Base (Igiswayire) | Kinyarwanda |
---|---|
TAARIFA YA USHIRIKI KATIKA WIKI YA VIJANA NA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MWALIMU NYERERE YALIYOFANYIKA MKOA WA KIGOMA TAREHE 8-14 OCTOBER 2010. 1.0 UTANGULIZI TEYODEN kila mwaka imekuwa ikipata nafasi ya kushiriki katika maadhimishomya wiki ya vijana yanayokwenda sambamba na sherehe za kuzima mwenge na siku ambayo baba wa taifa la Tanzania, mwalimu Julius Kambarage Nyerere alifariki Dunia. Wiki hii inawaleta pamoja vijana kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania katika kumuenzi baba wa taifa katika yale aliyoyahimiza kutendeka hasa katika kupiga vita ukabila na kudumisha umoja wa kitaifa hivyo basi vijana hupata nafasi ya kuonyesha kazi zao za mikono, ujuzi wao na vilevile huduma wanazozitoa katika jamii. TEYODEN ilipata nafasi ya kuwakilishwa na kijana mmoja ambae ni katibu mkuu bwana YUSUPH KUTEGWA katika taarifa hii utapata nafasi ya kupata maelezo ya mchakato wa uwakilishi wa TEYODEN katika maadhimisho haya toka tarehe 8-14 Oktoba ya 2010.Pia itaonyesha mafanikio changamoto pamoja na mapendekezo ya mwakilishi ili kuboresha ushiriki wa mwakani. 2.0 MCHAKATO WA MAADHIMISHO 2.1 Malengo ya ushiriki wa TEYODEN katika maadhimisho · Kuonyesha shughuli za mikono za vijana wa manispaa ya Temeke hasa wanachama wa TEYODEN.\ · Kubadilishana ujuzi na uzoefu wa jinsi ya kufanya shughuli ujasiriamali na utoaji wa huduma kwa vijana. · Kujenga mtandao wa kubadilishana uzoefu na kupata taarifa mpya. 2.2 Shughuli zilizofanyika Katika maadhimisho ya mwaka huu TEYODEN ilionyesha bidhaa zilizogawaganyika kama ifuatavyo:- -Bidhaa za viwanda vidogovidogo nazo zilikuwa ni,majiko ya mkaa,majalo,vifaa vya kuchotea unga dukani,mifuniko,sahani za kukaangia na vijiko vya kukaangia samaki. -Bidhaa za ususi na hizi zilikuwa ni vikapu vizuri vya kinamama -Nguo pia tulionyesha ubunifu wa nguo nzuri za kinamama na watoto zilizofumwa kwa kutumia mikono. TEYODEN pia ilitoa elimu kwa vipeperushi,vijarida,vitabu na uraghibishi na elimu iliyotolewa ilihusu athari za dawa za kulevya,umuhimu wa ushiriki na ushirikishwaji wa vijana na V.V.U/UKIMWI. 3.0 MAFANIKIO Katika safari hii TEYODEN imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kama ifuatavyo:- 1. Imefanikiwa kuuza bidhaa zake na hasa kwa kuwa ilikuwa na bidhaa kwa kina mama na watoto. 2. Wastani wa vijana 342 walitembelea banda na kupata elimu zilizokuwa zikitolewa na kuchukua vijarida na vipeperushi ili kujisomea wakiwa nyumbani. 3. Tulipata nafasi ya kubadilishana mawazo na uzoefu na Kigoma Youth Network,Tume ya kuthibiti dawa za kulevya,FEMINA,VETA Kigoma,Vijana wa Halmashauri ya Singida,Poverty Fighters Group na TAYOHAG 4. Lakini pia kufika Kigoma na kutoa huduma zetu ni uzoefu ambao utakumbukwa sana. 4.0 CHANGAMOTO Katika utekelezaji wa jambo lolote huwa hakukosi changamoto hivyo basi katika uendeshaji wa shughuli zetu Kigoma changamoto kadhaa zilijitokeza. 1. Chakula kilikuwa ni ghali arafu mafuta ya mawese yalisababisha ugojwa kwangu kama mshiriki wa maadhimisho yale. 2. Shughuli za uchaguzi zilidhoofisha sherehe nzima kutokana na mwitikio wa watu kuwa mdogo. 5.0 MAPENDEKEZO Kuna mapendekezo kidogo ambayo mimi kama mshiriki ningependa kuyatoa 1. Wizara ,Halmashauri na taasisi zinazowezesha vijana zizingatie sana kuwa katika siku muhimu kama hii ushiriki wa vijana unahitajika sana na hivyo si vyema kuhamisha ofisi nzima badala ya vijana 6.0 HITIMISHO Wiki ya vijana ni muhimu sana hasa katika kukutanisha vijana na kuwafanya wawehuru kubadilishana mawazo na uzefu katika kazi zao za kila siku na kuleta ufanisi katika shughuli wnazozifanya.Kila mdau na aweke rasilimali za kutosha kuruhusu vijana kote nchini kushiriki siku hii muhimu sana kwa Taifa letu.
|
(Not translated) |
Kugirango ugire icyo uhindura kubyo wasemuye, ugomba kwinjira mu rubuga Injira · Iyandikishe