Asili ((unknown language)) |
Kiswahili |
Kwa mara nyingine tena wakati tunapokaribia kuanza mwaka mpya wa fedha wa 2014 kulingana na kalenda ya TALISDA Foundation, Shirika hilo linatangaza nafasi za Kazi kama ifuatavyo: 1. Afisa wa Ufuatiliaji na Tathimini (Monitoring and Evaluation Officer) nafasi moja Sifa: Mwombaji awe na Elimu ya Shahada ya kwanza au zaidi katika kada ya takwimu,uchumi, mipango kazi au kada nyinginezo zinazofanana na hizo Mwombaji awe na uzoefu usiopungua miaka miwili katika tasnia ya ufuatiliaji na tathimini ya miradi ya jamii. Mwombaji awe na uwezo wa Kuandika ,kusoma na kuongea lugha ya kiingereza kwa ufasaha. 2. Afisa wa shughuli za uimarishaji uchumi ( Economic Strengthening Officer) Sifa: Mwombaji awe na elimu ya Shahada ya kwanza au zaidi katika mambo ya uchumi , maendeleo ya jamii au kada inayofanana na shughuli za uimarishaji uchumi hususan katika ngazi ya vikundi na kaya. MUHIMU: Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia Email: talisda_foundation @yahoo.com Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 26.09.2013
|
|