Base (Swahili) | Kiswahili |
---|---|
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ushetu, Wilaya ya Kahama, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Cherehani Emmanuel , leo Agosti 24, 2025, amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo. Cherehani ambaye aliteuliwa na Kamati Kuu ya CCM Taifa kupeperusha bendera ya chama hicho amepokelewa na kukabidhiwa fomu hiyo na Afisa Uchaguzi katika Jimbo hilo Charles Mburu. Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fomu, Cherehani amekishukuru Chama chake na wananchi kwa imani waliompa huku akisisitiza mshikamano ndani ya chama na kuondoa makundi ya makambi ili kujenga Ushetu yenye mshikamano na maendeleo kwa manufaa ya wananchi wote. |
(Not translated) |