Log in
Association of Zanzibar Salt Processing Organizations

Association of Zanzibar Salt Processing Organizations

WAWI CHAKE CHAKE, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations
Mashamba 5 ya chumvi ya majaribio (4 Pemba, 1 Unguja) yalidhaminiwa na mradi wa uzalishaji chumvi kwa kutumia miunzi ya jua mwaka 1997. Mradi huu wa miaka miwili (1997-1999) uliofadhiliwa na UNDP kwa mtazamo wa kupunguza umasikini ulilenga kuanzisha fursa za kujiajiri kwa makundi ya vijana na wanawake. Moja kati ya majukumu makuu ya mradi ilikuwa ni kuhakikisha kuwepo kwa chombo kitakachoweza kuendeleza juhudi hizo baada ya mradi kumalizika. AZASPO iliundwa na waanzilishi (waliokuwemo ndani ya mradi) matokeo ambayo baadae yalihamasisha makundi mengine ya wazalishaji chumvi. Mapema mwaka 2000 UNDP ilisimamisha ufadhili wake. Uwezo uliojengwa wakati wa kipindi cha mradi uliiwezesha AZASPO kuendeleza shughuli za uzalishaji chumvi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. Hivyo, ijapokuwa UNDP ilisitisha ufadhili, AZASPO inaenedeleza shughuli zilizoanzishwa na mradi kama ilivyokusudiwa