Log in

/juwassu/topic/106223: English: dM0005E7BA3BB8B000106365:content

« Previous   ·   Next »
Base (Swahili) English

MDAU WA MAENDELEAO UZINI.

Kwa muda mrefu sasa jimbo la uzini limekuwa nyuma katika suala la ELIMU,licha ya kwamba Jimbo hilo lina skuli iliyojengwa zamani tokea enzi za ukoloni kama sikosei shule hiyo ya UZINI imejengwa 1936.Ni skuli chache zilizojengwa katika miaka hiyo ikiwa ni pamoja na Ndijani kwa Wilaya ya kati,Makunduchi na Muyuni kwa Kusini Unguja.

Skuli ya Uzini imebahatika kutoa wasomi wengi ambao wamehudumu katika nafasi mbali mbali katika Serikali ya SMZ na SMT.Hata hivyo kwa kipindi kirefu sasa kada ya Elimu jimbo la uzini kwa imekuwa inasuwasuwa licha ya kuongezeka kwa skuli nyingi ikiwa ni pamoja na KIBOJE,BAMBI,UMBUJI,MPAPA,MCHANGANI NA GHANA.Skuli ambazo ni msingi na sekondari hadi sekondari ya juu.Hata hivyo sekta hiyo haina mafanikio kwa sasa kwani watoto wengi wamekuwa wakiishia kidato cha pili ambayo ndiyo elimu ya lazima na baada ya hapo vijana wengi imekuwa hawana la kufanya na matokeo yake kuwa wanazurura tu.

Nimefarajika kuona kuna JUMUIYA HII YA JUWASSU ambayo inajishughulisha na maendeleo ya ELIMU kwa vijana wa Uzini,pengine Jumuiya hii inaweza ikawa chachu ya maendeleo ya ELIMU UZINI.Inaweza kutoa mchango mkubwa katika kuleta mapinduzi ya ELIMU Uzini.

Hata hivyo najuwa jumuiya hii najuwa inachangamoto nyingi sana .Kwanza ni suala la "Recognition".Hapa nakusudia ili jumuiya iweze kufanya kazi ni lazima iwe imekubalika kwa walengwa na hapo ndipo itakapopata"LEGITIMACY" ya kufanya kazi zake sawa.Suala jengine ni Uwezo wa kujiendesha kwa jumuiya hii,hapa namaana uwezo wa kifedha wa jumuiya kwani bila ya fedha hakuna kinakachofanyika.Suala jengine ni Moyo wa kujitolea kwa wahusika pamoja na jamii inayohudumiwa .Vilevile suala la kuungwa mkono na jamii inayohudumiwa ni muhimu sana kwani bila ya hilo kazi hiyo haitakuwa na mafanikio kwani lengo ni kuwasaidia vijana hivyo jamii ya vijana hao lazima ikubali.

Ombi langu kwa wanauzini,nikwamba kuikubali jumuiya hiyo kwa kuiunga mkono ili iweze kufanya kazi zake kama ilivyokusudia.Pia kutafuta mbinu za kuiwezesha kifadha ili kazi zilizokusudiwa zisikwame.Vile tuwe tayari kuhimiza vjana wetu na kuhimizana wenyewe kwa wenyewe ili kuhakikisha tunaiwezesha jamuiya kufanya kazi ya kuwasaidia vijana hao katika sekta hiyo ya elimu .Vijana tuwe tayari kushiriki kikamilifu katika mikakati ya jumuiya hiyo ili malengo yaweze kufikiwa hasa ukitilia maanani kuwa sisi ndio walengwa.

MWISHO NISEME UZINI ITAJENGWA NA WANA UZINI,HATUJACHELEWA,TOA  MCHANGO WAKO ILI KUFIKIA MLENGO.

HEKO JUWASSU,MSIKUBALI KURUDI NYUMA.

 

 

(Not translated)

In order to edit translations, you need to log in. Log in · Register