Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations
WAMATA ni shirika lisilo la kiserikali lenye makao makuu yae Daer saalam na lina matawi mengi. Tawi la WAMATA Sengerema ni mojawapo ya matawi 19 ya WAMATA yanayofanya kazi. Lilifunguliwa rasmi mwaka 1994, likijumlisha wanachama mbalimbali kutoka idara za afya, elimu, wakulima na wafanya biashara pamoja na walio na virusi vya ukimwi na UKIMWI.
Tulianza kuwahudumia watoto yatima12 kwa kuwapatia mahitaji ya msingi,fedha ilitokana na michango kutoka kwa viongozi wenyeye na fedha nyingine kutoka kwa kikundi cha kina mama wa kanisa.
Mwaka jana 2010 tumewasaidia watoto yatima mahitaji ya shule kama ifuatavyo:
- Shule za msingi [1300]
- Shule za sekondari [211]
- wanachuo walisaidiwa [11] HUDUMA YA CHAKULA: Mwaka 2010 Tulinunua mahindi gunia [8] maharage gunia[1] mpunga gunia [5] na unga lishe kwa ajili ya waathirika wa ukimwi na watoto yatima wanaoishi peke yao. watu 40 walinufaika na huduma hii. USHAURI NASAHA NA UPIMAJI huduma hii inatolewa na baadhi ya wajumbe wa kamati tendaji na wanachama kwa ujumla. KUSIMAMIA SHUGHULI ZA KUWEKA NA KUKOPA KWA WATU WAISHIO NA VVU/ UKIMWI. Tuna vikundi vitatu[ upendo 1&upendo 2,na tufarijiane] Mwaka jana tulishiriki katika matukio mbali mbali
- Maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani.
- Tulijumuika na watoto yatima kutoka asasi zingine kula chakula kwa pamoja 25/12/2010
- Mapambano dhidi ya malaria kwa kushirikiana na asasi ya TANDABUI Mwanza.
- Tuliendesha semina kwa viongozi wa madhehebu ya dini kuhusu kupunguza unyanyapaa kwa wenye vvu/ukimwi.semina ya malezi kwa watoto yatima na semina ya kupunguza unyanyapaa kwa wenye vvu/ukimwi.