imesambaa. Hivyo ni muhimu kwa jamii kushughulika na uzingatiaji wa sheria ya ardhi, ili kukabiliana na migogoro inayojitokeza ndani ya watumiaji a namna yote kwa maana ya wakubwa, wa kati na wadogo. Kuizingatia sheria ya ardhi ni jambo muhimu kwa jamii, ili kupunguza au kuondoa kabisa migogoro ya Ardhi. Tupambane pamoja.
17 Agosti, 2021

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.