Envaya

/top-tanzania/news: English: WIqEFO0FFX5R1Gn5q0ptd6Nb:content

Base ((unknown language)) English
 
MAADHIMISHO YA SIKU YA WAZEE DUNIANI - NGAZI YA KATA - NSHAMBA - BUKOBA. YAFANA.
WILAYA YA KARAGWE IMETANGAZA KAMPENI YA KUANZA KUWAKAMATA WAGANGA WOTE WA JADI AMBAO WANAENDESHA SHUGHULI ZAO BILA KUSAJILIWA KWANI HUDUMA YA BAADHI YA WAGANGA HAO IMEKUWA IKICHOCHEA MAUAJI YA WALEMAVU WA NGOZI ALBINO NA WAZEE AMBAO HUUWAWA KWA VISINGIZO KUWA NI WACHAWI BAADA YA KUPIGIWA RAMLI NA WAGANGA WA JADI.
MWNAHABARI WETU VEDASTO MSUNGU NA TAARIFA ZAIDI KUTOKA MULEBA
MKUU WA WILAYA YA MULEBA LEMBRIS KIPUYO AKIONGEA KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA WAZEE DUNIANI YALIYOFANYIKA KATIKA MJI WA NSHAMBA KATIKA HOTUBA ILIYOSOMWA KWA NIABA YAKE NA KATIBU TAWALA WA WILAYA YA MULEBA NASHON KABABAYE AMESEMA WAGANGA WATAKAOSHINDWA KUJISAJILI KAMA SHERIA INAVYOTAKA WATAKAMATWA NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWANI WANAVUNJA SHERIA NA AMETUMIA FURSA HIYO KUSISITIZA DHAMIRA YA SERIKALI KUHAKIKISHA WAZEE WANAPATA TIBA NA HUDUMA YA AFYA BURE:… nashon kabaye- katibu tawala muleba
MAPEMA KATIKA RISALA YA VIKUNDI VYA WAZEE WA NSHAMBA BAADHI YA WAZEE WAMESEMA MPANGO MZURI UNAOENDESHWA NA SHIRIKA LA WAZEE NSHAMBA UMESAIDIA KUBORESHA MAISHA YA WAZEE KWANI WANAPATA PENSHENI YA SHILINGI ELFU KUMI NA MIA TANO KILA MWEZI KWA KILA MZEE MPANGO AMBAO WAMESEHAURI SERIKALI IANZE KUUTEKELEZA KAMA ZINAVYOFANYA NCHI NYINGI ZA AFRIKA:..
TAARIFA YA SHIRIKA LA WAZEE NSHAMBA ILIYOSOMWA NA ESTHER MAJURA IMEELEZA KUWA SHIRIKA HILO LIMEANZISHA VIKUNDI MBALIMBALI KATIKA JAMII WAKIWEMO WAZEE AMBAO WAMEKUWA WAKIHUDUMIWA NA SHIRIKA NA KUPATA MAHITAJI MUHIMU YA KIJAMII IKIWEMO KUWAJENGEA MAKAZI YA GHARAMA NAFUU:.. esther majura- msoma risala shirika la wazee
MAADHIMISHO HAYO YALIYOANDALIWA NA SHIRIKA LA WAZEE NSHAMBA YALIPAMBWA NA MUZIKI WA ZAMANI AMBAPO WAZEE WENGI WALIJITOKEZA KUBURUDIAKA NA KUJIKUMBUSHA ENZI ZAO:.. upsound
MWISHO



(Not translated)

In order to edit translations, you need to log in. Log in · Register