Asili (Kiswahili) | Kiswahili |
---|---|
MADHUMUNI1.1.1 Kusaidia jamii wakati wa maafa na/au majanga mbalimbali. 1.1.2 Kusaidia wakati wa shughuli mbalimbali za kijamii na kiutamaduni. 1.1.3 Kubuni program zitakazohusisha ajira rasmi na zisizorasmi zinanohusu uzalishaji Mali na huduma. 1.1.4 Kubuni mikakati mbalimbali itakayoweza kuimarisha maendelao ya Elimu miongoni mwa Wananchi watokao Wilayani Lushoto. 1.1.5 Kuonyesha kwa vitendo katika kuwajali watu walioathirika na kuathiriwa na UKIMWI na WALEMAVU. 1.1.6 Kukuza ajira miongoni mwa Vijana na Wananchi kwa njia ya Kilimo, Ufugaji na Biashara. 1.1.7 Kujenga mahusiano na Taasisi za ndani na nje ya nchi ili kuleta mahusiano kati ya CHAMA na Taasisi husika. 1.1.8 Kuboresha uhifadhi na kuonyesha kwa vitendo katika kujali Ulinzi wa Mazingira. 1.1.9 Kushiriki katika kubuni, kupanga na kutekeleza mipango mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa. 1.1.10 Kuhamasisha jamii mbalimbali ili kujiunga na vyama vya Akiba na Mikopo yaani Savings and Credit Cooperative Society (SACCOS). 1.1.11 Kuendesha Makongamano, Warsha, Semina, Majadiliano na Mikutano inayohusu maswala mbalimbali ya Michezo na Maendeleo. 1.1.12 Kuhimiza utunzaji wa vyanzo vya Mito, Upandaji wa Miti na utunzaji Mazingira.
1.2 KAZI1.2.1 Kuhamasisha utoaji wa Michango itakayo wezesha Ujenzi wa Shule:Za Awali,Msingi,Sekondari,Vyuo,Vituo vya Afya na Zahanati Wilayani Lushoto pamoja na sehamu mbalimbali za nchi. 1.2.2 Kuhamasisha Uanzishwaji wa Vituo vya kulelea Watoto Yatima,na waishio Mazingira hatarishi.Na Vituo vya Ushauri nasaha kuhusu magonjwa ya Ukimwi. 1.2.3 Kuanzisha Mfuko wa Jamii kwa ajili ya kusaidia Wajane, Wazee, Vijana na Yatima. 1.2.4 Kuainisha na Kuwezesha utekelezaji wa Program za Mafunzo kuendeleza Vijana na Watoto katika kupanua Vipaji vyao maalumu kimichezo. 1.2.5 Kuwasiliana na Mashirika yaliyoko ndani na nje katika kusaidia Madhumuni na Malengo ya CHAMAKIVU. 1.2.6 Kutoa Elimu ya Ujasiliamali kwa lengo la kuboresha Kilimo, Ufugaji, Biashara na utoaji wa Huduma mbalimbali. 1.2.7 Kuendesha Makongamano, Warsha, Semina, Majadiliano na Mikutano mbalimbali inayo husu Maendeleo. 1.2.8 Kuwa Wadhamini kwa Wanachama walengwa wote wa CHAMAKIVU katika uwezeshaji wa Mikopo na/au Utoaji wa Mikopo kulingana na Taratibu za CHAMA. |
(Bila tafsiri) |
Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe