Base (Igiswayire) | Kiswahili |
---|---|
Shirika la TWSEDHRO lilianzishwa lini? Tanzania Women Social Economic Development and Human rights Organization ni shirika lisilo la Kiserikali, ambalo linafanya au kutoa huduma zake bila kujali rangi, kabila Utaifa,au hali ya mtu pia ni shirika lisilo la kidini au siasa. Shirika hili lilianzishwa mwaka 2001 na lilianza kufanya kazi zake mwaka 2003. Shirika hili pia liliandikishwa November 2004 na kupata hati ya usajili Namba SO. 12861,toka Wizara ya mambo ya ndani ya nchi. Walengwa wakuu wa shirika hili ni nani? Walengwa wakuu wa shirika hili ni, wanawake maskini, wajane, walioachika, walemavu, wanawake wakimbizi, watoto yatima na wale wanaoishi katika manzingira magumu na mazingira magumu zaidi. Dira ya shirika hili ni: Kuwa shirika linalo jali, kutetea na kulinda Haki za Binadamu, hasa haki za wanawake na watoto katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania..
Dhamira ( Mission) Kusaidia, kutetea na kupambana dhidi ya ukiukwaji wa haki za Binadamu, haswa haki za wanawake na watoto na kutoa huduma za kijamii kama vile elimu, afya, misaada ya kiutu, kuimarisha hali ya uchumi kwa wanawake na kuboresha hali ya maisha ya wanachama na jamii kwa ujumla. Eneo la kazi za Shirika: Kwa mjibu wa katiba ya shirika la TWSEDHRO, shirika hili ni shirika la KItaifa lenye uwezo wa kufanya kazi eneo lolote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hata hivyo kwa sasa shirika limefanikiwa kufungua taw katika Wilaya yaKasulu. Mpango wa mbeleni ni kufungua ofisi katika wilaya ya Kibondo, Mkoa wa Shinyanga, Mwanza, Kagera Kilimanjaro na Dar es Salaam, Malengo/ Madhumuni ya TWSEDHRO ni: 1. Kutoa elimu na mafunzo (semina, Warsha) Ushawishi juu ya haki za binadamu ambazo ni haki za wanawake na watoto na utawala bora ili kudumisha haki hizo. 2. Kutoa huduma zaa afya kupitia vituo vya utoaji huduma za fya vilivyo/vitakavyokuwa chini ya shirika hili, pamoja na kutoa elimu juu ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango, magonjwa kama vile malaria na VVU/Ukimwi 3. Kutoa huduma za kiutu kw watoto yatima, wajane, wazee na watu wenye ulemavu na wahanga wa majanga mbalimbali. 4. Kutoa elimu na mafunzo ya ufundi staid kama vile elimu ya awali, msingi,na sekondari, kwa ama kujenga shule au kulipia ada wanafunzi . Kutoa mafunzo ya computer, ushonaji, ufumaji n.k. kutoa mikopo midogomidogo na kuwawezesha wanwake kushiriki katika shughuri za kiuchumi, kujenga vituo vya maendeleo ya wanawake na watoto ili punguza umaskini miongoni mwa jamii.
|
(Not translated) |
Kugirango ugire icyo uhindura kubyo wasemuye, ugomba kwinjira mu rubuga Injira · Iyandikishe