Asili (Kiswahili) | Kiswahili |
---|---|
CLUB ZAOMBA MAKTABA, TUISHENI KUNUSURU UFAULU KIDATO CHA IV, 2012 Na. Davis Makundi Wanachama wa Club za Marafiki wa Elimu Dodoma kutoka katika shule mbalimbali Mkoani Dodoma wameomba msaada wa kupata walimu na Maktaba za jamii ili kuwanusuru na matokeo mabaya katika mtihani wa kidato cha nne na kidato cha pili mwaka huu. Wanachama hao ambao ni wanafunzi wa shule za sekondari kutoka katika shule mbalimbali ndani ya Manispaa ya Dodoma wamesema ili kuhakikisha kuwa wanachama wa Club hizo wanakuwa mfano wa kuigwa katika matokeo yao ni vyema uwepo mkakati wa aina yake wa kuongeza ufaulu kwa kuwapatia wanachama hao masomo ya ziada na fursa ya huduma za Maktaba ili kuongeza ufaulu wao. Maombi hayo ya wana Club yamekuja kufuatia uchambuzi uliofanywa na wanachama hao kwa ushirikiano na MED kuhusu kero ambazo zinawafanya wasifanye vizuri kwenye mitihani yao ya kidato cha pili na ile ya kidato cha nne. Wakiongea katika mjadala huo wanafunzi hao wamekiri kuwa juhudi za ziada za kila mwanafunzi zinachangia kwa zaidi ya asilimia 70% kiwango cha 30% kilichosalia kinapaswa kutoka kwa walimu, jamii, wazazi na wadau wengine. "tunajitahidi lakini wadau wengine nao watusaidie kupata vitabu na walimu kwa masomo ya ziada ili tufaulu" alisema Charles Chunga pichani mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya Kikuyu Sekondari. Wakiunga mkono wazo hilo wanafunzi hao walitoa ombi kwa wadau kuchangia uanzishwaji wa Maktaba za jamii na kutafuta namna ya kuwezesha walimu wa masomo ya ziada ili wanafunzi wasio na uwezo wa kujiunga na Maktaba ya Mkoa na malipo makubwa ya tuisheni wapate huduma hiyo kwa gharama nafuu au bure kabisa pale inapo wezekana. ___________________________________________________________________________ MVUA YAEZUA PAA, MABATI YAANIKWA KWENYE NYAYA ZA UMEME Na. Baraka Mosi Mvua iliyoambatana na upepo iliyonyesha juma lililopita imeezua paa la nyumba moja katika Mtaa Sehemu kubwa ya paa la nyumba hiyo lililoezuliwa lilisukumwa na upepo na kutua kwenye nyaya za umeme hali iliyo ufanya mtaa huo kukosa umeme kwa muda wa siku mbili mfululizo. Taarifa zaidi zinasema kuwa hakunamtu aliyejeruhiwa kufuatia tukio hilo lililotokea usimu wa kuamkia jumamosi ya juma lililopita. ___________________________________________________________________________ ULE USEMI WA "MVUMILIVU HULA MBIVU" UMETIMIA Na. Davis Makundi
Akizungumza kwa kujiamini na kuwa na uhakika wa alichikuwa akikisema, Kurwa alituahidi kuwa Ahadi ya binti huyu ilitimia baada ya kuvumilia na kuvuna mbivu zake kwa kufanya mtihani wa kidato cha nne na kuambulia alama 35 ambazo si nzuri kwa wahitimu wetu. Kwa Kurwa yeye angeepuka vipi alama hizi kama darasani wako watatu (wasichana wawili na mvulana mmoja) na shule yake yenye wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne ina walimu watatu? Kurwa Martin na Zainabu Idi wao walipata alama 35 wakati Yasini Ali yeye alipata alama 33 baada ya kupata daraja D katika masomo ya CIV na GEO. Uvumilivu wa vijana hawa na matokeo yao ni kichocheo kwa vijana wote walio katika shule zetu za kata kutambua kuwa licha ya changamoto ya walimu, vifaa, na mazingira magumu ya kujifunzia na kufundishia; wanapaswa kufanya juhudi za ziada ili kufikia malengo yao. ___________________________________________________________________________ |
(Bila tafsiri) |
Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe