Base (English) | English |
---|---|
HIFADHI NA MATUMIZI ENDELEVU YA MISITU Misitu ni nini? Misitu ni ardhi yoyote yenye uoto wa mimea na wingi wa miti ya kimo chochote ivunwayo na isiyovunwa na iliyo na uwezo wa kutoa timbao au mazao mengine yenye kurekebisha hali ya hewa au mfumo wa vyanzo vya maji au yenye kuhifadhi mifugo au wanyamapori Msitu wa hifadhi Hili ni eneo la misitu, aidha kwa uzalishaji wa mbao na mazao mengine ya misitu, ama ni kwa ajili ya ulinzi wa maeneo muhimu yenye lindimaji chini ya udhibiti wa sheria ya misitu baada ya kutangazwa na waziri mhusika. Matumizi endelevu ya misitu Maana ya matumizi endelevu ya misitu Matumizi endelevu ya misitu ni utumiaji wa maliasili zilizopo kwenye msitu pamoja na kuendelea kuzizalisha maliasili hizo bila kuathiri uwepo wake. Katika matumizi endelevu kwa kawaida kiasi kinachovunwa hakizidi uwezo wa eneo lile wa kuzalisha maliasili hizo. Kwa maana hiyo, japokuwa maliasili hizo zinatumiwa, ni rahisi kuwepo kwa ajili ya vizazi vijavyo ikiwa matumizi yake ni endelevu. Namna ya kufanya matumizi endelevu ya misitu Kuna njia mbalimbali za kuhifadhi na kutumia misitu katika njia endelevu kama ifuatavyo: Ushirikishwaji wa wananchi katika kusimamia na kuhifadhi misitu Maana ya usimamizi shirikishi wa misitu Usimamizi Shirikishi wa Misitu (USM) unahusu utaratibu wa kusimamia misitu ambapo jamii inahusika kwa sehemu kubwa katika utekelezaji.Usimamizi huu unaweza kuwa kwenye misitu iliyohifadhiwa ndani ya ardhi ya kijiji au ardhi ya jumla au kwenye misitu ya hifadhi ya serikali Sababu za ushirikishwaji Lengo kubwa la usimamizi shirikishi wa misitu ni kuwashirikisha wananchi katika kuendeleza kuhifadhi na kutumia misitu kwa vizazi vilivyopo na vijavyo. Hapo awali wakati wa sheria za misitu za kikoloni shughuli za kuhifadhi misitu ziliendeshwa kama za kijeshi na hivyo kujenga mawazo kuwa misitu ni mali ya serikali na wananchi hawahusiki. Kutokana na hali hiyo wananchi hawakuipenda misitu iliyowazunguka na walijenga uadui mkubwa baina yao na watendaji wa idara ya misitu matokeo yake uharibifu wa misitu uliendelea kwa kiasi kikubwa. Kwa kuwa watumiaji wakubwa wa misitu ni wananchi wanaoizunguka, serikali iliona ni vyema ikawashirikisha wananchi wake katika swala zima la kuhifadhi ndiyo maana siku hizi wananchi wanashiriki kwenye suala la kuhifadhi misitu kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kutoa maamuzi. Swala la ushirikishaji limeainishwa kwenye sera ya taifa ya misitu (Forest policy) ya mwaka 1998 na sheria ya misitu (Forest Act ya mwaka 2002) Faida za ushirikishwaji Faida za ushirikishwaji wananchi kwenye kuhifadhi misitu zipo nyingi ikiwa ni pamoja na wananchi kushiriki kwenye kufanya maamuzi kuhusu misitu yao, Kupata fursa ya kujipatia mazao ya misitu kama kuni, madawa, matunda na mboga bila vikwazo, wananchi kupewa fursa ya kanzisha misitu yao ya hifadhi kama vile misitu ya hifadhi ya kijiji, ya vikundi na hata ya mwananchi mmojammoja. Kwa upande mwingine serikali inanufaika kwa kuwa inaongezewa nguvu na wananchi katika kuhifadhi misitu. Idadi ya misitu katika Tanzania ni kubwa sana ukilinganisha na idadi ya watumishi wake hivyo kwa kuwashirikisha wananchi wanasaidia katika swala zima la kulinda misitu ili isiharibiwe na wahalifu wenye nia mbaya. Matumizi ya mila za jadi katika kuhifadhi misitu Matumizi ya mila za jadi kama tambiko yamechangia kwa kiasi kikubwa kulinda misitu katika maeneo ya Usambara na sehemu nyinginezo mbalimbali Tanzania kwa kuwa maeneo yanayotumika kwa shughuli za jadi yamekuwa yakipewa heshima ya pekee. Kwa mfano wanavijiji na wazee wa tambiko wamekuwa wakipanga faini kama za mifugo au pombe na hata fedha kwa yeyote aliyejaribu kukiuka kanuni za utunzaji wa maeneo haya muhimu. |
(Not translated) |