Asili (Kiswahili) | Kiswahili |
---|---|
Taasisi ya kupambana na UKIMWI Kitangari ilianzishwa mwaka 2007,na ilipata usajili wa kudumu Aprili 2008. Asasi hii imeweza kuendesha mafunzo ya aina mbili. 1.Imeendesha mafunzo ya kujenga Uelewa wa Ugonjwa wa UKIMWI kwa wasichana wenye umri kati ya miaka 11-20 kwa Ufadhili wa RFA-Mtwara. Kata iliyonufaika na mafunzo hayo ni MNYAMBE wilaya ya Newala. 2.Imeendesha mafunzo ya UNASIHI NA UPIMAJI WA HIARI WA VIRUSI VYA UKIMWI. Kata zilizonufaika na mafunzo hayo ni Kitangari na Maputi. Mafunzo hayo yaliwashirikisha Wakunga wa Jadi,Wasichana,akina mama,Wazee,Walemavu wa aina mbalimbali na akina baba.Mafunzo haya yalifadhiliwa na The Foundation for Civil Society mwaka 2009.
|
(Bila tafsiri) |
Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe