Log in
kijogoo group for community development

kijogoo group for community development

morogoro, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

TAARIFA YA UPOTEVU WA VOCHA ZA RUZUKU ZA PEMBEJEO ZA KILIMO KATIKA TARAFA YA GAIRO , WILAYA YA KILOSA.

KGCD katika kuendesha mradi wa uwajibikaji wa Serikali  kwa Umma, imebaini kupotea kwa Vocha za Pembejeo za Kilimo katika Tarafa ya Gairo Wilayani Kilosa katika Mkoa wa Morogoro zenye Thamani takribani Shilingi milioni arobaini na sita laki nne na elfu tisini (46,490,000) kwa Vocha 2214.

kati yake 1107 za kupandia na 1107 za kukuzia

Hata hivyo katika kata ua Chakwale Vocha zipatazo 2936 zikiwa za Mbolea ya kupandia na kukuzia.

hii ilitokana na mawakala kutoa mbegu za mahindi badala ya mbolea kwa kutumia vocha za Mbolea.

taarifa ya Ufuatiliaji imetumwa kwa Serikali ya Wilaya ya Kilosa, Ofisi ya Mkurugenzi, Ofisi ya Afisa Kilimo, Ofisi zote za Kata na Ofisi ya Afisa Tarafa Gairo kwa ajili ya kufanyiwa kazi.

Wakati wa ufuatilaji wa taarifa hizo viongozi na wafuatiliaji walinyimwa baadhi ya taarifa na kulazimika kuzitafuta kwa mbinu za ziada au kutumia Viongozi Mfano Madiwani na Afisa Tarafa.

USHAURI

Wajumbe wa Kikao cha Upokeji wa taarifa za Mwisho kilichofanyika katika Ukumbii wa SHule ya msingi Gairo "B" walikubaliana yafuatayo

1. waliohusika na upotevu huo hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

2. wananchi waelimishwe juu ya matumizi sahihi ya Mbolea na Mbegu

3.Mbolea na Mbegu ziwe zinafika kulingana na wakati kutokana na Jografia na Hali ya hewa ya   Eneo husika.