Base (English) | Kiswahili |
---|---|
Edit Design |
Hariri Mwonekano |
Comments
JIKWAMUE DEVELOPMENT ASSOCIATION,ITAHAKIKISHA KUYAFIA MALENGO YAKE,KWA KUTOA ELIMU KWA JAMII KWA NJIIA YA SEMINA,MIDAHALO MIKUTANO YA KUIHAMASISHA JAMII NA MAKONGAMANO YA WAZI
September 24, 2012 by JIDA
Katika harakati za kufikia malengo yEtu,JIDA imeshaandaa Mradi wa Mafunzo ya kuwajengea Uwezo wananchi wa Kata ya Lundi juu Mafunzo ya Mbinu za Ufuatiliaji wa Matumizi ya fedha za Ruzuku za Umma {PETS} zinazotengwa na Serikali kwa ajili ya maboresho ya Sekta ya Elimu katika Kata ya Lundi,Mradi huu umefadhiliwa na Foundation for Civil Society,Pia JIDA tumeshafanya mafunzo ya Kuwajengea Uwezo wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Kata ya Lundi na Wajumbe wa Kamati za Shule zilizomo katika kata ya Lundi juu ya Upangaji wa Bajeti,Kanuni na Sheria za simamizi wa fedha za Umma na Misingi ya Utawala Bora.Mradi huu pia umefadhiliwa na FCS.Mradi huu umefanikiwa sana sana,kwa upande wa Mradi wa mafunzo ya PETS,Wananchi wa Kata ya Lundi sasa wa uelewa wa kutosha katika ufuatiliaji wa fedha za Umma na wanaitumia mbinu ya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma kama ni Nyenzo yao endelevu si katika ufuatiliaji wa fedha za umma,bali pia wametambua kuwa Usimamizi wa Rasilimali za Umma ni jukumu lao,wamepata muamko wa kuhudhuria katika Mikutano ya Wananchi na kuhoji mapato na matumizi ya fedha wanazochangia katika kuboresha Elimu katika Kata na Vijiji vyao,Kwa upande wa Kamati ya Maendeleo ya Kata na Kamati za Shule wameweza kutambua kuwa njia pekee ya kufika katika mafanikio ni kuwajibika na kuwa wawazi katika utendaji wa shughuli zao za kila siku,Kutoa taarifa za mapato na matumizi na kuwashirikisha wananchi katika kupanga na kusimamia Miradi ya Maendeleo ya Sekta mbalimbali ikiwemo ya Elimu.
September 24, 2012 by JIDA
|
Translation History
|