Log in
AFRICAN STUDENTS GOODHEART SOCIETY

AFRICAN STUDENTS GOODHEART SOCIETY

Muheza, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

MIRADI ILIYOTEKELEZWA NA ASGOHES

1. Mradi wa kuibua changamoto zinazowakabili wazee katika wilaya ya Muheza(Sensitization creation) 2006-2008.

Mradi huu ulitekelezwa katika wilaya ya Muheza ukizijumlisha kata za Mbaramo, Magila na Masuguru, ambapo katika vijiji vya Majembe, Mafleta,Mbaramo na Estate; jamii ilipewa elimu kupitia sanaa; mikutano na makongamano ambapo katika makongamano vijana na wazee walipata fursa ya kujadili changamoto zinazowakabili wazee na pia wajibu wa jamii na serikali za mitaa, serikali kuu na halmashauri zilizowekewa bayana wajibu na majukumu yao katika kuboresha maisha ya wazee kwa mujibu wa sera ya Taifa ya wazee.

2. Mradi wa vita dhidi ya VVU/UKIMWI kwa wazee 2007-2009.

Ukizingatia wazee ni kundi liliohatarini kusahaulika na jamii kabisa, ASGOHES, ilitekeleza mradi wa VVU/UKIMWI dhidi ya wazee, ambapo mpaka kumalizika kwa mradi katika awamu ya kwanza, jumla ya wazee 1505 walinufaika na mradi kwa kupata elimu juu ya kuwatunza wagonjwa wa UKIMWI majumbani. Kata zilizonufaika na mradi huu ni Mbaramo, Magila, Masuguru; katika vijiji vya Jembe na Mafleta. Aidha katika kata ya Masuguru shughuli za mradi zilijumuisha wazee wengi zaidi.

3. Mradi wa kuhudumia wazee majumbani 200-2009.

Mradi huu ulitekelezwa kwa kuwapatia huduma za mahitaji ya kibinadamu kama chakula, n.k. Pia ASGOHES ilitekeleza kazi ya ukarabati wa makazi ya wazee katika kijiji cha Jembe-Sega.

Mradi huu ulitekelezwa kwa njia ya kujitolea ambapo vijana ambao ni wanachama kutoka katika Shule za Sekondari walijitolea kuwahudumia wazee wapatao 257.

Wazee waishio katika mazingira magumu walinufaika na mradi huu. Aidha katika mradi huu ASGOHES iliibua changamoto nyingine zinazowakabili wazee kama kubaguliwa katika baadhi ya huduma za jamii ikiwemo afya.

4. Mradi wa elimu ya Ujasiriamali kwa wazee na mfano kwa vitendo 2009.

ASGOHES baada ya kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wazee, kwa kushirikiana na wazee 30 katika kitongoji cha Jembe, kata ya Magila; kilianzisha bustani ya mbogamboga ikiwa na lengo la kuongeza kipato kwa wazee na pia kutoa elimu ya kilimo cha mbogamboga kwa wazee wengine kutoka vijiji vya jirani.

Baada ya mradi kuimarika ASGOHES iliuacha uendelee kusimamiwa na kuendelezwa na wazee wenyewe.

Mradi huu ulivutia wazee wengi kutoka katika maeneo mengine ambao walipata elimu kwa njia ya vitendo juu ya kujiongezea kipato na kwa njia ya bustani za mbogamboga kwa kutumia mabonde yaliyopo yenye rutuba katika maeneo yao.