Afisa Mipango na Mratibu Miradi wa shirika la Tanzania Women Social Economic Development and Human Rights Organization Bwana William Daudi amesema kwamba, shirika lake kwa sasa linatarajia kuendesha mradi wa kuongeza nguvu katika utekelezaji wa Sera ya maendeleo ya wanawake na jinsia ya mwaka 2000. akizungumza katika kikao cha Kamati kuu Mapema wiki jana, alisema kwamba shirika lake litatekeleza mradi wenye thamani ya shilingi arobaini na nne milioni na laki nane na hamsini elfu ( 44,850,000) ambapo kata sita zilizoko katika Wilaya ya Kigoma na kasulu zitanufaika. Ruzuku hiyo inatolewa na shirika la Foundation for Civil Society.
Aidha baada ya Taarifa hiyo, mratibu huyo kwa sasa yuko Dar es Salaam kuhudhulia kikao cha HUMAN RIGHTS AND BUSINESS NETWORK ambacho kinafanyika katika Hotel ya Peackock Hotel mjini Dar es Salaam. Aidha alieleza kwamba kikao hicho kitashughulikia masula ya kutiwa sahihi kwa katiba ya mtandao huo. pili kupitia joint proposal na mpango mkakati. aidha washiriki pia watapata mafunzo juu ya mbinu za kufanya fundaraising. Kikao hicho kitahudhuliwa na mashirika kumi (10) wanaanzilishi, na wataalamu toka Ulaya na kutoka MDF-ESA toka Arusha. Kikao hicho kitafanyika kwa muda was siku nne (4) ambapo kitaanza tarehe 17 hadi 20 january 2011.
Imetolewa na idara ya habari na Mahusiano
Kigoma Makao Makuu.