Mkurugenzi mtendaji na Afisa mshauri wakiendelea na uandikaji wa majina ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Afisa mshauri wa asasi ya Bright Light akiwa katika zoezi la kuandika majina ya watoto yatima.
Afisa mshauri Kim Adiel (kulia) wa asasi ya Bright Light akielezea makundi ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi yatakayosaidiwa.
Afisa mshauri wa asasi ya Bright Light akielezea makundi ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ambao watasaidiwa.
Mkurugenzi mtendaji wa asasi ya Bright Light akitoa maelezo ya kina kwa wanafunzi wa shule ya msingi Mkoani jinsi ambavyo asasi ilivyodhamiria kuwajengea uwezo watu wenye kada mbalimbali wakiwamo watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Mwalimu wa zamu (kushoto), mkurugenzi mtendaji (katikati) na afisa mshauri (kulia) wa asasi ya Bright Light wakiwa katika zoezi la kubaini watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi katika shule ya msingi Mkoani hapa Geita.