Asili (Kiswahili) | Kiswahili |
---|---|
ELIMU DUNI YA FEDHA INAWAATHIRI WANAKOPAJI BENKI… October 10 hadi 13 mwaka huu, ilikuwa ni wiki ya huduma za kifedhana uwekezaji, iliyofanyika jijini Dar es salaam. Katika maonyesho hayo hakuwepo kwa taarifa maalumu ya kuonyesha idadi ya washiriki, lakini ilionekana kuwa na washiriki wengi katika wiki hiyo. Inawezekana idadi kubwa ya washiriki ilikuwepo kutokana na kutokuwepo kiingilio,pia na kutolewa bure kwa elimu iyo ya ujasiria mali kwenye mabanda zaidi ya matatu kwnye viwanja hivyo. “nimejua mengi kuhusu namna gani naweza kupata mikopo na jinsi ya kusimamia biashara yangu katika hali ambayo itanipa ufanisi wa kudumu”. “mimi n mjane,nina watoto wa tatu ambao nawatunza na nimekuwa nahangaika kupata mkopo, nafuga kuku, ambao nafikiri sasa nahitaji mkopo ili nikuze mtaji wangu” anasema Muro. Anasema ipo haja ya wiki ya huduma za fedha zikaendeshwa katika maeneo mengine nchini ili kuwasaidia watanzania wengi zaidi ambao tafiti zinaonyesha kwamba hawana ujuzi wa kusimamia fedha zao kwa ufasaha.
ELIMU DUNI NI CHANZO CHA WAKOPAJI KUTOREJESHA MIKOPO. Muro anasema kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu elimu ya fedha, kumesababisha watu wengi kushindwa kulipa madeni wanaokpa benki. “nilichogundua kwenye wiki hii ya fedha ni kwamba taasisi nyingi za mikopo nchini zimekuwa hazitoi elimu nzuri ya mikopo , na taasisi hizo zinafanya hivyo kwa lengo la kuwadhulumu hasa katika marejesho na kupitia riba za mkopo, lakini hakupewa elimu jinsi atakavyoendesha biashara yakeau kusimamia fedha yake sawasawa..”
MAMBO MUHIMU KABLA YA KUKOPA MKOPO.. Taarifa ya taasisi ya Bogach Finance Co.Ltd inaeleza kwamba ni lazima mkopaji awe na sababu ya uhakika ya kuchukua mkopo huo, kabla ya kuamua kufanya hivyo. Bogach Finance Co. Ltd imekwa ikitoa mikopo kwa ajili ya watakaotaka kujiendeleza kielimu, kulipia pango la nyumba,kununua viwanja na huduma za mikopo kwa vikundi. Kampuni hiyo imebainisha kwamba siri moja ya kuw a na mafanikio mazuri yatokanayo na mkopo ni kutimiza malengo ambayo muombaji anakuwa amejiwekea kabla ya kuamua kukopa. Baadhi ya wakopaji wamebaini kwamba zipo taasisi ambazo zinatoa mikopo bila kubainisha aina ya riba wanatozwa katika mikopo wanayotaka. Mfanyabiashara wa soko l kariakoo Jonathan Kihaule , ambaye alikwenda kwenye wiki ya huduma ya fedha , alisema kuna benki zimekuwa zikifurahia wakopaji kutokuwa na elimu ya mikopo. “nilichogundua baada ya mafunzo, kutokuwa na elimu ya kifedha kunasababisha matatizomengi katika maisha. Kwa mfano mtu anaeza kukimbilia riba ya asilimia mbili kwa mwezi, ambayo ukichanganua ni sawa na asilimia 24 kwa mwaka na kuacha riba ya asilimia 10 kwa mwakaambayo ni nafuu” Anasema kihaule. Mfanyabiashara huyo amewashauri watanzania kujua muda wa marejesho ya mkopo, masharti ya riba kabla ya kukimbilia kukopa kwa kuwa kadri muda wa kurejesha mkopo unapokuwa mrefu riba pia inakuwa kubwa. Kwa mfano, mkopo wa sh5 milion unatozwa riba ya 24% kwa mwaka ukitaka ukatwe ndani ya miaka mitatu riba itakuwa 964,000 lakini watu wengi hawana ufahamu kuhusu hilo.
NI KOSA LA TAASISI ZA FEDHA KUTOA SIRI. Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wakopaji kwamba baadhi ya taasisi zimekuwa zikiwatangaza watu wanaokopa mikopo katika taasisi hizo jambo ambalo kampuni ya huduma ya fedha ya Finscope Survey imeonya tabia hiyo. Finscope Survey inakiri kwamba watoa mikopo wamekuwa wakitangaza taarifa za wateja wao kwa watu wengine na kukiukasheria za mikopo ya Benki Kuu ya Tanzania( BOT Act2007). Taarifa za mkopaji zinatakiwa kuwa siri kati ya ofisi ya mkopo na mteja wake kwani kutoa siri ya mtu mwingine ni kinyume cha sheria.
TAFAKARI DHAMANA YA KUWEKA KABLA YA KUKOPA. Mchambuzi wa maswala ya uchumi kutoka Zanzibar, Hawa Maljuni, anasema mkopaji yoyote anatakiwa kuwaza kwa makini kuhusu dhamana ya kuweka hasa kwa mikopo inayotaka mkopaji kuweka nyumba, gari au biashara kama dhamana kabla ya kupewa mkopo. “kuna watu wengine wamepoteza gari, nyumba baada ya kuweka dhamana ili wapate mkopo. Ukweli ni kwamba unatakiwa kuweka gari au nyumba yako iwapo tu una uhakika kwamba una uwezo mkubwa wa kurudisha deni kwa wakati” anasema Hawa. Kama una wasiwasi kuhusu kurejesha mkopo usikubali kuweka dhamana ya gari au nyumba. Pia imebainika asilimia 21 tu ya wakazi wajiji la dare s salaam na vitongoji vyake wana elimu ya usimamizi wa fedha huku asilimia 48 wana ufahamu wa kuweka akiba, hii ni kwa mujibu wa utafiti uliyofanywa na taasisi ya kifedha ya Finscope . Kwa mujibu wa ofisa mmoja wa taasisi hiyo, Ally Goronya, karibu asilimia 80 ya wananchi wote jijini dar es salaam hawana ufahamu kuhusu maswala ya mkopo. Utafiti unabahinisha, asilimia 54 ya wanawake wote jijini dare s salaam wanaochukua mkopo wengi wao wameishia kunyang’anywa dhamana wanazoweka ili kufidia fedha wanazokopa. Kwa mfano, vyombo vya ndani, kama friji na mali nyinginezimekuwa zikichukuliwana taasisi za fedha kutokana na wakoaji kuwa na elimu duni ya kutunza fedha na kurudisha kwa wakati. Utafiti huo ulifanyika mwaka 2009 na kubaini kuwa kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu fedha kumesababisha watanzania wengi kushindwa kufikia malengo ambayo wameweka kabla ya kuchukua mkopo. Wateja wengi wanachukua mikopo wamekuwa wakidhulumiwa haki zao kwa sababu hawana elimu ya kutosha kuhusu fedha. Mratibu wa wiki ya huduma za fedha, Godfrey Kivamba,anasema zaidi ya wajasiria mali 1600 walihudhuria na kupatiwa mafunzo, na jitihada zinafanyika kuhakikisha watu wengi wanapatiwa elimu. Anasema lengo la mpango huo ni kutoa elimu kuhusumatumizi bora ya taasisi za fedha hasa suala la mkopo kwa kuwa wananchi wengi nchini hawana elimu ya kutosha, ukilinganisha na nchi kama Kenya, Uganda, Rwanda, na nyingine nyingi za Afrika. Mafunzo yaliyotolewa na pamoja na kutambua jinsi ya kufungua kampuni, mikopo na biashara. Ofisa mikopo wa wajasiriamali wadogo katika benki ya CRDB, Frank Peter, anasema wajasiriamali wanakabiliwa na matatizo ya mitaji na kukosa elimu sahihi kuhusu jinsi ya kukopa katika taasisi za fedha. Chanzo: Mwananchi, oct 18 2012 |
(Bila tafsiri) |
Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe