Log in

Translations: Kiswahili (sw): User Content: WI00096CAF72CC4000121204:content

« Previous   ·   Next »
Base (Swahili) Kiswahili

Dira ya kitaifa iliwekwa na umoja wa mataifa mwaka 1982 kwamba wazee washirikishwe katika mipango ya maendeleo. Mwaka 1999 serikali ya Tanzania iliamua kuwa na sera ya Taifa ya wazee. Mwaka 2002, mpango huu wa kimataifa ulifanyiwa mapitio kubaini matatizo na mahitaji ya wazee karne ya 21.

 Saidia Wazee Tanzania, shirika la kitaifa, ilianzishwa tarehe 21 machi,1994. Saidia wazee Tanzania – Mara (SAWATA MARA) ni tawi la Saidia Wazee Tanzania, (kitaifa). Lililoandikishwa na Wizara ya Mambo ya Ndani kumbukumbu na. SO 8039.

 Shughuli za asasi

SAWATA MARA ilianza shughuli zake rasmi Mkoani Mara tarehe 15 Julai 2000 baada ya kuundwa mwaka 1998. Tarahe 28/03/2001, asasi hii ilizinduliwa rasmi na Mheshimiwa mama Maria Nyerere hapa mjini Musoma.

Matawi na wanachama.

SAWATA MARA ilianzishwa na wanachama 22 wanaume 12 na wanawake 10. kwa sasa kuna matawi madogo 34. katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Vijijini, kuna matawi 26 Halmashauri ya Manispaa ya Musoma Mjini, matawi 3. Halmashauri ya Wilaya ya Bunda matawi 3 na Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ni Matawi 2. Yote yana jumla ya wanachama 680.wanaume 310 na wanawake 370.

Miradi

Katika uhai wa asasi hii tumefanikiwa kuendesha miradi mitatu yenye ufadhili

  • Maradi wa kwanza ni ujenzi wa Nyumba 15 kwa wazee 15 wa Halmashauri ya Wilaya Musoma Vijijini, kwa wazee wasiojiweza katika vijiji vya Butata, Bisumwa na Busilime. Tulifadhiliwa na visiwa vya jessy kupitia HelpAge international (HAI). Mradi huu ulikuwa wa Tshs. 12,580,000/- kwa kipindi cha tarehe 01/06/2003 hadi 30/05/2004. Ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa Nyumba ulifanyika na kupata hati safi kutoka kwa wakaguzi DH KATO & COMPANY wa S.L.P. 1289 DAR ES SALAAM ya tarehe 13th Julai, 2004.
  • Mradi wa pili, kupitia HelpAge International (HAI) ofisi ya Tanzania                                   Mradi wa pili ulikuwa ni kuelemisha wazee juu ya kujikwamua kiuchumi na uundaji wa mabaraza ya wazee katika Kata ya Suguti, mwaka 2006 hadi 2009 kwa ufadhili wa HAI.

  Mashindano ya shule

 Katika mwaka 2007/2008 SAWATA MARA ilianzisha mradi wa kushindanisha shule za Msingi kuchora picha zinazoonyesha maisha ya wazee.Vilevile Shuel za Sekondari zilishindanishwa kuandika insha juu ya maisha ya wazee.

 Mashindano ya kubuni na kuandika miradi inayoweza kutoa elimu ya sera ya Taifa ya wazee. Katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Vijijini Kuhamasisha jamii na viongozi kushirikiana na vyombo vya habari na mitandao.

      Utetezi na ushawishi

Kutetea na kushawishi Bunge lipitishe sheria kuhusu wazee kukomesha vitendo vya kikatili kwa wazee, mauaji ya wazee kwa imani za kishirikina. Kukusanya takwimu za kuaminika kuhusu wazee. Kuhamasisha wazee kudai haki zao za msingi ilikufikio mwaka 2012 wawe na uwakilishi katika vikao vyote katika ngazi zote za maamuzi, katika ngazi za Mitaa/Vijijini, Kata, Wilaya na hata Taifa.

Mtandao salama:

SAWATA MARA imewahi kutoa misaada mbalimbali kwa wazee wasiojiweza.

 Nguo na viandarua.

Mwaka 2004 SAWATA MARA ilitoa nguo kwa wazee 20 wasiojiweza. Mwaka 2005 SAWATA MARA ilitoa msaada wa chakula, mafuta ya taa na vibatari kwa wazee 25 wa Suguti wasiojiweza katika sherehe kwa mwaka huo, iliyofanyika Chitare, Kata ya Makoja, wazee 10 wasiojiweza walipatiwa nguo. Mwaka 2009, wazee 40 wasiojiweza wa Manispaa ya Musoma walipatiwa shuka 40 zilizotolewa na Mheshimawa Vedastus Mathayo (Mbunge) na viandarua 40 vilivyotolewa na “Red Cross Society” ya  Manispaa ya Musoma.

  • Matibabu

Katika sherehe ya siku ya wazee Duniani ya mwaka 2010 Wilayani Serengeti, (Kimkoa) SAWATA MARA kwa kushirikiana na Mganga Mkuu wa hospitali ya Mkoa wa Mara wazee 102 walipata huduma ya macho. Yaani wanume 54 na wanawake 48. Wazee waliopewa miwani ni 28. Wazee 71 walipewa dawa za kutumia Nyumbani.


 Mradi wa tatu

Mradi wa Elimu ya sera ya wazee

Katika mwaka 2011, kuanzia tarehe 1 Agosti 2011 hadi tarehe 31 Octoba 2011. SAWATA MARA ilitekeleza mradi wa Elimu ya sera ya wazee. Mradi huu ulifaahiliwa na The Foundation for civil seciety – Tanzania wenye thamani ya Tshs 7,395,000/-. ulitekelezwa Mkoani Mara, Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Vijijini, Kata za Bukima, Nyambono, Kyanyari na Bwiregi. Elimu iliyotolewa ni:-

  • Elimu ya sera ya Taifa ya wazee
  • Elimu ya ujasiriamali
  • Sheria ya mfuko wa Bima ya Afya ya jamii.

 Lengo lilikuwa ni kufikia wazee 80 katika mafunzo hayo. Wazee 83 walifikiwa katika Kata zote sawa na asilimia 103.75.

  • Kuunda mabaraza

Shughuli mojawapo katika mradi huu, ilikuwa kuunda mabaraza ya wazee ili waweze kupata uwakilishi katika vikao vya maamuzi. Mabaraza yaliundwa kuanzia ngazi ya Kitongoji Kijiji, na Kata. Mabaraza yaliyoundwa yalifanyika  15 kati ya 16 sawa na asilimia 93.75, kwa Kata zote.

  • Kutoa Elimu kwa Viongozi

Elimu ilitolewa kwa Viongozi wa mabaraza na Viongozi wa Kata, ni watu 33 sawa na asilimia 91.7 (wanaume 25 na wanawake 8) kati ya walengwa wote 36.

Walengwa wote

  • Walengwa wote waliotarajiwa kufikiwa ni wazee 4,000, waliofikiwa moja kwa moja ni 1,566 (wanaume 929 na wanawake 637) sawa na asilimia 39.15 na wasio wa moja kwa moja ni 2,434 (wanaume 951 na wanawake 1,483).

 

 

 

(Not translated)

In order to edit translations, you need to log in. Log in · Register