Kikundi hiki kimeanzishwa leo tarehe 6/2/2015 hapa GOLD CREST HOTEL, Baada ya wanakikundi kutafakari juu ya namna bora ya kuboresha hali zao za kimaisha na kuona kuwa kuna haja ya kuanzisha kikundi chenye malengo ya kujikwamua na maadui wakuu watatu yaani umasikini,maradhi na ujinga katika kujiletea maendeleo ya kweli kwa jamii yetu ya kitanzania bila kujali jinsia, kabila, dini, ulemavu na hata rangi. Baada Kikundi kuanzishwa kilianza mchakato wa kutafuta rasimali fedha kama mtaji kutoka kwa wanachama wake ambapo walikubaliana kuwa kila mwanachama atapaswa kutoa Mchango /Ada ya Tsh 40,000/= kwa kila Mwezi ili kukiwezesha kujijenga na kuanza kutekeleza miradi yake mara moja iwezekanavyo ili kusukuma gurudumu la maendeleo ya mwanakikundi na hata ya Taifa kwa ujumla. kikiwa na wanachama (7) saba ambao ni MICHAEL CHARLES, GRACE MASELE, FOCUS HIGHEST, BENEDICTO PAUL, LAMLATI YASSIN, REYMOND DOMINIC, NA JONAS MICHAEL.