Injira

Ubusobanuro: Kiswahili (sw): User Content: WIvk99qwgoT5X6JnCUNba3DP:content

« Inyuma   ·   Ahakurikira »
Base ((ururimi rutazwi)) Kiswahili

DSCN0643.JPG


Maoni ya Wadau wa Elimu kuhusu Bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliosomwa Bungeni 13 Agosti, 2012 - HakiElimu, Dar es Salaam.
HakiElimu inalitazama suala la elimu kwa kila mtu kama haki ya msingi baada ya haki ya kuishi, kwetu sisi elimu ndiyo haki pekee inayoweza kumsaidia mtoto au mwanadamu yoyote aweze kupata haki zake nyingine zote. Kwa sababu hiyo, HakiElimu inaamini kuwa suala la kupambana na changamoto zinazoikabili sekta ya elimu nchini si la kufumbiwa macho na ni jukumu la kila Mtanzania. 

Kama shirika linalojihusisha na utetezi wa haki ya kupata elimu, HakiElimu iliandaa na kufanya mkutano na wadau wa elimu mbalimbali uliyolenga kujadili hali ya elimu nchini, kufuatilia Bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya 2012/2013, ikiwasilishwa Bungeni  tarehe 13 Agosti, 2012 na kutoa maoni, mitazamo na ushauri juu ya bajeti hiyo na mwelekeo wa elimu kwa ujumla.

1.      Katika hotuba yake Waziri hajazungumzia kabisa mgomo wa walimu uliofanyika hivi karibuni. Hii inatia shaka kama serikali ina nia ya dhati kushughulikia kero na matatizo ya walimu. Kama serikali inataka kufikia muafaka na walimu na kuboresha ufundishaji ni lazima ikubali kuwa kuna tatizo na isikwepe wala kuona aibu kulijadili suala hili kwa uwazi. Aidha, Bajeti haina mkakati maalumu wa kuongeza ubora wa walimu ambao ni muhimu katika kuleta elimu bora. Serikali imeendelea kupuuza maslahi ya walimu huku ikikataa kukubali kuwa bila kukuboresha maslahi yao hawatafanya kazi kwa moyo.
 Mhadhiri-mwenzao-kutoka-Shule-Kuu-ya-Uan
2.      Waziri pia hakugusia vizuri suala la migomo ya wanafunzi vyuo vikuu ambayo mingi husababishwa na matatizo ya Bodi ya Mikopo. Ni muhimu kubadilisha mfumo wa utoaji wa mikopo; Bodi ya Mikopo iwe na matawi mikoani ili kurahisisha utoaji wa mikopo na kupunguza urasimu. Pia, katika kupunguza kero zilizopo kwa wanafunzi wasiokuwa na uwezo wa kujilipia masomo ya juu, Serikali ingekuja na mkakati wa kuwasomesha wanafunzi waliofaulu kwa kiwango cha juu. Hii ingekuwa tumaini kwa watoto wanaotoka kwenye familia masikini.

3.      Bajeti hii haina tofauti yoyote na ile ya mwaka jana kwa maana ya uwezo wa kutatua changamoto za elimu na hatutegemei mapya katika utekelezekaji wake. Bajeti haizungumzii kwa kina jinsi ya kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta ya elimu; haina upembuzi yakinifu wa matatizo na njia za kuyatatua. 

4.      Bajeti bado inatoa kipaumbele katika matumizi ya kawaida na kupuuza uwekezaji wa msingi katika elimu. Mathalani, katika makadirio ya bajeti ya takribani shilingi bilioni 724, ni shilingi bilioni 92.5 tu zilizotengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo katika elimu. Hii ina maana kuwa ni asilimia 13 ya bajeti itaenda kwenye shugghuli za maendeleo na zaidi ya bilioni 630 (87%) zimekwenda katika matumizi ya kawaida!
5.      Aidha, suala lingine lililojitokeza ni utegemezi mkubwa wa Serikali kwa fedha za wahisani katika kutekeleza miradi yake ya maendeleo. Katika Bajeti hii kati ya shilingi bilioni 92.5 zilizotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo, ni shilingi bilioni 18.5 (asilimia 20) tu ndizo zitatoka katika vyanzo vya ndani wakati shilingi bilioni 74 (asilimia 80) zinatarajiwa kutoka kwa wahisani! Utegemezi kwa wahisani wa kiwango kikubwa hivi ni hatari kwa maendeleo ya nchi yetu kwani kama wahisani hao watakwama kutoa misaada yao basi mipango yetu ya maendeleo  nayo itakwama 

Mhadhiri-wa-UDSM-Dk.-Kitila-Mkumbo.jpg

6.    Tumemsikia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akisema uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi umeboreshwa kutoka 1 kwa 48 hadi 1 kwa 46. Kwa juu juu, inaonekana tumefanya vizuri, kwani lengo letu ni kufikia uwiano wa 1 kwa 45. Lakini kuna angalizo; huu ni wastani na unaficha ukweli kwamba katika maeneo mengi watoto wanaweza kuzidi 50, 60 au 70 kwa mwalimu mmoja. Bajeti ikijaa maelezo yanayojikita kwenye kutoa wastani bila ufananuzi kuhusu hali halisi ni hatari sana kwani haitoi taswira halisi ya ama kukua,  kudumaa au hata kudorora kwa elimu nchini.
7.      Waziri ameahidi kwamba katika kipindi cha 2012/13, Wizara yake itaifanyia kazi sera mpya ya elimu; lakini, hajasema ni lini sera hiyo itakuwa tayari. Tunasistiza umuhimu wa kutimiza ahadi hii mapema kwani sera hii ndiyo itaongoza utoaji wa elimu Tanzania. Sera ya 1995 imepitwa na wakati na sasa ni serikali inapaswa  ije na sera mpya inayozingatia mabadiliko ya kiuchumi na dira ya maendeleo.
8.      Serikali imeendelea kutoa ahadi juu ya mpango mpya wa maendeleo ya elimu ya msingi awamu ya tatu baada ya ule wa awamu ya pili kumalizika 2010, lakini haielezi maandalizi yamefikia hatua gani na lini utakuwa tayari. Ni vema serikali ikaharakisha mpango huo ili kutoa dira kwa watekelezaji wa sera na bajeti za kila mwaka.
9.      Hotuba ya Waziri imeendelea kupuuza matatizo katika shule za kata hasa suala la kutokuwa na mabweni. Kuna athari nyingi sana za kuwa na shule umbali mkubwa kutoka makazi ya wanafunzi. Hii ni pamoja na wasichana kuwa hatarini kupata mimba n.k. Serikali haijasema wala kuonesha mkakati madhubuti wa kuyafanyia kazi matatizo kama haya.
10.  Alipokuwa akiongelea suala la ubora, Waziri alijikita zaidi katika kuongelea namna Wizara ilivyoboresha matokeo katika mtihani wa kuhitimu shule ya msingi, kutoka asilimia 53.5 hadi 58.3. Wakati kweli hili ni ongezeko, bado haliridhishi. Aidha, kumekuwa kuna tatizo kubwa sana kwenye ufaulu wa mtihani wa kuhitimu kidato cha nne kwani asilimia 90 ya waliofanya mtihani huu mwaka jana walipata div 4 au 0. Utoaji wa elimu bora ya sekondari utaisadia sana Tanzania kufikia malengo yake ya maendeleo kwani mwananchi anayeipata atakuwa na uwezo mkubwa wa kulinda afya yake, kujiendeleza kiuchumi na kujitambua. Hivyo, tunashangazwa na kushtushwa na ukimya wa Waziri kuhusu suala hili.
11.  Wakati tunatarajia kuandaa sera mpya ya elimu ni vema pia tukatafakari kuhusu suala la lugha ya kufundishia. Wakati ni muhimu kwa Mtanzania wa karne hii kukijua Kiingereza na ufundishaji wa lugha hii lazima uboreshwe, ni muhimu zaidi kuwafundisha watoto kwa lugha ambayo wanaielewa ili wapate ujuzi.
12.  Mwisho, wakati Wizara inapanga mikakati yake, ni muhimu kuwa na mpango madhubuti kuhusu wahitimu kwani kundi hili likikata tamaa kutokana na kushindwa kupata ajira n.k., linaweza kuleta mtikisiko mkubwa katika taifa.



(Not translated)

Kugirango ugire icyo uhindura kubyo wasemuye, ugomba kwinjira mu rubuga Injira · Iyandikishe