Log in
Chanika Tuamke Youth Organization (CTYO)

Chanika Tuamke Youth Organization (CTYO)

Ilala Dar Es Salaam, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

CHANIKA TUAMKE YOUTH ORGANIZATION (CTYO)

Ni shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa rasmi tarehe 13/03/2005 likijulikana kama Tuamke Arts Group na kusajiliwa tarehe 15/01/2014 Katika wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia na watoto na kupata namba 00NGO/00006839

Shirika linatekeza shughuli zake katika kata ya Chanika na Zingiziwa wilaya ya Ilala Dar es salaam.Lengo kuu la {CTYO} ni kuwawezesha vijana kushiriki katika mipango,kusimamia na kuitekeleza ili kuleta maendeleo Chanya.

{CTYO} Inafanya shughuli za Ushawishi na Utetezi katika kuhakikisha utekelezajiwa haki ya Afya ya uzazi kwa vijana,Uzingatiwaji wa Maadili,Malezi na Huduma bora ya rafiki kwa vijana.Pia CTYO imelenga kufanya uchambuzi wa sera mbalimbali za vijana na kusimamia utekelezaji wake.

Shirika la {CTYO} zamani Tuamke Arts Group kupitia mkurugenzi wake ndugu Seleman Nyonde limejifunza shughuli za Ushawish, Utetezi ,Uandaji wa Mpango wa kazi,Uandaaji wa Bajeti,Utunzaji wa kumbukumbu,Namna ya kuendesha Semina,Namna ya Uwajibikaji katika NGO na Kuandaa aTaarifa na Uwasilishaji wake. n.k Katika shirika la AMREF na SIKIKA kwa kupitia nafasi ya kujitolea.

DIRA

Kuwa na Vijana bora wanaoweza kupanga mipango,kuisimamia na kuitekeleza ili kujiletea maendeleo chanya.

DHAMIRA:

Kufanya ushawishi na utetezi kuhakikisha kuwa vijana wanapata Afya,Maadili,Malezi na Huduma bora Rafiki kwa vijana katika jamii na serikali kwa ujumla na kuchambua sera mbalimbali za vijana na kuhakikisha kuwa sera hizo zinakwenda na wakati na zinafanyiwa kazi.

MALENGO YA CTYO

12.1 Kuwajengea uwezo vijana kujiajiri wenyewe

12.2 Vijana kujikwamua kiuchumi

12.3 Kudhibiti maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi

12.4 Kukuza vipaji vya vijana katika sanaa na michezo.

12.5 Kuelimisha jamii juu ya Afya kwa vijana

12.6 Kuhakikisha kuwa vijana wanapata masilahi yao katika ngazi zote za serikali na jamii .

Latest Updates
Chanika Tuamke Youth Organization (CTYO) updated its Home page.
CHANIKA TUAMKE YOUTH ORGANIZATION (CTYO) – Ni shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa rasmi tarehe 13/03/2005 likijulikana kama Tuamke Arts Group na kusajiliwa tarehe 15/01/2014 Katika wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia na watoto na kupata namba 00NGO/00006839 – Shirika linatekeza shughuli zake... Read more
May 19, 2018
Chanika Tuamke Youth Organization (CTYO) created a Wafadhili page.
Chanika Tuamake Youth Organization (CTYO) kwa sasa CTYO haina Mfadhili ila Inaendeshwa na michango ya WWanachama na Tuna Miradi miwili 1.AFYA YA UZAZI KWA VIJANA. 2.TUTUNZE MAZINGIRA YETU. OMBI tunawaomba wadau mbalimbali wanao weza kutufadhili tunawakarinisha.
November 27, 2017
Chanika Tuamke Youth Organization (CTYO) added a News update.
Mikakati mbalimbali inaendelea juu ya kumsaidia watoto waishio katika mazingira hatarishi
July 30, 2017
Chanika Tuamke Youth Organization (CTYO) added a News update.
AFISA MAHUSIANO KCB BENK TAWI LA BUGURUNI ALIPOTEMBELEA OFISI CHANIKA TUAMKE YOUTH ORGANIZATION (CTYO) KATIKA MPANGO WAO WA KUTEMBELEA ASASI NA VIKUNDI MBALIMBALI VYA KIJAMII. Read more
June 20, 2017
Chanika Tuamke Youth Organization (CTYO) added a News update.
Karibuni Chanika tuamke youth organization (CTYO) Kujifunza masuala mbalimbali ya Afya ya uzazi kwa vijana
May 29, 2017
Chanika Tuamke Youth Organization (CTYO) added 2 News updates.
Jitihada bado zinahitajika katika kuhakikisha kuwa vijana wanapata elimu ya Afya ya Uzazi ili kuepukana na Changamoto mbalimbali zinazo wakabili Vijana.
May 18, 2017
Sectors
Location
Ilala Dar Es Salaam, Dar es Salaam, Tanzania
See nearby organizations