Envaya

Translations: Kiswahili (sw): User Content: WIODSeA8VK86OFXf4z6tDwWb:content

Base (Swahili) Kiswahili

       

 

 KATIBA YA MFAWICA.

 

UTANGULIZI

 

TAFSIRI / TAMKO RASMI KWA NGO YA MFWICA.

TAFSIRI YA ASASI YA MFAWICA NI KWAMBA:-

  1. NI SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI
  2. NI SHIRIKA LISILOFANYA KAZI YA FAIDA BINAFSI
  3. NI SHIRIKA HURU KATIKA SHUGHULI ZAKE
  4. NI SHIRIKA LISILO LA KISIASA
  5. NI SHIRIKA LISILO LA KIDINI
  6. NI SHIRIKA LISILO LA UKOO, UKABILA, JINSIA MOJA, WAJANE, YATIMA N.K.
  7. NI SHIRIKA LINALOFANYA SHUGULI ZAKE KWA KUJITOLEA
  8. NI SHIRIKA LINALOFANYAKAZI KWA UWAZI, UKWELI, KISHERIA, TARATIBU NA KATIBA YA ASASI.
  9. NI SHIRIKA LINALOFANYA SHUGHULI ZA KIJAMII KWA MAENDELEO YA TAIFA NA DUNIA NZIMA.

 

HISTORIA

Shirika la MFAWICA lilianzishwa mwaka 2005 katika Kijiji cha Lubalisi – Kata ya Igalula, Tarafa ya Buhingu, wilaya ya Kigoma, Vijijini – Mkoa wa Kigoma ambao unapakana na :-

-         Nchi ya Burundi – upande wa Magharibi

-         Nchi ya Congo (DRC) – upande wa Kusini Magharibi

-         Mkoa wa Rukwa – upande wa Kusini

-         Mkoa wa Tabora – upande wa Mashariki

-         Mkoa wa Shinyanga – upande wa Kaskazini Mashariki

-         Mkoa wa Kagera – upande wa Kaskazini

 

Shirika lilianzishwa na wanachama kumi na moja (11) kwa lengo la kutunza mazingira, misitu na wanyama pori tokana na uzoefu wa kazi hiyo.

 

Uzoefu wa kazi hiyo ni kutokana na kufanya kazi ndani ya Hifadhi ya Mahale National Park, Kigoma.

 

Wanachama waanzilishi mwaka 2005 ni:-

  1. RAMADHANI NYUNDO SIKA
  2. BARAKA PETER NZOVU
  3. SILINDILA ATHUMAN KALIMBA
  4. SALUMU SHABANI KITOPENI
  5. MAKELELE MASANYUKE KAKOMO
  6. AKSA ANDREW CHAGAMBA
  7. MOHAMED HAMIS KALIMALINZA
  8. MOSHI HARUNA MADIGIDI
  9. BUHURU HAMISI BUTATI
  10. RAULENTI RICHARD GABRIEL

Wanachama wapya wa kujiunga mwaka 2009/12ni:-

  1. HAMISI ALMASI
  2. MWAMBA KIEMENA.
  3. ALEX EKAMA MNENE
  4. Simoni Patilo Bwilo
  5. Imani Richard Gabriel
  6. Issa Lufwifwi
  7. Simon Petro
  8. Laimond Simon
  9. Rajabu Juma Madolla
  10. Rajabu Kakumo
  11. Shabani Mussa Kibanga
  12. Mashaka Almas
  13. Shabani Kijungi
  14. Goodnes Issak Baziyaka

Shirika lilisajiriwa tarehe 10 Machi, 2008 na kupata Usajiri Namba OONGO/0436 inayotoa kibali kwa Asasi kufanyakazi katika eneo lote la Tanzania. Pia shirika linamiliki eneo la ekari 2000 zinazohifadhiwa kwa kutunza Maliasili zote zilizopo eneo hilo la hifadhi ya Milele Forest Kalobwa kijiji cha Lubalisi kata ya Igalula Kigoma Vijijini.

Lengo kuu la asasi ni kuona uharibifu wa mazingira, misitu, vyanzo vya maji, viumbe hai n.k. umepungua na kukoma kabisa. Na kuona hali ya umaskini na magonjwa yamepungua ndani ya jamii ya Watanzania mahali lilipo shirika na duniani kote. Na kuzingatia utaratibu mzima kama ilivyo tafsiriwa au tamko rasmi hapo juu.

 

BAADHI YA RASLIMALI ZILIZOPO ENEO LINALOHIFADHIWA NA MFAWICA:

WANYAMAPORI

Tembo, nyati, pongo, chui, sokwe mtu, nguruwe pori, nyani, kima, tumbili mwekundu (tusolima), ndugulungu (jamii ya kima), digidigi, mbuzi mawe, seuzi, mbubhu, swala, ngiri, panya n.k.

WADUDU

Vipepeo, panzi, nyuki, sisimizi, minyoo n.k.

NYOKA

Mamba pori, chatu, nyoka kamba, n.k.

NDEGE

Kwale, kanga, kiluwiri, kukutanda mdogo n.k.

MAHALI OFISI KUU YA ASASI ILIPO.

Ofisi ilipo ya Asasi ya MFAWICA ni Kijiji cha Rukoma kata ya Igalula, tarafa ya Buhingu, wilaya ya Kigoma vijijini mkoa wa Kigoma.

Ukiwa Kigoma Bandarini hadi Kituo cha Meli cha Rukoma penye ofisi kuu ya MFAWICA ni km.121 kwa kipomo cha GPS muda wa safari ya Meli ni wastani wa masaa 10. Kwa kutumia Boti za abiria kutoka Forodhani Ujiji ni wastani wa masaa 14 kufika Rukoma. Kwa usafiri wa ndege ni wastani wa dakika 30. Usafiri kutoka ofisi kuu ya Asasi ya MFAWICA Rukoma hadi kwenye Hifadhi ya

MILELE FOREST KALOBWA Kijiji cha Lubalisi –. Ni safari ya km zipatazo 30. Zaidi ya hapo Asasi bado inahitaji ujuzi, na vifaa kwa kupata taarifa sahihi zaidi.hifadhi hiyo yenye kufahamika kwa jina la milele forest KALOBWA ni moja ya juhudi zinazofanywa na Asasi ya MFAWICA kwa maendeleo ya Taifa na kimataifa katika kupambana na umaskini, magonjwa na usimamizi wa maliasili.

KATIBA

 

SEHEMU YA KWANZA

 

1.0 KATIBA

1.0   JINA LA ASASI :             MILELE FOREST AND WILDLIFE CONSERVATION

                                              ASSOCIATION (MFAWICA)

1.1     MAKAO MAKUU YA ASASI

KIJIJI CHA RUKOMA

KATA YA IGALULA

TARAFA YA BUHINGU

WILAYA YA KIGOMA (V)

KIGOMA, TANZANIA – AFRIKA MASHARIKI

1.2   OFISI NDOGO

IPO KATIKA ENEO LA UWANJA WA MPIRA LAKE TANGANYIKA

KATA YA RUSIMBI

TARAFA YA KIGOMA KUSINI (LAKE TANGANYIKA STADIUM)

KATIKA MANISPAA YA KIGOMA/UJIJI

1.3   MAWASILIANO

S.L.B. 35, KIGOMA

SIMU: +255 762 219605; +255 714 465053

Simu/nukushi; +255 28 2803976

EMAIL: mileleforest2007@yahoo.com/info@mfawica.org

TOVUTI: www.mfawica.org

1.4   ENEO LA UTENDAJI WA ASASI TANZANIA BARA

1.5   NEMBO YA ASASI

PICHA YA MNYAMA SOKWE JUU YA MTI

1.6 KUTAKUWA NA MATAWI NDANI YA TANZANIA BARA AMBAYO YATAKUWA NA MAMLAKA       YA KUJIENDESHA YENYEWE KWA KUFUATA KATIBA HII.

 SEHEMU YA PILI

2.0          LENGO KUU LA ASASI (DIRA)

2.1        KUONA HALI YA UMASKINI NA MAGONJWA NDANI YA JAMII YA WATANZANIA NA

   DUNIANI KOTE INAPUNGUA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA, UCHOMAJI MISITU

   VIUMBE HAI NA VYANZO VYA MAJI UNAKOMA KABISA

SEHEMU YA TATU

3.0           LENGO MAHUSUSI (DHAMIRA)

3.1  KUTOA ELIMU YA KUPAMBANA NA UMASKINI, MAGONJWA, UHARIBIFU WA

MAZINGIRA, UCHOMAJI MISITU, VIUMBE HAI NA VYANZO VYA MAJI KATIKA JAMII YA WATANZANIA NA DUNIANI KOTE.

                                                    SEHEMU YA NNE                                                   

4.0           SHUGHULI

4.1        UTOA ELIMU YA KUTUNZA MAZINGIRA YAWE BORA NA ENDELEVU KWA

   MANUFAA YA KIZAZI CHA SASA NA BAADAYE

4.2      KUTOA MAFUNZO YA KUTUNZA NA KULINDA VYANZO VYA MAJI KATIKA MAENEO

YA JAMII WALIPO WATANZANIA KWA KUBORESHA MITO, MABWAWA, MAZIWA,  VISIMA NA BAHARI KWA FAIDA YA WATANZANIA NA DUNIA NZIMA.

4.3       KUTOA ELIMU YA KUTUNZA NA KULINDA MISITU KATIKA MAENEO YA MISITU YA

   ASILI NA YA KUPANDIKIZWA KATIKA TANZANIA KWA KUELEZA SERA YA TAIFA YA

MISITU.

 

4.4       KUANZISHA HIFADHI YA MAZINGIRA,MISITU, VYANZO VYA MAJI NA VIUMBE HAI

   KATIKA MAENEO YA JAMIIKWA MALENGO YA KUTUNZA KI-UJUMLA KAMA MFANO

   KWA JAMII YA KITANZANIA NA DUNIA.

4.5       KUTOA ELIMU YA UJASILIA MALI KWA JAMII ILI KUJIONGEZEA KIPATO

KISICHOWEZA KUATHIRI MAZINGIRA, VYANZO VYA MAJI, MISITU NA VIUMBE HAI    ILI KUONDOKANANA UMASKINI KAMA NJIA MBADALA YA KULINDA MALI ASILI

4.6      KUANZISHA VIKUNDI VYA UZALISHAJI MALI KWA KUTOA ELIMU NA MAFUNZO JUU

   YA:- KILIMO, UFUGAJI KUKU, NYUKI, MABWAWA YA UFUGAJI SAMAKI, MIFUGO

NA VIKUNDI VYA KUWEKA NA KUKOPA NA KUTUMIA FURSA ZINAZOPATIKANA ILI

   KUONGEZA KIPATO NA KUONDOKANA NA UMASKINI, BILA KUATHILI MALI ASILI.

 

4.7      KUWEKA SHERIA NDOGO NDOGO KWA AJILI YA USALAMA WA MALI ASILI, MISITU,

   VYANZO VYA MAJI, MITO, MAZIWA, VIUMBE HAI WAISHIO KATIKA MAZINGIRA

   HAYO KWA JAMII KOROFI, SAWA SAWA NA MUJIBU WA SHERIA ZA NCHI.

4.8       KUSHAWISHI JAMII KATIKA MAENEO YANAYOFIKIWA NA UTENDAJI WA MFAWICA

         KUANZISHA MICHEZO YA JADI ILI KUIBUA UTAMADUNI WA MTANZANIA NA

         KUWA SEHEMU YA UTALII WA NDANI NA NJE YA TANZANIA NA KWA SEHEMU YA

        KIPATO.

 

4.9      KUJITANGAZA KWA MASHIRIKA MENGINE NA KUUNGANA KAMA MTANDAO ILI

   KUJENGA MAHUSIANO YA KARIBU KATIKA KUPAMBANA NA UMASKINI,  

   MAGONJWA, USAWA NA HAKI ZA BINADAMU HUSUSANI JINSIA NA WATOTO.

4.10   KUTANGAZA FURSA ZA VIVUTIO VINAVYOPATIKANA KATIKA MAENEO MBALIMBALI

   NCHINI NA KUKARIBISHA WATALII TOKA NJE KWA KUTANGAZA:- VYOMBO VYA

   HABARI, MAGAZETI, VIPEPERUSHI, MTANDAO N.K.

4.11     KUFANYA UTAFITI WA MALI ASILI KAMA VILE:- MIMEA AU UOTO WA ASILI,

   MADINI, WANYAMA PORI, WADUDU, NDEGE, JAMII YA NYOKA; HASA MAENEO

   YANAYOHIFADHIWA NA ASASI YA MFAWICA NA MAENEO MENGINE NDANI YA

   TANZANIA.

4.12   KUSHAWISHI NA KUSHIRIKIANA NA JAMII KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO KWA

   KUJITOLEA KUJENGA SHULE, ZAHANATI, BARABARA, MADARAJA NA KILIMO.

4.13    KUANZISHA VITALU VYAKUOTESHA MICHE YA MITI ITAKAYOPANDWA KATIKA

   MAENEO MBALIMBALI KAMA VILE MAKAZI, MASHAMBANI, KANDOKANDO YA

   MITO ILI KUBORESHA MAZINGIRA NA KUWA ENDELEVU ILI KUPUNGUZA UKAME

   NA HEWA CHAFU NA HATIMAYE MITI HIYO KUWA KITEGA UCHUMI KAMA VILE

   MBAO ZITAZARISHWA.

 

4.14    KUTOWA ELIMU YA KUPAMBANA NA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA VVU NA

   UNYANYAPAAJI WA WAATHIRIKA WA UKIMWI NDANI YA JAMII YA WATANZANIA .

4.15    KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU KWA

   KUWAPA MISAADA KAMA VILE ELIMU, MATIBABU, VIFAA VYA SHULE, CHAKULA

   PALE INAPOWEZEKANA NA KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU, WAFADHILI NA

   SERIKALI.

4.16   KUTOA ELIMU JUU YA MADHARA YA KUTUMIA MADWA YA KULEVYA KWA VIJANA

   JINSIA YAKIUME NA KIKE NA JAMII KATIKA MAENEO YOTE YANAYOFIKIWA NA

   ASASI (IKIWA NI PAMOJA NA KUPAMBANA NA UINGIZAJI AU UZALISHAJI WA

   MADAWA YA KULEVYA.

4.17   KUBORESHA ELIMUKWA WANA ASASI KWA KUGHARAMIA ELIMU SHULENI,

   SEMINA, WARSHA, KONGAMANO, VYUONI N.K. KWA GHARAMA ZA ASASI,

   WADAU NA PIA WAFADHILI WENYE KUPENDA MAENDELEO ILI ASASI KUWA NA

   UFANISI BORA, KIUTENDAJI

4.18  KUWA NA MFUMO WA ULINZI WA MALIASILI NA MALI ZA ASASI KWA KUFUATA

       SHERIA ZA NCHI KILA ITAKAVYOHITAJIKA.

SEHEMU YA TANO

5.0           IDARA:

SHIRIKA LITAKUWA NA IDARA AMBAZO ZITASIMAMIWA NA WAKUU WA IDARA KAMA IFUATAVYO:-

5.1  ELIMU NA MAFUNZO

5.2            AFYA

5.3 MAZINGIRA, MISITU NA VIUMBE HAI

5.4 MAHUSIANO, UTALII NA UTAFITI

5.5 MIPANGO KAZI, USHAWISHI NA UWAKILISHI

5.6  FEDHA

5.7  MAENDELEO YA JAMII

5.8 ULINZI NA UTETEZI WA SERA YA TAIFA YA MALIASILI

SEHEMU YA SITA

6.0  UANACHAMA

6.1  ASASI ITAKUWA NA WANACHAMA WA AINA MBILI MAKAO MAKUU NA MATAWI

(i)WANACHAMA WAANZILISHI

(ii)WANACHAMA WAPYA KWA KUOMBA

 

SEHEMU YA SABA

 

7.0 MASHARTI YA UANACHAMA

7.1AWE ANAJUA KUSOMA NA KUANDIKA

7.2 AWE NA UMRI KUANZIA MIAKA 18 NA KUENDELEA

7.3 AWE NA AKILI TIMAMU, TABIA NZURI NA NGUVU YA KUFANYAKAZI KIKAMILIFU

7.4ASIWE MWEHU, KICHAA, MWENDAWAZIMU N.K.

7.5AWE MLIPAJI ADA, MICHANGO INAYOPANGWA NA ASASI ILI KUIMARISHA MAJUKUMU YA MRADI/MIRADI KATIKA MUDA ULIOPANGWA.

7.6 AWE NA NIDHAMU NA MAHUSIANO MAZURI KWA WANACHAMA WENZAKE, WAFANYAKAZI NA WASIO WANACHAMA NDANI YA JAMII.

7.7 AWE MTIIFU KWA KUTEKELEZA MAAGIZO YANAYOTOLEWA NA VIONGOZI WAKE, KAMATI TENDAJI, MKUTANO MKUU WA ASASI HATA KWA KUTUMIA GHARAMA BINAFSI.

7.8 ASIWE MCHOCHEZI,VURUGU, MAJUNGU, UONGO, NDUMILAKUWILI AMBAPO AKIBAINIKA HATUA KALI ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE.

SEHEMU YA NANE

8.0           MASHARTI YA KUJIUNGA KWA WANACHAMA WAPYA NA KATIKA MATAWI YA ASASI

8.1  (i)  MTU ANAYETAKA KUWA MWANACHAMA MPYA WA MFAWICA ATAANDIKA

     BARUA KWAKATIBU MTENDAJI, AMBAPO KAMATI ITAANDAA MAOMBI YOTE

     NA KUYAPELEKA KATIKA MKUTANO MKUU KUPATA MAJIBU YA MAOMBI

     YAKE.

(ii) MAOMBI YALIYOFANYIWA UHAKIKI NA MKUTANO MKUU NA KUPITA WATATUMIWA FOMU YA MAOMBI NA WALE WALIOANGUKA WATATUMIWA TAARIFA YA POLE.

 

(iii)MWANACHAMA HUYO ATATAKIWA KULIPIA ADA, KIINGILIO KITAKACHOPANGWA NA MKUTANO MKUU WA ASASI.

 

8.2  ASASI ITAFUNGUA MATAWI TANZANIA BARA

 

(i)  ASASI ITAFUNGUA MATAWI MAPYA KATIKA KUPANUA WIGO WA SHUGHULI ZAKE.

(ii) TAWI LITAFUNGULIWA KWA KUANZA NA WANACHAMA KUMI (10)

 

(iv)              KILA MWANACHAMA ATALIPA ADA YA KILA MWEZI SHILINGI 5,000/= NA KIINGILIO CHA SHILINGI 100,000/=

 

(v)WATACHAGUA VIONGOZI WAO KAMA VILE:- MWENYEKITI, MAKAMU M/KITI, KATIBU, KATIBU MSAIDIZI, MHASIBU NA WAJUMBE WAWILI. LAKINI UONGOZI WA TAWI LOLOTE UTAKUWA CHINI YA UTAWALA WA VIONGOZI WA MAKAO MAKUU YA SHIRIKA.

8.3 UTARATIBU WA SHUGHULI

(i)TAWI LITAFUNGULIWA NA MWENYEKITI WA MFAWICA AKIWEPO KATIBU MTENDAJI NA MHASIBU NA MGENI RASMI ATAKAYEOMBWA KUHUDHURIA KAMA MFUNGUZI WA TAWI HILO N.K

(ii)TAWI LITAFANYAKAZI KWA MAELEKEZO YA MAKAO MAKUU TU, NA SI VINGINEVYO.

(iii) VIKAO VITAFANYIKA KAMA ILIVYO KATIKA SEHEMU YA NNE YA KATIBA YA MFAWICA

8.4 MASHARTI YA KUJIUNGA UANACHAMA

(i)KUJIUNGA ITAKUWA KAMA ILIVYO SEHEMU YA NANE YA KATIBA KIF. 8.0; 8.1 (i) – (iii) NA 8.2 (iii)8.5 MASHARTI MENGINE

(i)  KILA MWANACHAMA ATAZINGATIA VIPENGELE HUSIKA NDANI YA KATIBA YA MFAWICA

SEHEMU YA TISA

9.0          HAKI NA WAJIBU WA MWANACHAMA

9.1  KUCHAGUA / KUCHAGULIWA KUWA KIONGOZI KWA WADHIFA WOWOTE KATIKA ASASI

9.2KULINDA NA KUTETEA KATIBA, MALI, MIONGOZO NA KWA KUTUMIA SHERIA YA NCHI.

9.3KUPATA TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI YA ASASI

9.4KUWA NA MOYO WA KUJITOLEA KIFEDHA, MALI NA NGUVU PALE INAPOBIDI BILA KULAZIMISHWA.

9.5            KUWA MWADILIFU NA MKWELI KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YA ASASI.

9.6 KUHUDHURIA VIKAO VINAVYOKUHUSU KWA MUJIBU WA KATIBA

9.7KUTOPOKEA RUSHWA AU KUTOA RUSHWA KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MFAWICA

9.8            KUSHIRIKIANA NA WENZAKE, VIONGOZI NA JAMII KATIKA KUTENDA SHUGHULI ZA MFAWICA KAMA ZILIVYOAZIMIWA.

9.9KUSHIRIKISHWA KATIKA JAMBO LA MAAMUZI KWA MUJIBU WA KATIBU, KAMATI TENDAJI NA MKUTANO MKUU

9.10 KUHESHIMU MAONI, MAWAZO, USHAURI, MAPENDEKEZO YA KILA

MWANACHAMA NA KUYAFANYIA KAZI.

9.11KUTAFUTA MISAADA YA KIFEDHA NA MALI AU VIFAA KUTOKA KWA WAHISANI,

       SERIKALI, WADAU NDANI NA NJE YA NCHI KWA MANUFAA YA ASASI NA JAMII.

 

9.12  KUPATA/KUPEWA NAFASI YA KUJITETEA KWA KIONGOZI, KAMATI TENDAJI,

       MKUTANO MKUU NDANI YA ASASI TOKANA NA KOSA AU TUHUMA PALE

     INAPOBIDI KWA MAELEZO, USHAHIDI NA VIELELEZO.

 

9.13 KUKOSOA NA KUKOSOLEWA KATIKA VIKAO KWA MUJIBU WA KATIBA YA

       MFAWICA NA HATIMAYE KUONYWA, KUSHITAKI AU KUSHITAKIWA

     MAHAKAMANI.

 

9.14 KUEPUKA MALUMBANO KATIKA ASASI KWA UONGO, UZUSHI, UMBEA,

       UCHOCHEZIKWA NAMNA YOYOTE ILE.

 

9.15.KUHESHIMU MAAMUZI YANAYOTOLEWA NA VIONGOZI, KAMATI TENDAJI, NA

     MKUTANO MKUU.

9.16.KUTANGAZA KAZI ZA ASASI NA KUZITETEA SEHEMU MBALIMBALI I.E. MASHIRIKA,

     SERIKALINI, TAASISI ZA DINI, WARSHA, MAFUNZO NA SEMINA N.K.

 

9.17.KUSAMBAZA VIPEPERUSHI VYA MATANGAZO YA MFAWICA KATIKA MAENEO

       MBALIMBALI NA KUTOLEA MAELEZO/UFAFANUZI.

9.18. KUITAMBUA KATIBA KWA KUISOMA MARA KWA MARA

9.19.KUBEBA DHAMANA KWA JANGA LOLOTE LITAKALOTOKEA KATIKA ASASI.

SEHEMU YAKUMI

10.0       UKOMO WA UANACHAMA

10.1 KUHAMA ENEO LA MBALI NA ASASI ILIPO NA KUSHINDWA KUWAJIBIKA.

 10.2         KUSHINDWA KULIPIA ADA MIEZI MITATU MFULULIZO BILA TAARIFA/SABABU ZENYE USHAHIDI WA KUTOSHA.

 10.3.KUSHINDWAKULIPA MICHANGO YA KIMAENDELEO KWA MUJIBU WA KATIBA NA MAAGIZO YA MIKUTANO HUSIKA.

10.4.KUANDIKA BARUA KUOMBA KUJIUZULU KWA MWENYEKITI AU KATIBU

10.5.KUTOHUDHURIA VIKAO VITATU MFULULIZO VINAVYOKUHUSU KWA MUJIBU WA KATIBA

10.6.KUFUKUZWA

10.7 KWA HUJUMA AU WIZI WA MALI ZA ASASI NA KUSHITAKIWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.

10.8  KUUGUA UGONJWA WA AKILI, KICHAA, WEHU NA KIFO

10.9 KUFUNGWA BAADA YA VYOMBO VYA SHERIA KUTHIBITISHA KIFUNGO TOKANA NA JINAI NA SHIRIKA

10.10 KUUGUA MARADHI YA MUDA ZAIDI YA MIEZI SITA NA YALE YASIYOPONA KAMA UKIMWI (PALE ASIPOWEZA KUFANYA KAZI

10.11   KWA MUJIBU WA KIF.10.1 HADI 10.10 HAKUNA MWANACHAMA YEYOTE MWENYE HAKI YA KUDAI KITU CHOCHOTE TOKA KATIKA ASASI HATA HAKI YA KUOMBA UANACHAMA TENA.

SEHEMU YA KUMI NA MOJA

11.0         UCHAGUZI NA MUDA WA UONGOZI

11.1UCHAGUZI UTAFANYIKA CHINI YA USIMAMIZI WA KAMATI RASMI YA UCHAGUZI

     ITAKAYOPANGWA NA KUTEULIWA NA MKUTANO MKUU WA ASASI.

11.2UCHAGUZI UTAFANYIKA KWA WAGOMBEA WALIOTIMIZA MASHARTI KATIKA FOMU NA KUREJESHWA KWA MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI NDANI YA MWEZI MMOJA TU.

11.3 FOMU ZA KUOMBA KUGOMBEA UONGOZI WA NAFASI ZITAKAZOTANGAZWA ITAKUWA SIKU KUMI NA NNE TU.

11.4           UCHAGUZI UTAFANYIKA KUANZIA SAA 2:00 ASUBUHI HADI SAA 10:00 JIONI NA KUTOLEWA MATOKEO YA UCHAGUZI KUTANGAZWA NA MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI.

11.5           NAFASI YA MWENYEKITI WA ASASI MSHINDI NI LAZIMA APATE ZAIDI YA NUSU YA KURA ZILIZOPIGWA NA ZIKILINGANA ZITARUDIWA TENA ILI KUPATA MSHINDI.

11.6  KIONGOZI AMBAYE MUDA WAKE WA UONGOZI UNAELEKEA KUISHA ANAWEZA KUOMBA TENA HIYO NAFASI AU KUBADILISHA.

11.7 KIONGOZI AKIONEKANA KUFAA ANAWEZA KUGOMBEA TENA NA TENA KWA KIPINDI KINGINE KWA MANUFAA YA ASASI.

11.8           MUDA WA UONGOZI KATIKA ASASI UTAKUWA MIAKA MITANO TU, BAADA YA HAPO MPAKA ACHAGULIWE TENA.

11.9 NAFASI YA UONGOZI ITAKAYOACHWA WAZI KABLA YA MUDA KUISHA KAMATI YA UCHAGUZI ITATANGAZA KUFANYA UCHAGUZI BAADA YA UTARATIBU WA KIF. 11.3 NA 11.2KUTIMIA

SEHEMU YA KUMI NA MBILI

12.0       MUUNDO WA UONGOZI

12.1           MKUTANO MKUU NDIYO WENYE MAAMUZI YA MWISHO YA ASASI NA MIPANGO

     YA UENDESHAJI

12.2   KAMATI TENDAJI NDICHO CHOMBO PEKEE CHENYE KUANDAA NA KUITISHA

     MKUTANO MKUU WA WANACHAMA WOTE, ½ AU 2/3

12.3 WASHAURI WA KUTEULIWA WATAKUWA WATATU NA WA KUAJIRIWA AU

     KUJITOLEA KULINGANA NA TAALUMA ZAO KATIKA UTENDAJI WA SHUGHULI ZA

     ASASI IWEZE KUFIKIA MALENGO.

12.4  KAMATI TENDAJI NA WAKUU WA IDARA ITASIMAMIWA NA KATIBU AU

     MKURUGENZI MTENDAJI WA ASASI.

12.5   WAKUU WA IDARA WATAKUWA SABA, NAO NI:-

(i)             ELIMU NA MAFUNZO

(ii)             AFYA

(iii)             MAZINGIRA, MISITU NA VIUMBE HAI

(iv)             MAHUSIANO, UTALII NA UTAFITI

(v)           MIPANGO KAZI, USHAWISHI NA UWAKILISHI

(vi)         FEDHA

(vii)            MAENDELEO YA JAMII

(viii)          ULINZI NA UETETEZI WA SERA YA TAIFA YA MALIASILI

SEHEMU YA KUMI NA TATU

13.0       MUUNDO WA ASASI NA UONGOZI

13.1 MUUNDO WA ASASI UTAKUWA KAMA IFUATAVYO :-

(i)                MKUTANO MKUU

(ii)                KAMATI TENDAJI

KATIKA MAKAO MAKUU NA MATAWI

SEHEMU YA KUMI NA NNE

14.0       VIKAO

14.1           MAJUKUMU YA MKUTANO MKUU, MAKAO MAKUU NA KATIKA MATAWI

(i)                  MKUTANO UTAFANYIKA MARA MOJA KWA MWAKA

(ii)                KUSOMA MUHTASARI WA MKUTANO ULIOPITA

(iii)              KUSOMA YATOKANAYO YA MKUTANO ULIOPITA

(iv)              KUTHIBITISHA TAARIFA YA UTENDAJI NA YA FEDHA YA MWAKA JANA

(v)                KUPOKEA NA KUPITISHA MAKISIO/BAJETI YA MWAKA UJAO

(vi)              KUTHIBITISHA NA KUPITISHA MAJUKUMU YOTE YA KAMATI TENDAJI, SERA NA MIONGOZO YA ASASI

(vii)            KUPOKEA TAARIFA YA WANACHAMA WAPYA NA WALIOPO

(viii)          KUTHIBITISHA KAMATI YA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA ASASI

(ix)               KUHAKIKISHA KUWA MAAMUZI/MABADILIKO YOTE YA ASASI YANAFANYWA NA MKUTANO MKUU TU

(x)                 KUPITIA NYARAKA NYETI, MIKATABA, TAARIFA NYINGINE ZINAZOHUSU ASASI.

14.2.0                       KAMATI TENDAJI

14.2         UWEZO NA MAJUKUMU YA KAMATI TENDAJI MAKAO MAKUU NA KATIKA MATAWI

(i)                  KUFANYA KIKAO CHA KILA MWEZI

(ii)                KUSOMA MUHTASARI WA KIKAO KILICHOPITA

(iii)              KUSOMA YATOKANAYO YA KIKAO KILICHOPITA

(iv)              KUWEKA MPANGO WA SHUGHULI KWA MALENGO NA MGAWANYO

(v)                KUANDAA MIKATABA, NYARAKA NYETI, SERA, MIONGOZO, TARATIBU KWA MANUFAA YA ASASI.

(vi)              KUANDAA TAARIFA YA FEDHA YA KILA ROBO MWAKA HADI MWAKA 1

(vii)            KUANDAA MAKISIO/BAJETI YA MAPATO NA MATUMIZI YA MWAKA

(viii)          KUBUNI VITEGA UCHUMI

(ix)               KUANDAA MKUTANO MKUU WA WANACHAMA WOTE WA MWAKA

(x)                 KUANDAA TAARIFA YA WANACHAMA WANAOOMBA KUJIUNGA

(xi)               KUANDAA TAARIFA YA WANACHAMA WALIOONDOKA KWA MUJIBU WA SEHEMU YA KUMI YA KATIBA KIF. 10.1 - 10.10

(xii)             KUFANYA MAAMUZI YALIYO NDANI YA MAMLAKA NA UWEZO WAO

(xiii)           KUFANYA KAZI ITAKAYOAGIZWA NA MKUTANO MKUU.

(xiv)           KUPIGIA KURA MAJINA MAWILI YA KUPATA WAJUMBE WAWILI KATI YA MAJINA MANNE YALIYOPENDEKEZWA NA KAMATI TENDAJI: WATAKUWA JINSIA YA KE (1) NA ME (1)

(xv)             KUPIGIA KURA MAJINA MAWILI KATI YA MANNE YA JINSIA YA KE (1) NA ME (1) AMBAO NI WASTAAFU AU TAALUMA, HEKIMA NA BUSARA ILI KUPATA WASHAURI NDANI YA ASASI AMBAO SI WANACHAMA WA MFAWICA KUTOKA KATIKA JAMII.

14.3.0                       MKUTANO WA DHARURA

14.3          UTAKUWA WA MKUTANO MKUU TU

(i)                  UTAANDALIWA NA KAMATI TENDAJI NA KUTOLEWA WITO KWA WANACHAMA NDANI YA SIKU (5) TANO TU

(ii)                UTAZUNGUMZIA JAMBO LA DHARURA TU

(iii)              UTAONGOZWA NA MWENYEKITI KAMA HAYUPO ATACHAGULIWA MWENYEKITI TOKA MIONGONI MWAO KUONGOZA

(iv)              USIPOFANYIKA MKUTANO HAUTAITISHWA TENA, ILA VIONGOZI WAANDAMIZI WA ASASI WATACHUKUA JUKUMU LA DHARULA HIYO

 

14.4        MUUNDO WA UONGOZI

(i) MWENYEKITI

(i MAKAMU MWENYEKITI

(iii)KATIBU/MKURUGENZI MTENDAJI

(iv)KATIBU MSAIDIZI

(v) MHASIBU/MWEKA HAZINA

(vi)MRATIBU

(vii)WAKUU WA IDARA

(viii) WAJUMBE WAWILI – WANA ASASI

(ix) WASHAURI WAWILI – KUTOKA KATIKA JAMII (WENYE MAARIFA, WENYE UJUZI)

(x) WAKUU WA IDARA NANE (8) ZA ASASI

KATIKA MATAWI HAKUTAKUWEPO MKURUGENZI MTENDAJI NA,MRATIBU BALI KATIBU TU NA MWENYEKITI KWA MAJUKUMU MENGINE YANASALIA KUWA KAMA ILIVYO KATIKA KATIBA HII

SEHEMU YA KUMI NA TANO

15.0   MGAWANYO WA MAJUKUMU YA VIONGOZI

15.1     MAJUKUMU YA MWENYEKITI

(i)  MSEMAJI MKUU WA ASASI KATIKA MAAMUZI YALIYOTOLEWA NA MKUTANO MKUU.

(ii) MWENYEKITI WA VIKAO VYA KIKATIBA VYA ASASI

(iii) ATAKUWA NA KURA YA TURUFU

(iv)KUTIA SAINI KATIKA:- MIKATABA, NYARAKA NYETI, MAMBO YA SERA, SHERIA N.K. ZIHUSUZO ASASI

(v) KUTIA SAINI KATIKA HUNDI NA NYARAKA ZA KUTOA FEDHA BENKI

(vi) KUKASIMU MADARAKA PINDI HAYUPO ENEO LA ASASI.

 

15.2   MAJUKUMU YA MAKAMU MWENYEKITI

(i)   ATAFANYA KAZI ZOTE ZA MWENYEKITI PINDI HAYUPO

(ii)   ATASHUGHULIKIA MASUALA NA MAJUKUMU YA KILA SIKU KAMA WANACHAMA WENGINE.

(iii)  ATAFANYAKAZI ATAKAYOAGIZWA NA MKUTANO MKUU NA KAMATI TENDAJI

(iv)  HATAKUWA NA MADARAKA YA KUTIA SAINI KATIKA HUNDI NA NYARAKA ZA KUTOA FEDHA BENKI TOKANA NA TARATIBU ZA KIBENKI.

 

15.3   MAJUKUMU YA KATIBU/MKURUGENZI MTENDAJI

(i) MSIMAMIZI MKUU WA SHUGHULI ZOTE ZA UTENDAJI NA UTAWALA WA ASASI

(ii)  ATASIMAMIA UANDAAJI WA MIRADI YOTE YA ASASI

(iii)ATASHIRIKIANA NA WAKUU WA IDARA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA ASASI.

(iv)              ATAANDAA NA KUTOA TAARIFA YA SHUGHULI ZA UTEKELEZAJI WA MIRADI NA ZA UTENDAJI KWA MKUTANO MKUU NA KAMATI TENDAJI.

(v)                KUANDIKA MIHTASARI YA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA ASASI.

(vi)              KUTUNZA KUMBUKUMBU ZA MIHTASARI YOTE YA ASASI.

(vii)            KUSHIRIKIANAN A WAKUU WA IDARA KUANDAA:- MIKATABA, NYARAKA NYETI, SERA, MIONGOZO, TARATIBU, KANUNI N.K. ZA ASASI.

(viii) ATASHUGHURIKIA AJIRA NA KUONDOA AJIRA NDANI YA ASASI

(ix)KUWA NA MAHUSIANO MAZURI KWA WADAU, WAFADHILI, WAHISANI, WATAALAM, WASHAURI, SERIKALI KATIKA NYANJA ZA KUKUZA NA KUBORESHA UTENDAJI WA ASASI KWA KUPATA FEDHA, MALI, USHAURI N.K.

(x) KUJIBU BARUA ZOTE ZA MAWASILIANO YANAYOHUSU SHUGHULI NA UTEKELEZAJI WA ASASI.

(xi) MSHAURI MKUU WA MWENYEKITI WA ASASI.

(xii)KUTOA TAARIFA YA MKUTANO KWA WANACHAMA SIKU SABA (7) KABLA YA KIKAO.

(xiii)MSIMAMIZI MKUU WA FEDHA NA MALI ZA ASASI.

(xiv) KUIDHINISHA MALIPO YA SHUGHULI ZOTE ZA ASASI.

(xv)KUTIA SAINI KATIKA HUNDI NA NYARAKA ZA KUTOA FEDHA BENKI.

(xvi) ATAKUWA MWENYEKITI WA KAMATI TENDAJI.

(xvii)MTIA SAINI KATIKA NYARAKA NYETI, MIKATABA, SERA, SHERIA, VYETI NA VITAMBULISHO VYA ASASI.

 

15.4   MAJUKUMU YA KATIBU MSAIDIZI

(i) ATAFANYA KAZI ATAKAZOAGIZWA NA KATIBU AKIWA YUPO NJE YA ASASI AU AKIWA NA MAJUKUMU MENGINE.

(ii) ATAFANYA SHUGHULI YOYOTE ATAKAYOAGIZWA NA MKUTANO MKUU NA KAMATI TENDAJI

(iii) ATAFANYA SHUGHULI ZA KILA SIKU ZA ASASI KAMA WANACHAMA WENGINE.

15.5   MAJUKUMU YA MHASIBU / MWEKA HAZINA

(i)  KUTOA STAKABADHI YA FEDHA INAYOPOKELEWA.

(ii) KUPELEKA FEDHA BENKI KATIKA AKAUNTI YA ASASI.

(iii) KUTUNZA KUMBUKUMBU YA MAPATO NA MATUMIZI.

(iv)KULINGANISHA MAPATO NA MATUMIZI KILA SIKU.

(v) KULINGANISHA BENKI STATEMENT NA VITABU VYA ASASI KILA MWEZI.

(vi)KUANDAA TAARIFA YA MWEZI, ROBO, NUSU, MIEZI 9 NA MWAKA; TAARIFA YA FEDHA.

(vii)KUTOA TAARIFA YA FEDHA YA MAPATO NA MATUMIZI KATIKA VIKAO VYA KIKATIBA NA UTENDAJI.

(viii)ATAWAJIBIKA KATIKA MASWALA YOTE YA FEDHA KWA KUTUMIA MWONGOZO WA FEDHA.

(ix) ATAANDAA MAKADIRIO/BAJETI YA ASASI YA MWAKA

(x)  ATAIDHINISHA MALIPO/MATUMIZI YA FEDHA PINDI KATIBU/MKURUGENZI MTENDAJI AKIWA SAFARINI/NJE YA KITUO KWA BARUA RASMI.

(xi)  KUJENGA MAHUSIANO MAZURI NA TAASISI ZA FEDHA, SERIKALI NA ASASI NYINGINE ZA KIFEDHA

(xii)ATAKUWA MSHAURI WA MWENYEKITI NA KATIBU/MKURUGENZI MTENDAJI KATIKA MASWALA YA FEDHA

(xiii) ATASIMAMIA FEDHA YA MATUMIZI MADOGO MADOGO KUPITIA PETTY CASH SYSTEM

(xiv) KUTIA SAINI KATIKA HUNDI NA NYARAKA ZA KUTOA FEDHA BENKI

(xv) ATAFANYA KAZI NYINGINE KAMA ATAKAVYOELEKEZWA NA MKUTANO MKUU, MWENYEKITI, KATIBU/MKURUGENZI MTENDAJI

(xvi)           ATAKUWA KATIBU WA KAMATI TENDAJI

(xvii)         ATATUNZA MIHTASARI YA VIKAO VYA KAMATI TENDAJI NA KUANDAA MIKUTANO

15.6   MAJUKUMU YA MRATIBU

(i) KUANDIKA MICHANGANUO YA MIRADI YA ASASI

(ii)KUTAFUTA/KUIBUA MIRADI NA KUIFUATILIA ILI KUPATA FEDHA KWA KUENDESHEA SHUGHULI ZA ASASI

(iii)KUSHIRIKIANA NA KATIBU/MKURUGENZI MTENDAJI KUFANYA MAWASILIANO NA UHUSIANO WA KARIBU NA WAFADHILI AMBAO ASASI ITAKUWA IMEPATA FEDHA YA MRADI AU INAPOTAFUTA FEDHA KWA WAFADHILI.

(iv)              KUSHIRIKIANA NA MHASIBU NA MKURUGENZI MTENDAJI KATIKA UANDAAJI WA BAJETI YA MRADI UTAKAOKUWA UNAOMBEWA FEDHA KWA MFADHILI.

(v)KUANDAA SHUGHULI ZA MRADI AMBAO UTAKUWA UMEPATA FEDHA YA RUZUKU.

(vi)KUFANYA MREJESHO WA SHUGHULI ZA MRADI ULIOTEKELEZWA KWA MKURUGENZI MTENDAJI KATIKA MUDA WA SIKU 5 BAADA YA KUFANYIKA.

(vii)KUTUNZA KUMBUKUMBU ZA MRADI

(viii)KUTOA USHAURI KWA MKURUGENZI MTENDAJI JUU YA MASWALA MUHIMU YA KUFANIKISHA LENGO MAHUSUSI, LENGO KUU NA SHUGHULI ZA MRADI.

(ix)KUTOA TAARIFA YA SHUGHULI ZAKE KATIKA KIKAO CHA KAMATI TENDAJI.

(x)KUFANYA KAZI YOYOTE ATAKAYOELEKEZWA NA MKURUGENZI MTENDAJI

(xi)KUTIA SAINI KATIKA HUNDI NA NYARAKA ZA KUTOA FEDHA BENKI.

15.7   MAJUKUMU YA WAKUU WA IDARA

(i) YATOKANAYO NA SEHEMU YA NNE YA KATIBA

(ii) YATOKANAYO NA MAELEKEZO YA MKUTANO MKUU

(iii) YATOKANAYO NA MAELEKEZO YA MKURUGENZI MTENDAJI

(iv) ATAWAJIBIKA KUANDAA MAJUKUMU YA IDARA YAKE

(v) MJUMBE WA KAMATI TENDAJI

15.8   MAJUKUMU YA WAJUMBE NA WASHAURI

(i)KUTOA USHAURI KWA MWENYEKITI, MKURUGENZI MTENDAJI, MHASIBU NA MRATIBU KWA UFANISI WA ASASI.

(ii)KUKUTANA NA KAMATI TENDAJI KWA MWAKA MARA MBILI KWA LENGO LA KUONA UFANISI NA UTENDAJI WA SHUGHULI ZA ASASI KWA MIEZI SITA NA MWAKA MZIMA.

(iii) WATAKUWA CHOMBO CHA KUSULUHISHA MIGOGORO, MIGONGANO NA DHANA YOYOTE POTOFU KWA MANUFAA YA ASASI.

(iv)WATAKUWA NI WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA ASASI.

SEHEMU YA KUMI NA SITA

16.0  WAJUMBE WA KAMATI TENDAJI

16.1    MWENYEKITI

16.2  MAKAMU MWENYEKITI

16.3   KATIBU/MKURUGENZI MTENDAJI

16.4   KATIBU MSAIDIZI

16.5   MHASIBU/MWEKA HAZINA

16.6  MRATIBU

16.7  WAKUU WA IDARA

16.8   WAJUMBE (2)

16.9  WASHAURI (2)

SEHEMU YA KUMI NA SABA

17.0  UTAWALA WA ASASI

17.1    UTAWALA WA ASASI UTAKUWA CHINI YA KAMATI TENDAJI

17.2  VIONGOZI WAANDAMIZI WATAKAO WAJIBIKA SIKU KWA SIKU KUANDAA NA KUJIBU SHIDA MBALIMBALI WATAKUWA NI :-

(i)  KATIBU / MKURUGENZI MTENDAJI

(ii) MHASIBU / MWEKA HAZINA

(iii) MRATIBU

 

17.3 KATIKA NGAZI YA TAWI VIONGOZI WATAKAO WAJIBIKA SIKU HADI SIKU NI :

(I) KATIBU WA TAWI

(II) MWEKA HAZINA WA TAWI

 

NA VIONGOZI HAO WATA WAJIBIKA MOJA KWA MOJA KATIKA KAMATI TENDAJI YA      

TAWI KWA SHUGHULI ZA KILA SIKU

SEHEMU YA KUMI NA NANE

18.0   MIIKO YA UONGOZI

18.1     KUTOTOA SIRI ZA ASASI JUU YA JAMBO LOLOTE AMBALO HALITATOLEWA

           MAAMUZI NA VIKAO

18.2   KUTOSABABISHA, KUCHOCHEA , KUFANYA VURUGU, KUGOMBANA, N.K. NDANI

         YA MAENEO YA ASASI NA NJE PIA.

18.3   KUTOTUMIA MALI, FEDHA NA RASLIMALI YA ASASI KWA MANUFAA BINAFSI.

18.4   KUTOTOA RUSHWA AU KUPOKEA RUSHWA WAKATI WA SHUGHULI ZA ASASI.

18.5   KUTOHESHIMU MISINGI YA IMANI YA DINI, MILA NA DESTURI, JINSIA NA UTU.

18.6   KUTOJIHUSISHA NA MAMBO YA ITIKADI ZA KISIASA NA DINI

18.7   KUTOHESHIMU VIONGOZI WA ASASI PIA WANACHAMA

18.8   KUTOTIMIZA NA KUMALIZA KAZI ULIYOPANGIWA/AGIZWA NA MKUTANO MKUU,

           KAMATI TENDAJI, MKUU WA IDARA AU WAJUMBE NA WASHAURI KWA MUDA

         MAALUM.

18.9   KUTOTUMIA NEMBO YA ASASI, MIHURI NA KIELELEZO CHOCHOTE KILE CHA ASASI

           KWA MANUFAA BINAFSI.

SEHEMU YA KUMI NA TISA

19.0  MIPANGO NA MIKAKATI YA ASASI KUFIKIA MALENGO YAKE

19.1    KUAJIRI WATU WAZOEFU NA WENYE TAALUMA ILI KUBORESHA SHUGHULI ZA ASASI

19.2  KUTAFUTA FEDHA KUTOKA KWA WAFADHILI, WADAU, SERIKALI, WATU BINAFSI, MASHIRIKA, TAASISI ZA KIBENKI ILI KUENDESHEA MIRADI YA ASASI.

19.3   KUKUSANYA FEDHA YA ADA, MICHANGO NA VIINGILIO KWA KUTEKELEZA KAZI ZA ASASI.

19.4   KUWA NA MIPANGO YA MUDA MFUPI NA MUDA MREFU NA INAYOELEWEKA KWA UTEKELEZAJI.

SEHEMU YA ISHIRINI

20.0VYANZO VYA MAPATO

20.1  ADA, VIINGILIO NA MICHANGO

20.2RUZUKU NA UFADHILI KUTOKA KWA SERIKALI, MASHIRIKA, WATU BINAFSI NDANI YA TANZANIA NA NJE YA TANZANIA.

20.3 MIKOPO YA WAHISANI, SERIKALI, BENKI, MASHIRIKA YA DINI, MASHIRIKA YA UMMA NA WATU BINAFSI

20.4 UFUGAJI NYUKI NA KUUZA ASALI

20.5 UFUGAJI WA SAMAKI KATIKA MABWAWA NA KUUZA

20.6KILIMO CHA MAZAO YA BIASHARA NA CHAKULA

20.7MICHANGO YA UTUNISHAJI MFUKO

20.8 MALIPO YA HUDUMA KWA WATALII

20.9MAZAO YA ASILI YATOKANAYO NA UHIFADHI WA MALI ASILI.

20.10 MALIPO YATAKAYOTOLEWA NA WATAFITI WA MALI ASILI MAENEO

            YANAYOHIFADHIWA NA ASASI

SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA

21.0  MATUNZO YA FEDHA NA KUMBUKUMBU

21.1    FEDHA YOTE ITAPOKELEWA KWA KUTOA STAKABADHI

21.2  KUPELEKA FEDHA BENKI KWENYE AKAUNTI YA ASASI

21.3   KUWEKA KUMBUKUMBU KATIKA VITABU VYA KIHASIBU

SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI

22.0MATUMIZI YA FEDHA

22.1  UCHAPAJI, KURUDUFU, SHAJARA N.K.

22.2PANGO LA OFISI, UMEME, MAJI, VIFAA VYA OFISI N.K.

22.3 MAWASILIANOKAMA : SIMU, EMS, INTERNET, POSTA SANDUKU LA BARUA, EMS N.K.

22.4 GHARAMA ZA USHAURI WA SHERIA NA UHASIBU

22.5 POSHO KWA WATENDAJI WENYE TAALUMA N.K.

22.6MATIBABU YA WANACHAMA/WAFANYAKAZI

22.7SAFARI ZA KIKAZI ZA ASASI

22.8 KUNUNUA SAMANI, RASLIMALI, ARDHI, MITAMBO N.K.

22.9UJENZI WA SHULE, OFISI YA ASASI, BARABARA, ZAHANATI N.K.

22.10 KUFUATA MAKISIO/BAJETI YA ASASI

22.11   MALIPO KUANZIA LAKI TANO YATATUMIA UTARATIBU WA MANUNUZI KWA UGAVI NA KAMATI TENDAJIITAPITIA MAOMBI YA UGAVI KUANZIA 3 NA KUENDELEA.

22.12 MISAADA YA DHARULA PANAPOTOKEA MAJANGA YANAYOATHILI JAMII KILA  INAPOBIDI.

SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU

23.0 UTARATIBU WA MALIPO

23.1   KUWEPO KWA HATI ZA MATUMIZI KAMA ; ANKARA, MADAI YA AWALI, BARUA, STAKABADHI N.K.

23.2 HATI YA MALIPO – PAYMENT VOUCHER YA ASASI

23.3 VIAMBATANISHO KWENYE PAYMENT VOUCHER

23.4 MAELEZO KAMILI KATIKA HATI YA MALIPO :- MTAYARISHAJI, MKAGUZI,

           MUIDHINISHAJI MALIPO N.K.

23.5 JINA KAMILI NA ANUANI YA MLIPWAJI NA AINA YA MALIPO KAMA NI TASLIMU AU HUNDI / NA KIASI KILICHOLIPWA

23.6 HATI YA MALIPO NA VIAMBATANISHO KUPIGWA MUHURI WA ASASI

         ULIOANDIKWA « PAID »

23.7 STAKABADHI AU SAHIHI YA MLIPWAJI KUSAINI KATIKA VOUCHER ILIIYOKAMILIKA

23.8 KUINGIZA HATI YA MALIPO / PV KATIKA CASH BOOK KWA TAREHE MALIPO YALIPOFANYIKA NA KUIWEKEA NAMBA NA KUIFAILI.

SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE

24.0 WAWEKA SAINI KATIKA HUNDI/NYARAKA ZA KUTOA FEDHA BENKI

24.1   KUNDI : A :

(i)                  MWENYEKITI

(ii)                 MKURUGENZI MTENDAJI

24.2 KUNDI : B :

(i)                  MHASIBU/MWEKA HAZINA

(ii)                 MRATIBU

NB : MALIPO YATAFANYIKA KWA MTU MMOJA ; KUNDI ‘’A’’ WA PILI ‘’B’’ NA SIO TOKA KUNDIMOJA TU ie. ‘’A’’ TU / ‘’B’’ TU

24.3 KATIKA NGAZI YA TAWI :

WATIA SAINI : KUNDI A. (I) MWENYEKITI WA TAWI

                                   ( II) KATIBU WA TAWI

         WATIA SAINI : KUNDI B ; (I) MWEKA HAZINA WA TAWI

                                                 (II) MJUMBE MMOJA WA TAWI

NB : MALIPO YATAFANYIKA KWA MTU MMOJA ; KUNDI ‘’A’’ WA PILI ‘’B’’ NA SIO TOKA KUNDI MOJA TU ie. ‘’A’’ TU / ‘’B’’ TU

SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO

25.0 ELIMU NA MAFUNZO KWA WANACHAMA WAAJIRIWA

25.1    ASASI ITAWALIPA WANACHAMA NA WATAALAM WATAKAOONYESHA BIDII YA

KUFANIKISHASHUGHULI ZAO KWA MANUFAA YA MFAWICA

25.2 ASASI ITAGHARAMIA MAFUNZO YA MUDA MREFU, MFUPI, SEMINA, WARSHA, ILI  KULETA UFANISI.

25.3 WALE WATAKAOFANIKIWA KUIPATA HIYO ELIMU WATAITUMIA KUFUNDISHA WENGINE KWA MANUFAA YA ASASI.

SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA

26.0WAJIBU NA MAADILI YA WAFANYAKAZI WAAJIRIWA

26.1  WATATENDA KAZI ZAO CHINI YA MKURUGENZI MTENDAJI

26.2WATAKUWA WASHAURI WA MKURUGENZI MTENDAJI

26.3 WATAFANYA KAZI KWA TAALUMA ZAO

26.4 WATAPASWA KUJENGA HESHIMA WAO KWA WAO, KWA VIONGOZI,

           MKURUGENZI MTENDAJI, WANACHAMA NA WANA JAMII WOTE.

26.5 HATUA ZA KINIDHAMU ZITACHUKULIWA WAKATI WOWOTE KWA YULE

           ATAKAYEONESHA UTOVU WA NIDHAMUKWA MUJIBU WA SEHEMU YA KUMI NA NANE YA KATIBA

26.6WATAJAZA MIKATABA YA AJIRA/KAZI NA KUSAINIWA PANDE ZOTE MBILI

26.7MAOMBI YAO YATATUMWA KWA MKURUGENZI MTENDAJI WA ASASI AMBAYE ATAYAFANYIA KAZI NA KUTOA MAJIBU NDIYO/HAPANA.

26.8 TUNU/ZAWADI ITATOLEWA KWA MWAJIRIWA NA MWANACHAMA YEYOTE ATAKAYEONESHA JUHUDI NA UFANISI WA KAZI KWA FAIDA YA ASASI NA JAMII KWA UJUMLA KATIKA SIKUKUU YA WAFANYAKAZI.

SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA

27.0UUNDAJI WA KAMATI YA UCHUNGUZI/UKAGUZI

27.1  Kamati Ya Uchunguzi/Ukaguzi Itatoka Nje Ya Asasi

27.2Mkutano Mkuu Ndio Wenye Uwezo Wa Kuamua Hili

27.3 Itafanya Kazi Kwa Muda Wa Majuma Mawili Tu Kwa Kulipwa Gharama Zao Kwa Kazi Husika Kwa Makubaliano.

27.4 Hazitakuwa Za Kudumu

27.5 Taarifa Ya Kazi Yao Itatumwa Kwa Mwenyekiti Wa Asasi Ambaye

           Ataitisha Kamati Tendaji Kuipitia Kabla Ya Kwenda Mkutano Mkuu Kwa           Hatua Nyingine

27.6Baada Ya Mkutano Mkuu Taarifa Hiyo Itabaki Kwa Mkurugenzi

           Mtendaji Kwa Kazi Ya Asasi (Kiutawala)

SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE

28.0 MAWASILIANO

28.1   asasi itafanya mawasiliano sehemu mbalimbali kwa ajili ya shughuli zenye manufaa na maendeleo kwa njia kama vile:-

(i)                posta - rejesta

(ii)                ems

(iii)              barua pepe

(iv)              sanduku la barua

(v)                mtandao(Website)

(vi)              fax

(vii)            simu ya mezani

(viii)          simu ya mkononi n.k

SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA

29.0UBIA

29.1  Kufanya Ubia Kwa Uhuru

29.2Kufanya Ubia Na Serikali, Asasi, Cbo, Mdau, Mfadhili, Mtu Binafsi,

           Shirika, Taasisi Ya Dini, Benki.

29.3 Kutuma Barua Ya Maombi Kwa Mkurugenzi Mtendaji Wa Asasi

29.4 Kujaza Fomu Ya Makubaliano Pande Mbili Ambayo Itakuwa Na

           Utaratibu Wa Mkataba Wa Muda Mrefu Au Mfupi

29.5 Kutoa Kiingilio Cha Ubia Sawa Na Itakavyojadiliwa Na Mkutano Mkuu.

29.6Ubia Utakuwa Na Muda Ambao Ni Makubaliano Ya Asasi Na Mbia

29.7Kukubali Kutoa Michango Ya Hiari Kwa Kazi Ndani Ya Ubia

29.8 Ubia Unaweza Kufutwa Wakati Wowote Endapo Masharti Yaliyomo

           Ndani Ya Mkataba Yatakiukwa

29.9Mkataba Wa Ubia Utafutwa Kwa Makosa Ya Jambo La Jinai – Hatua Za

           Kisheria Zitachukuliwa Kwa Kufungua Kesi Na Utaratibu Wote

           Utafuatwa. Kama Yatakavyokuwa Makubaliano.

29.10 Mkataba Utawekewa Saini Na Muhuri Toka Pande Zote Mbili

           Zinazokubaliana.

29.11   Mkataba Wowote Utakaofanywa Kati Ya Asasi Na Mbia, Patakuwa Na

           Mashahidi, Ikibidi Wa Kisheria Za Mahakama.

SEHEMU YA THELATHINI

30.0 KUHESHIMU MAAMUZI YA MKUTANO MKUU, KAMATI TENDAJI NA KATIBA YA ASASI NA MIONGOZO NA KATIBA YA NCHI.

30.1   Mambo Ambayo Hayakuandikwa Ndani Ya Katiba Na Miongozo/Kanuni

           Yataamuriwa Na Mkutano Mkuu.

30.2 Mkutano Mkuu Utachukua Hatua Ya Jambo Lolote Lenye Utata Baada

           Ya Kuwa Limeanzia Katika Idara Kupitia Kamati Tendaji Ambayo Ni

           Chombo Kikubwa Katika Utendaji Wa Asasi.

30.3 Jambo Ambalo Litaonekana Kuleta Athari Katika Asasi Ruhusa

           Itatolewa Na Kupeleka Jambo Hilo Mahakamani Baada Ya Taratibu

Kukamilika Na Kusimamiwa Na Mkurugenzi Mtendaji Wa Asasi.

SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA

31.0   KUVUNJIKA KWA ASASI

31.1     Mkutano Mkuu Utaitishwa

31.2   Agenda Ya Kuvunja Asasi Itatolewa

31.3   Viongozi Wa Serikali Na Mtandao Wa Wilaya Ya Kigoma Wataalikwa

           Katikamkutano

31.4   Kabla Ya Uamuzi Wa Kuvunja Madeni Yote Yatalipwa Kwanza

31.5   Mali Zitakazosalia Hazitagawiwa Kwa Mwanachama Yeyote.

31.6   Wajumbe Wapatao Theluthi Mbili Ndiyo Watakuwa Na Uamuzi Wa

           Mwisho Kwakupiga Kura Za Siri.

31.7   Kamati Ya Kusimamia Na Kulinda Mali Itaundwa

31.8   Mali Zote Zitagawiwa Mashirika Yenye Lengo Sawa Na Mfawica

31.9   Kuvunjika Kwa Asasi Kutatolewa Taarifa Katika Serikali Mtandao (W)

           Kigoma, Pia Kutangazwa Katika Vyombo Kama Vile:- Radio, Gazeti, Mbao

           Za Matangazo N.K.

31.10    Zoezi Litakamilika Ndani Ya Siku 30 Tu.

SEHEMU YA THELATHINI NA MBILI

32.0 ORODHA YA WANACHAMA WAANZILISHI – MWAKA 2005

MAJINA YAO KAMILI                                         

  1. RAMADHANI NYUNDO SIKA                          
  1. BARAKA PETER NZOVU                            
  1. SILINDILA ATHUMAN KALIMBA                    
  1. SALUM SHABAN KITOPENI                    
  1. AKSA ANDREA CHAGAMBA                     
  1. MOHAMED HAMIS KALIMANZILA              
  1. 0MAKELELE MASANYUKE KIKOMO             
  1. MOSHI HARUNA MADIGIDI                   
  1. UHURU HAMIS BUTATI                         
  1. RAULENTI RICHARD GABRIEL              

33.0 ORODHA YA WANACHAMA WAPYA WA KUJIUNGA MWAKA 2009/12

MAJINA YAO KAMILI                        SAHIHI ZAO                           TAREHE

1.   MWAMBA A. KIEMENA             ……………………..                  ………………………..

2. Hamisi Almasi                            …………………………...             ……………………….

3 ALEX EKAMA MNENE                   ……………………………             ………………………

4 Simoni Patilo Bwilo                     ……………………………              ……………………

5 Imani Richard Gabriel                  ……………………………              ………………….

6  Simon Petro                            …………………………….                …………………..

7 Laimond Simon                         …………………….                      ...................                        

8  Rajabu Juma Madolla                ……………………………..              …………………….

9  Rajabu Kakumo                        …………………………….              …………………….

10Shabani Mussa Kibanga             ……………………………                ……………………..

11Mashaka Almas                      ……………………………                  …………………….

12Shabani Kijungi                       …………………………..                 ……………………..

13 Goodnes Issak Baziyaka         …………………………….                ……………………

14 Issa Lufwifwi.                          …………………………….               ……………………

15 Abdallah Mussa.                      ……………………………..               …………………..

MWISHO

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

    Asasi PROFILE

1.0 UTANGULIZI

MFAWICA ni zisizo za kiserikali, mashirika yasiyo ya faida - maamuzi uanachama shirika ilianzishwa mwaka 2005 na kusajiliwa kisheria mwaka 2008 chini ya Usajili No 00NGO/0436, unaojulikana kama "Milele Misitu na Uhifadhi wa Wanyamapori Association". Lengo kuu la shirika ni kuwawezesha wanamazingira mitaa, curators ya asili, misitu na watu wa jamii ya kuyahifadhi, kulinda na kuboresha mazingira na kupunguza hali ya kukokotoa wanakabiliwa na wanajamii na kuwawezesha kupata mali asili zao na usawa kutumia yao endelevu kuboresha maisha yao na maendeleo. Na kupambana na dutu inakabiliwa na jamii kama vile matumizi mabaya ya VVU / Ukimwi, madawa ya kulevya na ulevi kupita kiasi, magonjwa ya mlipuko na umaskini kwa lengo la kuweka jamii kuwa huru kutokana na umaskini na sababu kubwa ya hayo, na kukuza maendeleo endelevu

2.0 MFAWICA MAHALI & ENEO uendeshaji:

Tangu kuanzishwa, MFAWICA kazi katika Igalula, mmoja wa kata sana kijijini, wenyeji na maskini wa Kigoma Wilaya ya Vijijini. kata iko katika Kusini ya mkoa wa Kigoma kwamba iko katika Magharibi ya Tanzania na inayopakana na Jamhuri ya Burundi na Tanzania katika mkoa wa Kagera, Kaskazini, - Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika Magharibi, - Rukwa mkoa katika Kusini na Tabora na Shinyanga katika mikoa ya Mashariki. Robo Mkuu wa shirika ni imara katika kijiji Rukoma katika Igalula Kata, Buhingu Tawala wa Idara. Pia, Shirika lina sasa ni moja Field Station saa Lubalisi kijiji, mmoja Connection na Ofisi ya Habari katika Ziwa Tanganyika katika Uwanja wa Kigoma / Ujiji Manispaa kama Township ya Mkoa wa Kigoma, na moja ya Jumuiya za Wanyamapori na Misitu ya Hifadhi eneo kufunika zaidi ya hekta 2000 inayoitwa " Milele Msitu wa Hifadhi Karobwa ".

3.0 MFAWICA DIRA

maono ya MFAWICA ni kuona wanachama wote wa jamii katika Tanzania na duniani kote na umaskini uliokithiri, magonjwa na majanga kutokana na uharibifu wa mazingira, uchafuzi wa mazingira, moto uharibifu mkubwa wa misitu na maliasili ukatili.

Ili kufikia lengo hili, MFAWICA ni nia ya kupunguza umaskini uliokithiri, maradhi na burdening jamii kwa kuhakikisha haki za binadamu na maendeleo endelevu kwa ajili ya makundi ya idadi ya watu maskini katika Tanzania kwa njia ya mazingira, wanyamapori, uvuvi, misitu, maji na maliasili ulinzi, uhifadhi na utunzaji . kupambana na dutu inakabiliwa na jamii kama vile VVU / Ukimwi, madawa ya kulevya na ulevi kupita kiasi, magonjwa ya mlipuko na umaskini kwa lengo la kuweka jamii kuwa huru kutokana na umaskini na sababu kubwa ya hayo, na kukuza maendeleo endelevu

4.0 MFAWICA MISSION

MFAWICA ni NGO ya eneo ambayo ina mpango wa mkakati wa kuboresha hali ya maisha ya wakazi wanaoishi katika mazingira magumu kupitia uratibu na uendelezaji wa mshikamano kwa ajili ya kuboresha maisha na hifadhi ya mazingira na kutetea jamii kuwa na madaraka na utawala wa usimamizi wa maliasili ili kupambana dhidi ya umaskini na ya asili magonjwa. na kupambana na dutu inakabiliwa na jamii kama vile matumizi mabaya ya VVU / Ukimwi, madawa ya kulevya na ulevi kupita kiasi, magonjwa ya mlipuko na umaskini kwa lengo la kuweka jamii kuwa huru kutokana na umaskini na sababu kubwa ya hayo, na kukuza maendeleo endelevu

5.0 MAADILI MFAWICA

Shughuli zetu ni kuongozwa na seti ya maadili yafuatayo:

1. Usawa na Equity mahitaji ya msingi kwa ajili ya watu wote, bila kujali jinsia zao, jinsia na asili;

2. Ardhi, Misitu, Uvuvi, maji na wanyamapori ni kubwa maisha nguzo na misaada ya kiuchumi.

6.0 MFAWICA MALENGO:

malengo makuu ambayo MFAWICA ni kupunguza uharibifu wa Tanzania na sayari maliasili mazingira na kujenga mustakabali na muundo bora ya maisha ambayo binadamu na viumbe wote hai kuishi kwa amani na asili, kwa: -

  1. Kuwawezesha kiuchumi, kiufundi na kijamii katika jamii husika kwa njia ya mazingira na mali asili ya ulinzi na kukuza kutoka njia ya haki;
  2. Kucheza zaidi ya kisheria jukumu katika mazingira ya kupunguza umaskini,...

In order to edit translations, you need to log in. Log in · Register

Translation History

mfawica
June 16, 2012
Asasi PROFILE – 1.0 UTANGULIZI – MFAWICA ni zisizo za kiserikali, mashirika yasiyo ya faida - maamuzi uanachama shirika ilianzishwa mwaka 2005 na kusajiliwa kisheria mwaka 2008 chini ya Usajili No 00NGO/0436, unaojulikana kama "Milele Misitu na Uhifadhi wa Wanyamapori...
This translation refers to an older version of the source text.
Google Translate
June 16, 2012
Asasi PROFILE – 1.0 UTANGULIZI – MFAWICA ni zisizo za kiserikali, mashirika yasiyo ya faida - maamuzi uanachama shirika ilianzishwa mwaka 2005 na kusajiliwa kisheria mwaka 2008 chini ya Usajili No 00NGO/0436, unaojulikana kama "Milele Misitu na Uhifadhi wa Wanyamapori...
This translation refers to an older version of the source text.