Log in
INTEGRAL ASSISTANCE TO VULNERABLE CHILDREN (IAVC)

INTEGRAL ASSISTANCE TO VULNERABLE CHILDREN (IAVC)

Zanzibar, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Jengo la kudumu kwa asasi mbalimbali

Timothy W. Philemon (Zanzibar)
May 30, 2011 at 12:25 PM EAT

Napenda kuzungumzia swala nzima linalozikabili asasi mbalimbali Nchini la kukosa majengo ya kudumu. Swala hili limekuwa tatizo kwa asasi nyingi hapa Nchini na kupelekea asasi nyingi kushindwa kufanya shughuli zake kwa ubora unaotakiwa, ukizingatia wafadhili wengi hivi sasa awatowi pesa kwa ufadhili wa ujenzi majengo ya ofisi. Je, swala hili mnafikiri nini kifanyake ili kukabiliana na tatizo nzima la majengo ya kudumu kwa asasi? Naomba mchango wa mawazo katika swala hili, kwa kuwa limekuwa tatizo kubwa kwa asasi nyingi hapa Nchini. Binafsi na kabiliwa na tatizo hilo kwa mda mrefu sasa, hadi nafikia kupoteza mwelekeo washuguli zangu.

Modest J.Mkude (Morogoro-WEETU)
June 9, 2011 at 1:17 PM EAT (edited March 26, 2012 at 8:06 AM EAT)

@Timothy W. Philemon (Zanzibar): 

Timothy umewaza vizuri saana juu ya kuwa na jengo la mashirika , ila tatizo Tanzania hadi sasa hatuna Mtandao wetu ambao utatuwakilisha ndani na nje ya nchi. kwanini nasema hivi tuliitegemea saana TANGO na NACONGO lakini mabo yapo kimya saana juu ya hili. FSC, UNGO na Mtandao wa Mkoa wa Arusha walianza safari ya kuanzisha mtandao/Apex kwa lengo la kuwa Mtandao wa NGO zote Tanzania hata hivyo shughuli hizo ziliishia na kuzimwa na baadhi ya NGO kuwa na waswasi kuwa watamezwa na mtandao huo na badala yake tukasema kuwa NACONGO iwe ndiyo Apex lakini kasoro yake ni kuwa inaishia ngazi ya mkoa tu na mapendekezo ya NACONGO kuanzia chini yalifanyika lakini hakuna kinachoendelea mpka sasa.Hivyo mimi naamini FCS bado ina nafasi ya kuendeleza Ule mchakato wa APEX ili tupate uwakilishi wa kweli katika ngazi za Kikata, kiwilaya,kimkoa, kitaifa na kiamataifa juu ya mambo yanayohusu maendeleo uwanaharakati Tanzania.

TIMOTHY W. PHILEMON (Zanzibar)
September 9, 2012 at 12:14 AM EAT

Kwanza samaani sana kwa kuchukuwa mda mrefu kujibu taarifa yako. Nashukuru sana kwa kunielewa. Mimi nafikiri mda umetimia wakuanganisha nguvu zetu ili tuweze kutatua kwanza swala la majengo ya ofisi ya kufanyia kazi. Tuendelea kufanya ushawishi kwa mashirika mengine yatuunge mkono katika wazo letu. Asante sana kwa mchango wako. kwa pamoja tunaweza. @Modest J.Mkude (Morogoro-WEETU): 

INTEGRAL ASSISTANCE TO VULNERABLE CHILDREN (IAVC)
May 19, 2014 at 10:00 PM EAT

Awali yote napenda kuomba radhi kwa kuchelewa kujibu. Kuhusu suala la jengo kwa ajili ya kufanyia. Sasa tunafanya nini ili tuweze kutatua tatizo hilo. Naomba muongozo wenu ili tuweze kuona uwezekano wa kusaidiana katika suala hii ambalo lime zikabili asasi hapa nchini kwetu.


Add New Message

Invite people to participate