Bwana Lishela mtaalamu wa Samaki kutoka Mbegani akiwa tayari kupima maji kwa kuonyesha mfano kwa wanafunzi waliohudhuria mafunzo hivi karibuni hapa anajiandaa kupima kijani katika Maji tayari kutoa elimu katika shamba darasa la mmoja wa wanafunzi waliohudhuria mafunzo ya samaki mwaka mmoja uliopita.
Mtaalamu wa samaki Ndugu Kissai akitoa maelezo maalum kwa Consoltant na Mkurugenzi wa Open Mind ambaye alitembelea Bwawa la ndugu Kibona kwa ushauri wa maswala mbalimbali na yeye akawa miongoni mwa mtu aliyejionea fahari ya mtanzania kwa kutumia nyezo rahisi katika kujipatia lishe na kipato.
Hili ni Bwawa la samaki ambapo ndani mwake wapo samaki wapatao zaidi ya elfu nne hadi kumi
Samaki hawa wamekufa kwa kukosa hewa baada ya mfugaji kuzidisha kijani katika maji au mbolea na kusababisha maafa katika Bwawa.
Lakini mfugaji huyu ambaye ni Tunda la Africa Upendo Group bado anajishughulisha sana na ufugaji wa aina mbalimbali ikiwemo Samaki.Hili ni moja ya mabwawa yake ambayo yapo maeneo ya wazo na hapa Wataalamu kutoka Africa Upendo Group pamoja na Mbegani Fisheries wakiwa katika kupima maji ili kuona kama hewa inapatikana kwa wingi ili samaki wasife
Sio tu Ngombe lakini mkulima huyu Bwana Kibona anajishughulisha sana na ufungaji mbalimbali ikiwemo mifugo hii ya Nguruwe.Nguruwe ni kitoweo kizuri sana na pia ni biashara nzuri sana kwa mtanzania.
Mifugo ni mojawapo wa mihimili mikubwa hapa kwetu Tanzania kama itatumiwa vizuri kwa chakula na biashara.Ndama huyu amezaliwa muda sio mrefu katika mikulima huyu wa maeneo ya Tegeta Dar es salaam Bwana KIbona.