Base (Swahili) | English |
---|---|
MAFUNZO YA UJASIRIAMALI YANAYOENDESHWA NA MTANDAO WA VIJANA (TEYODEN) YAENDELEA KATIKA WIKI YA TATU. Sasa imeshafikia wiki ya tatu toka mafunzo ya anzisha na kuza wazo lako la biashara yanayoendeshwa na TEYODEN hapa,Temeke kwa kushirikiana na mwezeshaji kutoka I.L.O yanayosimamiwa na asasi ya Restless Tanzania. Mafunzo haya yanachukua wastani wa wiki moja kwa kila kundi la vijana 30.Mpaka sasa tumefikia vijana 60 kutoka katika kata 3 ambazo ni Chang’ombe,Keko na kata ya Kijichi.Shabaha yetu hasa ni kufikia vijana 300 kutoka katika kata zote 30 za manispaa ya Temeke,wafikirie vyema mawazo yao ya biashara,wayakuze na yawezeshe ajira kwao na kwa vijana wengine. Tathmini ndogo tuliyofanya kwa walengwa waliopatiwa mafunzo haya,wanasema kuwa, hakujawahi kufanyika kwa mafunzo mazuri ya ujasiriamali kama haya ya wakati huu.Hivyo wanawashauri vijana wengine wa Manispaa ya Temeke kujitokeza na kutumia fulsa hii. Utaratibu wa kuomba nafasi hii ya kuwa mmoja wa vijana 300 watakaowezeshwa kupata nafasi ya kuelimishwa ni pamoja na kuchukua fomu,kuijaza na kuirudisha katika ofisi za TEYODEN zilizopo Mtaa wa Bora,karibu na TRA,Katika jengo la Afisa Mtendaji wa kata ya Chang’ombe tunawakaribisha sana vijana wote. |
Entrepreneurship training run by Youth Network (TEYODEN) CONTINUES IN THREE WEEKS. Now has made further inroads third week started out training and promote your idea and run business TEYODEN here, Temeke in conjunction with a facilitator from the ILO-supervised institution Restless Tanzania. This tutorial takes approximately one week for each group of teenagers 30.Mpaka now we have reached 60 youth from County 3 which is Chang'ombe, Keko and county of Our Kijichi.Shabaha exactly to 300 young people from all 30 county municipalities of Temeke, think positively their business ideas, and yawezeshe wayakuze their jobs and for other young people. Small evaluation we did for these beneficiaries trained, they say, there has never been done for good training in entrepreneurship as these when u.Hivyo advise other young emerging Temeke Municipal and use this fulsa. Procedure to apply for this opportunity to be one of 300 young people who were given a chance to be educated well and take the form, fill and return it in an existing office TEYODEN Bora Street, close to the TRA, in the building of the County Executive Officer Chang'ombe we welcome both very young. |
Translation History
|