Base (Igiswayire) | Kinyarwanda |
---|---|
Wananchi watakiwa kutunza mazingira Na ASIA KILAMBWANDA, Mtwara Wananchi Mkoani Mtwara wametakiwa kutotupa taka hovyo hususani katika maeneo ya pwani ya bahari ya bandari ya Mtwara na badala yake watunze na kuhifadhi maeneo hayo kwa kuwa ni sehemu ya vivutio vinavyoingiza pato la Taifa kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo. "Pwani ya Mtwara imepata athari kutokana na watu wengi kutupa taka hususani mifuko ya plastiki na chupa za maji hali hii inatokana na watu wengi kutokuwa na elimu ya mazingira",alisema Okachu. Kauli hiyo imetokana na katibu wa Occupational safety Health and Environment (OSHE), Melessy Edward Okachu wakati akiongea na waandishi wa Habari katika ofisi yake iliyopo katika bandari ya Mtwara kuhusu ushiriki wao katika kuadhimisha siku ya Mazingira ambayo itafikia kilele chake tarehe 5 mwezi wa 6 mwaka huu. Aidha Okachu amesema kuwa tatizo la uchafuzi wa mazingira linatokana na wananchi kwa idadi kubwa ya wananchi wasio na elimu ya mazingira jambo ambalo amelitaja kuwa changamoto inayotakiwa kufanyiwa kazi kwa haraka. Tafiti zinaonekana kuwa asilimia kubwa ya upatikanaji wa maji yanatokana na uwepo wa mazingira yaliyojitosheleza kwa kukidhi mahitaji hivyo watu wanatakiwa kubuni njia mbalimbali za kukabiliana na uharibifu wa mazingira. Wakati wa uandaaji wa mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini (MKUKUTA wa kwanza na wapili) wadau wa mazingira walijalibu kubuni njia za kukabiliana na uhalibifu wa mazingira mbinu hizo zililenga kupunguza idadi ya watu wanaotuma kuni na mkaa asilimia 90 hadi 80. Aidha athari zinazotokana na kuwepo uharibifu wa mazingira n pamoja na uharibifu wa tabaka la hewa ya ozone, magonjwa ya ngozi , ongezeko la Joto , ukame na mabadiliko ya tabia ya nchi.
|
(Not translated) |
Kugirango ugire icyo uhindura kubyo wasemuye, ugomba kwinjira mu rubuga Injira · Iyandikishe