Log in
AFRICAN STUDENTS GOODHEART SOCIETY

AFRICAN STUDENTS GOODHEART SOCIETY

Muheza, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

ASGOHES - Tanzania ilianzishwa rasmi mnamo mwaka 2006 na hatimaye kusajiliwa rasmi November 2007 kwa namba 00NGO/0188.

ASGOHES - Tanzania ilianza mara baada ya kuona matatizo mbalimbali kwa wazee haswa umasikini na kwa kuzingatia mambo makuu muhimu yafuatayo ndiyo yaliyochochea kuanzishwa kwake ambayo ni;

i. Wazee ni moja ya makundi yaliyo hatari kusahaulika kabisa na jamii.

ii. Wazee ni kundi la watu masikini na wasio na sauti katika haki zao.

iii. Wazee ni kundi lililohatari katika kupata maambukizi mapya ya VVU/UKIMWI hii ni kutokana na kuwa wao ndio wauguzi katika jamii.

iv. Vijana na jamii kwa ujumla haina elimu juu ya wazee na haitambui chanagamoto zinazowakabili wazee.

v. Vitendo vya ukatili hswa mauaji ya vikongwe na kutoweka kwa UPENDO na mmomonyoko wa maadili miongoni mwa jamii inayowazunguka wazee.

vi. Uharibifu wa mazingira na vitendo vya rushwa na ufisadi nchini.