Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations
Kuanzishwa kwa Asasi hii kumetokana na mawazo ya wanajamii wakulima na wafugaji ambao ni wadau wa utunzaji wa mazingira wanaoishi katika maeneo yanayojihusisha na kilimo cha zao la miwa katika Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.
Pamoja na ummuhimu wa zao la muwa kama mali ghafi ya utengenezaji wa bidhaa ya sukari lakini eneo zima la uoteshaji wa zao la miwa limekumbwa na uharibifu mkubwa wa mazingira.
zaidi ya hapo maeneo makubwa yamezungukwa na kilimo miti hususani aina ya mtiki.
Hivyo basi wanajamii waliamua kuunganisha nguvu za pamoja kuona kuwa wanashiriki katika hifadhi ya mazingira na uboreshaji wa misitu ya asili.