Ndg. Hassan Luheko Mnaute akifafanua jambo la mwezeshaji Mdg. Feruz kutoka idara ya ardhi, wilaya ya Tandahimba katika mkutano wa kupitisha mpango wa matumizi bora ya ardhi, wakati wa utekelezaji wa mradi wa kuwajengea uwezo wananchi, wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya vijiji na kata, kuhusu Sheria Na. 5 ya Ardhi ya vijiji ya mwaka 1999, na kanuni za Ardhi za mwaka 2002, katika ukumbi wa Parish holl uliopo Luagala, Wilaya ya Tandahimba mkoa wa Mtwara - Tanzania.
Ndg. Hassan Luheko Mnaute, mwenyekiti wa Organization for Land and Agriculture Improvement (OLAI)
Ni ndg. Hassan Luheko Mnaute, kiongozi wa OLAI, akisisitiza jambo la mwezeshaji katika mkutano wa hadhara wa uhamasizaji Ndg. Feruz kutoka idara ya ardhi ya wilaya Tandahimba, kuhusu kuizingatia sheria 5 ya ardhi ya vijiji ya mwaka 1999 katika kijiji cha Nachunyu kilichopo wilayani Tandahimba, mkoani Mtwara - Tanzania.
Aliyesimama na kipaza sauti ni Ndg. Hassan Luheko Mnaute, akihutubia katika mkutano wa hadhara wa uhamasishaji kuhusu Sheria Na. 5 ya Ardhi ya vijiji ya mwaka 1999 kwa wananchi wa kijiji cha Likolombe kilichopo Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba mkoa wa Mtwara - Tanzania, wakati wa utekelezaji wa mradi uliofadhiliwa na The Foundation for Civil Society (FCS).
Ndg. Hassan Luheko Mnaute, mratibu wa mradi wa kuwajengea uwezo wananchi kuhusu Sheria Na. 5 ya ardhi ya vijiji ya mwaka 1999, kwa ufadhili wa Foundation for Civil Society (FCS), mradi wenye thamani ya Tshs. 51,990,000/=