Base (Igiswayire) | Kinyarwanda |
---|---|
MARAFIKI WAJADILI NAMNA YA KUBORESHA MMES II- MOROGOROWawakilishi wa harakati za Marafiki wa Elimu kutoka kanda tatu za Mashariki, Kusini na Nyanda za juu Kusini; walikutana mjini Morogoro kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu mustakabali wa Elimu na namna nzuri ya kuboresha ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Elimu. Aidha washiriki hao waliipongeza Serikali kwa juhudi zake za kuboresha kiwango cha Elimu kupitia mipango yake ya maendeleo ya Elimu kama MMEM I&II, MMES I&II na Mafunzo ya Ualimu Kazini (TDMS). Wanaharakati hao walitambua mafanikio ya mipango hiyo kuwa ni pamoja na kufanikiwa kujenga shule nyingi za msingi na sekondari, ongezeko kubwa la uandikishaji wa watoto katika shule zetu, ongezeko la juhudi za kupeleka pesa shuleni kwa lengo la kuboresha hali ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika shule nyingi hapa nchini. Ushauri ulitolewa na wanaharakati hao kwa serikali kwamba; katika kutekeleza MMES II uliozinduliwa Januari 2011; ambao unalenga kuboresha kiwango cha elimu ya sekondari, uandikishaji wa wanafunzi, mfumo wa uongozi na mfumo wa ukaguzi; ni budi serikali iyafanyie kazi mapungufu yaliyojitokeza kwenye mipango iliyopita. Walitaja mapungufu yaliyojitokeza katika mipango iliyopita kuwa ni pamoja na udahili wa wanafunzi shuleni ambapo wanafunzi wenye hata chini ya alama 150 walichaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari, watendaji wa mipango hiyo hasa wakuu wa shule, bodi na kamati za shule kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusiana na mipango na kwa kiasi kikubwa wananchi ambao ndio wadau wakuu hawakuelimishwa wala kushirikishwa kama mpango unavyoeleza. Marafki wa Elimu kwa kauli moja waliazimia kuishauri serikali kutekeleza mambo 6 ambayo wanaamini kuwa kama yatafanyiwa kazi ipasavyo; mafanikio chanya yatapatikana katika maendeleo ya elimu haa nchini. Maazimio hayo ni pamoja na:-
Tamko hili la wanaharakati halina budi kuungwa mkono na wadau wote wapenda maendeleo ya Elimu nchini hasa kwa kuzingatia ushindani wa ubora wa Elimu tunaokabiliana nao hasa katika Muungano wetu wa Jumuia ya Shirikisho la Afrika Mashariki. |
(Not translated) |
Kugirango ugire icyo uhindura kubyo wasemuye, ugomba kwinjira mu rubuga Injira · Iyandikishe