Injira

/AUG/post/103320: Kinyarwanda: CM0000FB15D15B0000103366:content

« Inyuma   ·   Ahakurikira »
Base (Igiswayire) Kinyarwanda

Pamoja na mikutano na wanakijiji wa Singino kule Kilwa lakini tulipata bahati ya kutembelea wajasiriamali ambao wanapata kipato chao kwa njia ya uvuvi wa Maliasili za bahari.Wako duni sana hawana vifaa vya kuvulia na ili kuwatoa huko ni kwa kuwafundisha njia hii ya ufugaji wa samaki wa maji chumvi kwa njia ya kitaalamu zaidi ndio maana tumechukua eneo kwa kushirikiana nao basi tuache mazalia ya bahari yasiharibiwe ovyo kwa vifaa duni na badala yake tutumia njia mbadala ya kufuga kwa maji chumvi lakini kwenye mabwawa.angalia wavuvi hawa

Hawa ni samaki wa baharini wanaopatikana huko Kilwa.Tulipata bahati ya kuwala kwa wingi na ni watamu ajabu.

Wavuvi wana vifaa duni vya kuvulia Samaki.Tunawasaidiaje jamani

Vijana wamechoka na wanarudi bila Samaki kwani wangekuwa na Mashua na vifaa vizuri wasingeonekana katika hali hii

Hiki ni kijiji cha Singino Kilwa tulipofanyia mikutano yetu na wana kijiji.

Hapa tunasubiri kuuziwa Samaki wa baharini mwangalie mzee huyu anasema yupo hapa miaka mingi na anafanya kazi hii wakati wote

Hapa ni kwenye mnada wa Samaki wajasiriamali wanakuja kununua samaki

Mama huyu mjasiriamali akikaanga samaki zetu tulizonunua

Kaka yuko Busy akiwaparura samaki tulionunua kweli ni Utalii wa nguvu

Hapa ni Darasani kwenye ofisi za asasi watu mbalimbali wamekusanyika kumsikiliza mkufunzi kutoka Chuo cha Uvuvi Mbegani Bwana Kissai akiwafundisha njia bora na za kisasa za ufugaji wa samaki kwa kutumia mabwawa.

Hapa wanasemina wakishauriana jambo ambalo lilionekana kutokueleweka na mkufunzi msadizi anawaelimisha.

(Not translated)

Kugirango ugire icyo uhindura kubyo wasemuye, ugomba kwinjira mu rubuga Injira · Iyandikishe