Envaya

/MANGONET/post/20993: Kiswahili: WIjzphlRNoPZxVzsWQ2cOFYU:content

Asili (Kiswahili) Kiswahili

TAARIFA FUPI YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UTETEZI, JINSIA NA UKIMWI.

Mtandao wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Wilayani Masasi (MANGONET) umetekeleza mradi wa kupambana na maambukizi ya UKIMWI kupitia shughuli za utetezi jinsia na UKIMWI chini ya ufadhili wa shirika la Ujerumani GIZ.

Kwa mkoa wa Mtwara mradi huu umetekelezwa katika Wilaya mbili za Masasi (MANGONET) na Manispaa ya Mtwara (MTWANGONET) baada ya utafiti mbalimbali kuonyesha kuwa maeneo haya yameathiriwa sana na maambukizi ya UKIMWI. Mradi huu umefanywa kwa muda wa miaka miwili, yaani kuanzia Octoba 2010 hadi Septemba 2012.

Kwa MANGONET mradi umefanyika kwa Asasi 6 ikiwemo MANGONET yenyewe asasi hizo ni kama ilivyoonyeshwa kwenye kiambatanisho.

 

 

 

 

 

(Bila tafsiri)

Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe