Asili (Kiswahili) | Kiswahili |
---|---|
ELIMU YA STASDI ZA MAISHA. Mimba za utotoni na utumiaji wa dawa za kulevya nchini Tanzania limekuwa ni tatizo linalokuwa siku hadi siku.Takwimu zinaonesha kuwa watoto wenye umri kuanzia miaka 9-25,ndio wanaoathirika kwa kiwango kikubwa na tatizo hili. Mwaka 2008 katika shule ya msingi Ilagala mkoani Kigoma binti wa miaka tisa alionekana kuwa na ujauzito ,hali ambayo ilihatarisha maisha yake na kiumbe kilichokuwa tumboni.Mwaka 2006 wanafunzi 64 wa kike walioanza shule ya sekondari katika shule ya sekondari Ilagala,ni wanafunzi 4 tu waliobahatika kuhitimu kidato cha nne.Hapo unaweza kuona namna tatizo hili lilivyo kubwa. Asasi za kiraia na wadau wengine wa afya wanalojukumu la kutoa elimu kwa vijana wa shule za msingi,sekondari na wale walioko mitaani kwa lengo la kuwajengea stadi za kujitambua,kujiamini,kujithamini,na kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto zinazowakabili katika makuzi yao. Katika makuzi ya vijana,wamejikuta wakikabiliwa na shinikizo rika,hali ambayo imewaingiza baadhi yao katika matatizo.Miongoni mwa matatizo ambayo yanawakabili vijana kutokana na shinikizo rika ni pamoja na mimba za utotoni,utumiaji wa dawa za kulevya,ushoga,uchokoraa,na utumikishwaji katika biashara ya ngono. Somo la stadi za maisha limeonesha uwezo mkubwa wa kuwasaidia vijana wengi kukabiliana na changamoto zinazowakabili.Vijana wengi ambao walishaanza kutumia dawa za kulenvya na kujiingiza katika vitendo vya ngono katika umri mdogo,walijiondoa baada ya kupatiwa elimu ya stadi za maisha. Kwa wale ambao walikuwa hawajanza vitendo hivyo,baada ya kupatiwa elimu hiyo wamekuwa ni waelimishaji wazuri kwa wenzao,hali ambayo imesaidia kukuza uelewa wao kuhusiana na afya ya miili yao.Stadi za maisha ni mbinu au njia anazo tumia mtu katika kukabiliana na mazingira yanayomzunguka hatimaye abaki salama kimwili,kiroho na kiakili. Kwa kawaida stadi za maisha husaidia vijana kujiamini,kujithamini,kujiheshimu,kujitambua na kuwajenga uwezo wa kupambanua jambo baya na zuri na kufanya maamuzi sahihi pindi wanapokabiliwa na changamoto mbalimbali. Katika stadi za maisha tunawafundisha vijana kutatua matatizo kwa kutumia T3.Hii ina maana kuwa T1-----------tatizo T2-----------tatuzi T3----------tokeo Katika kupata tokeo la tatizo,kuna uwezekano tokeo likawa chanya au hasi.Kwa kutumia T3 kijana anaweza kutatua matatizo kimantiki zaidi,tofauti na ambaye hana elimu ya stadi hiyo,ambapo wengi wakabiliwapo na matatizo magumu hufikia hatua ya kujiua kwa kuamini kuwa matatizo kama hayo hayana utatuzi,hususani baada ya kufukuzwa nyumbani au kukataliwa na wenzi wao. Mada zifuatazo huwasaidia vijana kujitambua vizuri sana katika makuzi yao.
Vijana hupata habari nyingi ambazo nyingine ni potofu kwao.Kutokana na hilo ni vema wakapewa habari sahihi zinazohusu miili ya na makuzi yao.Mfano vijana wengi wa kike na wa kiume wanapata taarifa kuwa wasipofanya ngono mapema watapata matatizo wakiwa wakubwa,habari ambazo kwa hakika si sahihi na zinapotosha. Vilevile vijana hupenda kujaribu baadhi ya mambo ili kuona matokeo ama wanayo yasikia au kuona nini kitatokeo ya kufanya jambo fulani.Kutokana na hali hiyo wazazi,walezi,asasi za kiraia,azaki,na wadau wengine wanalojukumu la kutoa elimu kwao ili kuwaepusha na majaribio ambayo mwisho wake ni matatizo kwao. Jeanmedia imeliona hili na itashiriki kikamilifu kuhakikisha kuwa inawaandaa vijana bora kwa ajili ya kuwa viongozi mahiri wa kesho.Kwa kutambua ukubwa na ugumu wa tatizo hili,jeanmedia inawaomba wadau wote kuunga mkono juhudi hizi kwa kuiwezesha kwa hali na mali ili iweze kuwafikia vijana wengi wa mjini na vijijini. Nguvu kazi ya taifa lolote duniani ni vijana,hivyo wasipoandaliwa vizuri leo,kesho watakuwa bomu ambalo litakapolipuka litaangamiza taifa lote.Waafrika wanayo methali isemayo “mtoto umleavyo ndivyo akuavyo”,hivyo kama tunahitaji kuwa na kizazi bora chenye maadili,uzalendo na uwajibikaji tuanze kuwaandaa vijana sasa kisaikolojia,kimaadili,kifikra na kimtazamo.
ANTON MWITA KITERERI |
(Bila tafsiri) |
Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe