Base (Swahili) | English |
---|---|
asasi ilianza mwaka 2009 na lilipata usajili rasmi mwaka 2012 kwa namba 95109. ilikua ni wazo kutoka kwa habiba swedi, mtangazaji na mwandishi wa habari aliyeona kuna haja ya kuwa na asasi hii ya kiraia ili kuweza kuisaidia jamii hasa ya wanawake na watoto kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa elimu kwa watoto wao. wanawake masikini wanaolea watoto pekee yao wanazochangamoto katika kuwawezesha watoto wao hususan yatima kupata elimu. kumekuwepo pia na changamoto ya baadhi ya wazazi wa kiume na familia ya mume kwa ujumla kumtelekeza mtoto mwenye ulemavu kwa madai ya kuwa mtoto huyo ni laana ya mama yake. hivyo wanawake wengi kuachwa wakihangaika na watoto wao wenye ulemavu hata kushindwa kuwasomesha. kuna changamoto pia ya wajane kurubuniwa hata kudiriki kuuza mali walizoachiwa na marehemu waume zao na kuolewa na wanaume wengine, na kisha kutelekezwa na vichanga baada ya kufilisika. ama changamoto ni nyingi zilizopelekea asasi hii kuanzishwa, lakini kazi kubwa tunayoifanya ni kutoa elimu kwa wanawake na watoto wa kike ili wajitambue. |
(Not translated) |