Base (English) | Kiswahili |
---|---|
In just a few minutes, you can easily register your civil society organization on Envaya, for free, from any computer with an internet connection. (For civil society organizations in Tanzania and Rwanda, it is not necessary to ask for approval before registering for Envaya.) To register your organization, first go to http://envaya.org in any web browser and click Sign up now, as shown below: QualificationNext, Envaya will ask you a couple of questions to make sure that your organization qualifies to use Envaya. Click the appropriate answers for your organization, then click the blue button at the bottom of the page. Create AccountIf your organization qualifies to use Envaya, the next page will let you create an account for your organization. On this page, you will need to enter your organization's name and contact information, and choose a username and password for your organization on Envaya. For your username, you should enter a short name or abbreviation for your organization. The username will be used to determine your organization's web address on Envaya. For example, if your username is jeanmedia, your web address will be http://envaya.org/jeanmedia. For your password, choose a secret word or phrase at least 6 characters long. Together with your username, the password will let you log in to edit your organization's website. Remember your password and only share it with people who are allowed to edit your organization's website. If your organization has an email address or phone number, Envaya may use this information to contact you, such as verifying your organization, helping you if you forget your password, and contacting you about new updates with Envaya. When you have entered all the information, click the blue button at the bottom of the page to continue. If there are any red error messages at the top of the page, correct the errors and then click the blue button again. Set Up HomepageThe final step in registering your organization is to enter some more information that Envaya will use to create an initial homepage for your organization's website. Follow the instructions on this page to enter your organization's mission, choose up to 5 sectors to categorize your organization, enter the city and region where your organization is located, and choose a design for your website. When you are done, click the blue button at the bottom of the page to create your organization's website. If there are any error messages in red, correct the errors and click the blue button again. Finally, Envaya will take you to your organization's new website. Envaya's administrators will be notified that your organization has registered, and they will need to approve your website before it appears publicly, to make sure that your organization qualifies to use Envaya. If you entered an email address for your organization, Envaya will send you an email when your organization's website is approved. Even while your organization is awaiting review by Envaya's administrators, you can continue editing your website and adding other pages and information about your organization, as explained in the following pages. |
Katika dakika chache tu unaweza kuandikisha shirika lako la kijamii jamii kwenye tovuti ya Envaya, bure kabisa, kwenye kompyuta yenye mtandao. (Kwa mashirika ya kiraia yaliopo Tanzania na Rwanda, si lazima kuomba kibali kabla ya kusajili Envaya.) Kusajili shirika lako, nenda kwanza http://envaya.org kwa kutumia browser yoyote ya mtandao na bonyeza Jiunge Sasa au Sign up now, kama ilivyo hapa chini: SifaKisha utaulizwa maswali kadhaa ili kuhakikisha kwamba shirika lako lina sifa za kutumia Envaya. Chagua majibu yanayolingana na shirika lako, kisha bonyeza kifungo cha bluu chini ya ukurasa. Kujenga Akaunti YakoKama asasi yako ina sifa ya kutumia Envaya, ukurasa unaofuatia utakuwezesha kujenda akaunti ya asasi yako. Katika ukurasa huu, unahitaji kuingiza jina la asasi yako na namba za mawasiliano, na kuchagua jina la mtumiaji na neno la siri kwa shirika lako. Jina la mtumiaji linatakiwa liwe fupi au kifupi cha asasi yako. Jina la mtumiaji litatumika kwenye anwani ya mtandao wa asasi yako. Kwa mfano, kama jina lako ni jeanmedia, anwani ya mtandao wako itakuwa http://envaya.org/jeanmedia. Neno la siri au password yako inatakiwa iwe neno au sentensi fupi ya kisiri, iwe angalau na herufi 6. Jina la mtumiaji na neno la siri litakuwezesha kuingia na kuhariri tovuti la shirika lako. Kumbuka neno lako la siri na kulitoa kwa watu ambao wanaruhusiwa hariri tovuti ya asasi yako tu. Kama asasi yako ina anwani ya barua pepe au namba ya simu, Envaya inaweza kuzitumia kuwasiliana na wewe, kwa lengo la kuthibitisha shirika lako, kusaidia kama umesahau neno la siri, na kuwasiliana na wewe kuhusu mabadiliko mapya na Envaya. Utakapokuwa umeweka taarifa zote, bonyeza kifungo cha bluu chini ya ukurasa ili uendele. Kama ujumbe mwekundu utatokezea juu ya ukurasa , sahihisha makosa na kisha bonyeza kifungo cha bluu tena. Hariri Ukurasa wako MkuuHatua ya mwisho katika kusajili asasi yako ni kuingiza taarifa ambazo Envaya itatumia kujenga Ukurasa wako mkuu yaani homepage ya awali kwa ajili ya tovuti ya asasi yako. Fuata maelekezo katika ukurasa huu kuingiza malengo ya asasi yako, chagua hadi sekta 5 zinazohusiana na shirika lako, ingiza mji na mkoa ambapo shirika linapatikana, na chagua muonekano wa tovuti yako. Utakapomaliza bonyeza kifungu cha bluu chini ya ukurasa. Kama kuna kosa lolote ujumbe mwekundu utajitokeza. Sahihisha makosa na bonyeza batani cha bluu tena. Hatimaye, Envaya itakupeleka kwenye tovuti ya asasi yako mpya. Watendaji wa Envaya watajulishwa kuwa shirika lako limesajiliwa, na wanahitaji kuikubali tovuti yako kabla ya kuonekana hadharani kwenye mtandao, ili kuhakikisha kwamba shirika lako lina sifa za kutumia Envaya. Kama uliingiza anwani ya barua pepe ya shirika lako, Envaya litakutumia barua pepe ya tovuti ya asasi yako ikikubaliwa. Hata wakati unashubiri tathmini ya watendaji wa Envaya, unaweza kuendelea kuhariri tovuti yako na kuongeza kurasa nyingine na habari kuhusu shirika lako, kama itakavyoelezwa katika kurasa zifuatazo. |
Translation History
|