Envaya

/AFSC/post/5: Kiswahili: CMBKqUgDhNTPWBCmK5DYNmfZ:content

Asili (Kiswahili) Kiswahili
Madawa ya asili ni mengi ila bado hajafanyiwa utafiti wa kutosha kuhusu aina ya wadudu na magonjwa ninayotibu, jinsi ya kutumia na kiasi cha kutumia. Baadhi ya mimiea inayotoa madawa ya asili ni mbegu na majani ya muarobaini, tumbaku, pilipili kali, pareto, kitunguu swaumu, manung'anung'a, n.k. Muarobaini ni miongoni mwa mimea michahce ambayo mpaka sasa imefanyiwa utafiti wa kiina. Mfano, kuchanganya nusu kilo ya mbegu za muarobaini zilizotwangwa katika lita ishirini za maji husaidia kuua wadudu mbalimbali wakiwemo funza wanaotoboa matunda ya nyanya.

Madawa ya asili ni bora zaidi kuliko madawa ya viwandani kwani sumu yake ni kidogo na hupungua haraka baada ya kupiga dawa. Hivyo ni salama zaidi kwa mpigaji dawa na mlaji mboga. Hivyo kupendekezwa katika kilimo hai na hifadhi ya mazingira.

Kasoro kubwa katika kutumia madawa ya asili ni kwamba hayajafanyiwa utafiti wa kutosha ukilinganisha na yale ya viwandani. Mfano, nitumie dawa ipi inayofaa kwa mdudu yupi?. Nguvu yake ni kidogo, hayatafaa kuzuia mashambulizi makubwa ya magonjwa au wadudu vilevile yanakinga zaidi mboga dhidi ya wadudu waharibifu kuliko magonjwa.Pia uwiano wa kuchanganya dawa na maji bado haujulikani vizuri. Mfano, niweke kiasi gani cha dawa katika kiasi gani cha maji ?..
(Bila tafsiri)

Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe