Base (Swahili) | English |
---|---|
JIKWAMUE DEVELOPMENT ASSOCIATION-JIDA YAJIKWAMUA Asasi hii inastahili pongezi kubwa kwa mafanikio iliyoyapata tokea kuanzishwa kwake hadi mwaka 2014. Mwaka 2013,JIDA,imefanikiwa kuandaa Mradi wa Mafunzo ya Ufuatiliaji wa Matumizi ya fedha za Umma za Sekta ya Elimu katika Kata 6 za Halmashauri ya Wilaya Morogoro Vijijini ambazo ni Mtombozi,Kisemu,Tawa,Konde,Mvuha na Selembala, Mafunzo ambayo yaliwashirikisha Wanufaika 90,katika maana ya kwamba kila Kata iliwakilishwa na washiriki 15. Mafunzo haya yaliandaliwa na JIDA kwa Ufadhili wa Foundation for Civil society,Mradi huu umeleta mafanikio makubwa sana kwa Jamii kwa kupata Elimu ya Mbinu au Stadi za Ufuatiliaji wa fedha za Umma,bali pia Jamii imetambua kuwa ni wajibu wao pia kuzisimamia fedha za Umma,ikiwemo kupanga,kusimamia,kufuatilia na kupima ubora wa bidhaa au huduma ilyotolewa. Jikwamue Devel.Assoc.kupitia Mpango Mkakati wake ulioanza 2011 na kuishia 2013 imeweza kufanikiwa kutekeleza Azima yao ya kuwa na Ofisi kubwa na ya Kisasa,Kwa kuwa jida imejengga Heshima kubwa katika Jamii si ya Kijiji cha Tambuu Pekee na Nje ya Kata ya Lundi,hitajio hili la kuwa na Ofisi yetu wenyewe liliungwa Mkono na Wananchi wa Kijiji cha Tambuu na Viongozi wa Kijiji hicho akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji hicho ndugu Hassani Dege,kwa mafanikio haya yote mimi ninawapongeza sana JIDA. |
(Not translated) |