Base (Swahili) | English |
---|---|
Kutokana na hali hiyo,serikali,taasisi,mashirika na watu binafsi walijitoa kwa hali na mali kuhakikisha kuwa wahanga wa mafuriko wanasaidiwa,kwa kupatiwa malazi,mavazi na chakula.Maeneo yaliyoathirika zaidi kutokana na mafuriko hayo ni pamoja na kimara,mbezi,tabata,msewe na jangwani. Nyumba,miundo mbinu ya barabara na madaraja,viliharibiwa kabisa hali iliyopelekea kukatika kwa mawasiliano kati ya eneo moja na lingine. Kutokana na kuharibiwa kwa miundo mbinu hiyo,baadhi ya maeneo ya kazi yalikosa ufanisi,kutokana na ama wafanya kazi kuchelewa kufika kazini au kutofika kabisa. Athari ya mafuriko itaendelea kuwa kubwa iwapo hatua za makusudi hazitachuliwa hasa kwa wananchi wanaoishi sehemu za bondeni kwa kuwa idara ya hali ya hewa nchini imeelezea kuendelea kuwepo kwa mvua kubwa kati ya mwezi Februari na Machi.Baada ya mvua kusimama kwa muda baadhi ya changamoto mbalimbali zimeonekana kujitokeza.Moja ya changamoto hizo ni pamoja na uwezekano wa kuibuka kwa magonjwa ya mlipuko kama vile kuhara,kipindu pindu na magonjwa ya tumbo. Hali hii inatokana na uchafu uliokithiri katika maeneo hayo ya bondeni.Baadhi ya maeneo yameonekana kuwa na vinyesi ambavyo vilitapishwa wakati mvua ilipokuwa inanyesha. Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine,wana jukumu la kuhakikisha kuwa elimu ya mazingira inatolewa ili kuepuka madhara ambayo yatatoke baadae,iwapo hatua za makusudi hazitachuliwa kudhitibiti hali hiyo.Daima kinga ni bora kuliko tiba,ni vema utaratibu wa kudhitibi matatizo uzingatiwe kabla ya kutokea kwa tatizo,hali ambayo itasaidia kupunguza gharama zisizokuwa za lazima. Pamoja na serikali kuwataka wananchi wanaoishi sehemu za bondeni kuhama na kutafuta maeneo yaliyosalama kwa maisha na mali zao,bado uchunguzi unaonesha kuwa itakuwa ni vigumu kwa baadhi yao kuhama kutokana na ukweli kwamba,wananchi wengi hali zao za kimaisha ni duni sana.Mfano mkazi mmoja wa jangwani B amenukuliwa akisema kuwa yuko tayari kufia bondeni na hawezi kuhama kwa kuwa hana uwezo wa kufanya hivyo. wananchi hao ambao wengi wao huendesha maisha yao kwa kuokota makopo na kuyauza,inaonesha itakuwa ni vigumu kuwaondoa maeneo hayo kwa kuwa hawana njia nyingine mbadala ya kuwafanya wajikimu kimaisha. Katika kipindi hiki cha mpito,serikali,mashirika na watu binafsi wanalo jukumu la kuhakikisha kuwa upatikanaji wa huduma za afya unazingatiwa,kwa kutoa dawa za kutibu maji,vyandarua,sabuni pamoja na vyombo vya kupikia pale itakapobidi. Daima umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu,hivyo wadau kwa pamoja tuungane ili kuhakikisha kuwa tatizo lililojitokeza linakabiliwa.
ANTON MWITA KITERERI.
|
Given the situation, governments, institutions, organizations and individuals committed to state property to ensure that the flood victims are being assisted, to seek shelter, clothing and chakula.Maeneo most affected by the floods include Kimara, arrogant person, Tabata, child's rattle and deserts. Housing, infrastructure of roads and bridges, completely viliharibiwa situation leading up to disruptions in communication between one place and another. Due to the destruction of infrastructure, some areas of work yalikosa efficiency, due to either workers or helpers to work late at all. The effects of flooding will be great if deliberate steps not zitachuliwa especially for people living in parts of the valley to become the department's climate in the country reiterated the continued existence of the heavy rains between February and Machi.Baada the rain stop for a moment some of the challenges have been detected kujitokeza.Moja of these challenges include the possibility of the emergence of epidemic diseases such as diarrhea, recorded cholera and diseases of the stomach upside down. This is due to extreme dirt in these areas bondeni.Baadhi areas have proved that vilitapishwa faeces during rain was raining. Government in collaboration with other stakeholders, are responsible for ensuring that environmental education is provided in order to avoid side effects that yatatoke later, if deliberate steps not zitachuliwa kudhitibiti state hiyo.Daima prevention is better than cure, it is good procedure kudhitibi problems be considered before the problem, which will help reduce non-necessary expenses. With the government urging citizens living part of the valley to move to find places yaliyosalama to life and property, yet observation shows that it is difficult for some to move due to the fact that many citizens in their standard of living is low sana.Mfano resident one wilderness B has been quoted as saying that he is ready to die the valley and can not move because he has no power to do so. These people mostly run their lives by picking up cans and sell it, shows it is difficult to remove these areas because they have no alternative livelihood for them. During this period of transition, governments, organizations and individuals they have an obligation to ensure that access to health care is considered, by providing drugs to treat water, mosquito nets, soap and cooking utensils when itakapobidi. Always unity is strength and division is weakness, so let the stakeholders together to ensure that the problem arises faces. ANTON KITERERI ITA. |
Translation History
|