Fungua

/tahco/topic/123681: Kiswahili: dMQvSXzCQI8925rCCa8doh96:content

« Iliyotangulia   ·   Ifuatayo »
Asili (Kiingereza) Kiswahili

Ndugu wapendwa wenye moyo wa kujitolea na kujaribu kupambana na jambo la watoto wa mitaani,mnadhani ni jambo gani ambalo linafanya kuongezeka siku hadi siku idadi kubwa ya watoto wa mitaani?na tunafanya nini kupunguza ama kutokomeza jambo hili?

huwa napatwa na uchungu napowaona watoto hawa wakiwa barabarani wakisubiri folen ili waombe kwenye magari,roho inaniuma sana ukizingatia hata maeneo yao ya kulala imekuwa shida kwao,nimejaribu kufanya research juu ya jambo hili,nikakaa na baadhi ya watoto hawa nikawauliza kuhusu upatikanaji wa chakula na mahitaji mengine ambayo ni muhimu kwao kuyapata nikaona bado ni shida nyingi na changamoto nyingi wanakutana nazo.

TUJITAHIDI KUTETEA NA KUWASAIDIA WATOTO HAWA ILI NAO WAPATE FURAHA NA MATUMAINI MAPYA.

(Bila tafsiri)

Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe