Base (Swahili) | English |
---|---|
MED YAANZISHA MFUKO WA ELIMU YA SEKONDARI CHIDACHI Na. Barakaely Christopher Shirika la Marafiki wa Elimu Dodoma (MED) kwa kushirikina na wananchi wa kata za Kikuyu Kusini na Mkonze Manispaa ya Dodoma wameanzisha mfuko wa kuwalipia ada na michango mingine wanafunzi wote watakaofaulu mtihani wa darasa la saba na kujiunga na elimu ya sekondari kutoka shule ya msingi Chidachi. Lengo la mfuko huo ni kuwahamasisha wanafunzi wa shule ya msingi chidachi kuongeza juhudi kwenye masomo yao na kuwa na uhakika wa kuendelea na elimu ya sekondari. Muasisi wa mfuko huo Bw. Davis Makundi ambaye pia ni Mlezi wa shule ya Msingi Chidachi na Mratibu wa Shirika la Marafiki wa Elimu Dodoma (MED) alianza kampeni ya kuanzisha mfuko huo Septemba mwaka jana katika mahafali ya nne ya darasala la saba ambapo mgeni rasmi alikuwa Meneja wa Benk ya Posta Tanzania Bw. Emmanueli Gyumi aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania. Katika mkutano huo wazazi wa wanafunzi wa shule ya msingi Chidachi uliofanyika shuleni hapo wameomba mfuko huo uanze haraka na kuazimia kuwa wazazi wote wenye watoto katika shule hiyo wahusike kuchangia uendelevu wake ili kupunguza mzigo wa kusomesha watoto pasi na uhakika kutokana na kipato duni walichonacho. Akaunt ya Mfuko huo itafunguliwa katika Benki ya Posta Tanzania Tawi la Dodoma.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya hiyo Bi. Ashura Mhoji alieleza kuwa shule yake imekuwa ikifanya vizuri kwa kufaulisha wanafunzi kwa kati ya 80% hadi 100% kutokana na mwamko na ushirikiano uliopo baina ya walimu, wazazi, wanafunzi na wadau mbalimbali wa Elimu. Aidha alilishukuru shirika la MED kwa mchango wake mkubwa ambao limekuwa likitoa mara kwa mara katika shule hiyo. MED katika mkutano huo imechangia kiasi cha sh. 150,000 kwa ajili ya madawati na mfuko wa Elimu.
|
MED marks SECONDARY EDUCATION FUND CHIDACHI And. Christopher Barakaely Organization of Friends of Education Dodoma (MED) for superstition and citizens of the county of Kikuyu Africa and Mkonze Municipal Dodoma have set up a fund to pay fees and other contributions all students who passed the test of seventh grade and join secondary education from primary school Chidachi . The objective of the Fund is to motivate students of primary school chidachi increase efforts on their studies and be sure to continue with secondary education. Founder of the fund mr. Davis groups who also is Lord of primary school Chidachi Coordinator Organization of Friends of Education Dodoma (MED) began a campaign to establish the fund in September last year at the graduation of four darasala seven where the guest of honor was the Manager of Benk Tanzania Posts Mr. Emmanuel Gyumi who appeared for the Director General of the Tanzania Postal Bank. During the meeting the parents of students of primary school Chidachi held the school have asked the fund to start soon and planning that all parents with children at the school get involved donate their sustainability in order to reduce the burden of educating children without assurance from the income poor they had. Akaunt the fund opened at Tanzania Postal Bank Branch of Dodoma.
Head Teacher of the School of the Bi. Ashura Interviewer explained that his school has been good for pupils achieving between 80% to 100% due to the awareness and cooperation existing between teachers, parents, students and stakeholders of education. Either he thank MED agency's role which has given regularly at school. MED at the conference contributed a total of shs. 150,000 for desks and Education Fund. |
Translation History
|